Mbeya: Anusurika kifo baada ya kutaka kumbaka kikongwe wa miaka 80

Mwanongwa

Senior Member
Feb 15, 2023
169
198
Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Alex Mchinja mkazi wa Mtaa wa Mawala kata ya Iduda jijini Mbeya amenusurika kifo usiku wa kuamkia Jana jumapili baada ya kumtaka kumbaka bibi kizee wa miaka 80 ambaye amepooza mwili.

Taarifa zinadai kuwa kwa Mara ya kwanza mnamo mwezi wa nne tarehe 19 kijana huyo aliingia kwenye nyumba ya bibi huyo na kufanikiwa kumbaka kisha kijana huyo alitoroka kuelekea kusikojulikana.

Usiku wa kuamkia Jana kijana huyo akarejea na kwenda tena kwenye nyumba ya bibi huyo kwa lengo la kumbaka tena lakini Bibi huyo baada ya lile tukio la kwanza kutokea wasamalia wema wa Sumaujata walimuamisha huyo bibi.

Baada ya kumkosa Bibi huyo kijana huyo aliingia kwenye chumba cha mtoto wa Bibi huyo ambaye anamatatizo ya kusikia na kuvua nguo zote na kutaka kuanza kufanya tukio la ubakaji,Dada huyo alishituka na kuanza kupambana naye huku akipiga kelele.

Baada ya kuona zoezi limekuwa gumu kijana Alex akiwa uchi wa mnyama akaamua kuruka ukuta na kukimbia lakini wakati anakimbia akakutana na balozi wa mtaa huo ambaye alimkimbiza mpaka akamkamata na kumfikisha kituo cha polisi Uyole huku akiwa amejeruhiwa kwenye maeneo mbalimbali ya mwili wake kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa wananchi.

Watoa taarifa wanadai kuwa imani za kishirikina ndiyo imekuwa sababu kubwa ya matukio ya ubakini na ulawiti jijini Mbeya.

Diwani wa kata hiyo ya Iduda PISHON TALABHANI MWANIBHANZA amesema matukio kama hayo katika kata yake yamekuwa mengi na kila wanapokamatwa watuhumiwa hao wamekuwa wakiachiwa kutokana na ukosefu wa maadili kwa baadhi ya Askari polisi.

Na amedai kuwa mpaka wamefanikiwa kumkamata kijana Alex uliwekwa mtego ambao umefanikisha kukamatwa kwake.

Pia amewataka wananchi wa kata hiyo kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi wa kata na mitaa yake ili kuhakikisha matukio kama hayo hayaendelei kutokea .

#Mwanongwa nimekufikishia.
 
Hao wanaompiga "kijana" huenda na wao wana MADHAMBI MAKUBWA tu tena machafu sana kama vile UFIRWAJI, UFIRAJI, UCHAWII, UHARIBIFU WA WATOTO, INCEST, KUTOMBA DADA WA KAZI, WIZI na UTAPELI.

Lakini wanajifanya kumpiga MBAKAJI.
 
Back
Top Bottom