Pemba yaongoza kwa umasikini Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pemba yaongoza kwa umasikini Zanzibar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Aug 11, 2011.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema kisiwa cha Pemba kinaongoza kwa umasikini wa kipato Zanzibar.

  Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi, Mipango na Maendeleo, Omar Yussuf Mzee, wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Viti Maalumu, Viwe Khamis Abdalah, aliyetaka kujua Serikali imechukua hatua zipi kukabiliana na umasikini unaoukabili ukanda wa Mashariki wa Micheweni.

  Mzee alisema, kuna hatua zimechukuliwa na Serikali kukabiliana na tatizo hilo lililoko Micheweni, Pemba.

  Alizitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kuwasiliana na jumuiya za kimataifa kufanya utafiti na kuanzishwa kijiji cha milenia Micheweni.

  Alisema, baada ya kukubaliwa maombi hayo zilianzishwa programu zikiwemo za kupeleka maji safi na salama na umwagiliaji maji katika bonde la Sawinga na kuanzisha miradi ya ufugaji.

  Mzee alifafanua zaidi kwamba utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia kwa kiasi kikubwa utasaidia kupunguza umasikini kwa wananchi wa Micheweni.

  Alisema, katika malengo ya kutoa taarifa kwa wananchi kimeanzishwa Kituo cha Redio Jamii Micheweni.

  Aliongeza kuwa redio hiyo inafanya kazi ya kutoa taarifa kwa wananchi zinazohusu kilimo na ufugaji.

  HabariLeo | Pemba yaongoza kwa umasikini Zanzibar
   
 2. M

  Mwera JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kinachoshangaza kwanini pemba iwe inaongoza kwa umaskini wakati kwa mwakahuu wa mavuno yakarafuu kilo1 yakarafuu inauzwa kwa tshs 18000 bei iliyotangazwa na serikali?wakati pamba inauzwa 300 kwakilo nasijaskia usukumani wanaongoza kwaumskini?au ni mfumo kandamizi uliojengwa na SMZ miakanenda rudi kuitenga,kuikandamiza na kuidhalilisha pemba?ila sasa ktk serikali ya umoja wakitaifa CUF imewabana walafi wa smz bei yakarafuu imepanda,labda italeta unafuu.
   
 3. M

  Mwera JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kinachoshangaza kwanini pemba iwe inaongoza kwa umaskini wakati kwa mwakahuu wa mavuno yakarafuu kilo1 yakarafuu inauzwa kwa tshs 18000 bei iliyotangazwa na serikali?wakati pamba inauzwa 300 kwakilo nasijaskia usukumani wanaongoza kwaumskini?au ni mfumo kandamizi uliojengwa na SMZ miakanenda rudi kuitenga,kuikandamiza na kuidhalilisha pemba?ila sasa ktk serikali ya umoja wakitaifa CUF imewabana walafi wa smz bei yakarafuu imepanda,labda italeta unafuu.
   
 4. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,808
  Likes Received: 2,581
  Trophy Points: 280
  Msaada world market price karafuu?
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,164
  Trophy Points: 280
  Wapemba ndio wafuga majini, wachawi na watengeneza popobawa, wako busy na ugunduzi wa nguvu za giza, maendeleo na hali bora ya uchumi is not a part of their plans.
   
 6. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2011
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  ..... Pamoja na kujinyoosha chini ya miembe mchana kutwa..!!!.

  Takwimu zinaonyesha kwamba Kisiwa cha Pemba ndio eneo linalopata mvua nyingi kuliko sehemu zote barani Africa.
   
 7. a

  alley omar JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2013
  Joined: Jul 10, 2013
  Messages: 280
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  hao matajiri wote wakubwa wanatoka pemba akina edi zungu, bakhresa lkn kutokana na wananchi kutokuwa na imani na serikali yao ndo hawataki kupeleka maendeleo kule smz imesahau leo mauaji ya kinyama pemba mwaka 2011 kama wamesahau cc tunawakumbusha hatutasahau mpaka mbele ya haki hilo walijue moyoni mwao mungu hana haraka na dhulma tuliyofanyiwa
   
 8. Nyanidume

  Nyanidume JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2013
  Joined: Oct 24, 2012
  Messages: 2,156
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  "Nna n'jomba Oman miyee, kwan wafikir miye N'swaili mi mwarabu bwana, siku yoyote naenda zangu Maskat kwa n'jomba Mafruk Al Harid!". Ndicho kinachowaponza mpaka kuwa maskini, eti wenyewe wanajiona waarabu! wajinga sana hawa jamaa!
   
 9. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2013
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Failure nyingine hii ya Chama Cha Wananchi CUF. Licha ya wapemba kuonyesha upendo kwa hiki chama miaka yote kimeshindwa kuwaletea maendeleo. Hata wakati huu CUF Ina ubia serikalini inawaacha wapemba wanaangamia kwa umaskini huku Lipumba anapewa nishani ya Amani
   
 10. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2013
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,136
  Likes Received: 10,495
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha...Hii imekaa njema sana...
   
 11. hekimatele

  hekimatele JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2013
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 9,489
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Hawa jamaa wanataka kutoka kwenye muungano ili wamiminiwe mafwedha toka Uarabuni na nchi za kiarabu ili watajirike. Miradi yote itakayoanzishwa na serikali ni kazi bure tu. Tangu hiyo miradi mpaka sasa milestone ikoje?
   
 12. kukudume2013

  kukudume2013 JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2013
  Joined: Jan 8, 2013
  Messages: 1,497
  Likes Received: 283
  Trophy Points: 180
  Juu ya umasikini huo huwezi kuona ombaomba km dar
   
 13. s

  salum mabura Member

  #13
  Aug 4, 2013
  Joined: Jun 16, 2013
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashangaa Micheweni imewakilisha PEMBA yote au habari inaendelea? hv ukisema wilaya ya mpwapwa kuna ukame na ni masikini je inawakilisha Tanzania nzima?
  Mm naona watu washaanza kujiona matajiri na kuanza kushutumu mara wachawi, wafuga majini, wasiopenda kufanya kazi!
  Hivi hawajasikia ripoti iliyotoka inayosema Tanzania ndio nchi inayotegemea misaada zaidi ktk bajeti yake Afrika!
  Na ile taarifa inayosema wastani wa kipato ni dola moja kwa siku?
  Ndio maana taarifa ikasema ni masikini zaidi kwa Zanzibar na sio Tanzania!
   
 14. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2013
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,808
  Likes Received: 2,581
  Trophy Points: 280
  God bless Pemba. Pemba will set us free.
   
 15. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2013
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Watu kutwa wamelala misikitini,unategemea kuna maendeleo yatakayokuja kwa style hyo?
   
 16. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2013
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  na baada ya kupata mamlaka kamili wanayodai umaskini huo wa.wapemba ndio utakuwa sababu mojawapo ya kuendelea kubaguana katinya unguja na pemba.
   
 17. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #17
  Aug 4, 2013
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  wewe acha hata mitaa ya tandika kwenye miskiti utakuta wazee wakislamu wamelala wakisubr swala.
   
 18. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #18
  Aug 4, 2013
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  Eh.. lol
   
 19. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #19
  Aug 4, 2013
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  Hebu kwanza mnazungumzia wapemba mnazungumzia waislam.. ?? Wapemba hawanihusu kama waislam mada itanihusu sana
   
 20. Nyanidume

  Nyanidume JF-Expert Member

  #20
  Aug 4, 2013
  Joined: Oct 24, 2012
  Messages: 2,156
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  Huyo bwana hazungumzii wapemba bali amewalenga waislamu, hapa amepatia sababu!
   
Loading...