Pemba: Anusurika kifo baada ya kupigwa mapanga mwili mzima na ndugu yake

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Waswahili husema kikulacho ki nguoni mwako, mkulima mmoja kutoka Kisiwani Pemba, alinusurika kifo baada ya kupigwa na mapanga mwili mzima na ndugu yake ambaye alimkuta akimuibia ndizi shambani kwake.

Bwana Issa ni mkulima mdogo kisiwani Pemba wakati wa tukio hilo, aliigiza kama amekufa ili mwizi ambaye anatoka familia moja na yeye amuache.

Anasema anadhani alitaka kumuua kutokana na aibu ya kuja kufichuliwa kwamba alimkuta akiiba ndizi zake.

Issa ana shamba la mazao mbalimbali ikiwemo ndizi aina ya mkono wa tembo. Siku ya tukio alikua yeye na mtoto wa kaka yake wakichimba mihogo kwa ajili ya chakula cha nyumbani.

Mtoto huyo ndio aliyemsaidia kwa kukimbia kutoa taarifa ya tukio nyumbani.

 
Duuh!! Pole kwake.

Japo pia si ajabu ukasikia hakuna hatua aliyochukulia huyo jamaa na mwisho wa siku wapo ndugu walioshauri yazungumzwe yapate kuisha.

Ugumu wa maisha ndio utabeba lawama zote.
 
Back
Top Bottom