Pd Karugendo: Kwanini waliitaka sauti yangu?

Pd Karugendo: Kwanini waliitaka sauti yangu?

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
1,959
Reaction score
876
Padri Privatus Karugendo

KWA siku tofauti ndani ya juma hili nimepata simu za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Mwanza wanaojifunza uandishi wa habari, wakiuliza swali lilelile kuhusu rushwa kwenye vyombo vya habari.

Walitaka kujua kama kuna rushwa kwenye vyombo vya habari vya Tanzania, na walitaka mifano na maelezo ya ziada.Sikushindwa kujibu maswali yao, bali niliwaomba wanitumie kwa njia ya barua pepe, ili niyajibu.Hawakutaka pendekezo la barua pepe! Walitaka sauti yangu!

Ni wazi nina mengi ya kuelezea juu ya rushwa kwenye vyombo vya habari, lakini nilisita na sikuweza kuwapatia wanafunzi hao jibu. Walisikitika, walinibembeleza na kuniomba niwasaidie.Najua kabisa inaweza kuwa ni sehemu ya mitihani yao au kazi za mazoezi wanazopewa na maprofesa wao.

Nilikataa, si kwa vile nina roho mbaya na siwatakii mema wanafunzi hao ila baada ya tukio la Wilfred Lwakatare, la watu wenye nia mbaya kutengeneza video bandia hadi mtu kuitwa gaidi na kuwekwa gerezani na kufikishwa mahakamani, na matukio mengine mengi ambayo yameondoa kuaminiana katika taifa letu, ni vigumu kumwamini mtu anayepiga simu na kujitambulisha kwamba yeye ni mwanafunzi wa chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine na angetaka mawazo yako juu ya mambo kadhaa.

Sote tunajua uongo wa simu za kiganjani; mtu anasema yuko Mwanza, wakati yuko Dar es Salaam. Mtu anajitambulisha kuwa yeye ni Juma wakati yeye ni Paulo na mengine mengi.

Kwenye simu anajitambulisha ni mwanafunzi, lakini huku ni mtu mwenye nia mbaya ambaye anataka kutengeneza video juu ya Karugendo. Kesho utasikia Karugendo amesema hivi na hivi juu ya serikali au viongozi wa serikali. Kwa sauti, na kuunganisha picha, kujitetea inakuwa vigumu, kama ilivyotokea kwa Lwakatare, hadi leo hii anasota gerezani.

Kwa kuandika, mtu unaweza kusimama kidete na kufa na maandishi yako, maana Walatini wanasema "kilichoandikwa kimeandikwa".

Binafsi nilikuwa tayari kuyajibu maswali ya vijana hawa wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine kwa maandishi kwa njia ya barua pepe. Wao hawakutaka hilo, bali waliitaka sauti yangu! Kwanini walitaka sauti? Nilijiuliza maswali mengi. Kila aliyepiga simu, aliitaka sauti yangu na wala hakukubaliana na pendekezo la kuandika barua pepe. Watanzania wamezoea ‘cut and paste'.

Kwa mtazamo wangu majibu ya barua pepe yangewasaidia zaidi ya sauti. Tuliona kwenye video ya Lwakatare jinsi sauti na picha vilivyounganishwa. Kila mtu makini anaona wazi kwamba video hiyo imetengenezwa, kwani sauti na picha wakati mwingine haviendani. Lakini serikali haioni hilo, inaona video ni halisi.

Hivyo kama serikali haiwezi kutofautisha video ya kutengenezwa na video halisi, ni lazima tuwe makini tunaongea na nani kwenye simu, maana simu ni mojawapo ya chombo cha kuweza kuchota sauti ya mtu na kuitumia unavyotaka.

Ndiyo maana nimeandika makala hii ili niwaombe msamaha wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine. Kama kweli ni wao, na walikuwa na nia njema, basi wanisamehe.

Tunaelekea kujenga utamaduni wa kishenzi katika taifa letu. Utamaduni wa kutoaminiana, utamaduni wa kuwateka watu, kuwapiga na kuwaumiza, utamaduni wa kusingiziana vitu visivyo vya kweli:
"Ushenzi huu tuliusikia kwenye nchi nyingine za jirani na hasa zinazotawaliwa kidikteta. Sasa umeingia kwetu! Inasikitisha, lakini ndiyo ukweli ulio mbele ya macho yetu.

Jambo la kusikitisha ni kwamba vijana wetu wameukumbatia ushenzi huu kwa nguvu zao zote. Vijana wako tayari kuuza utu wao na uhuru wao ili kuutumikia.

Kitu kibaya kuliko vyote kwa maisha ya mwanadamu ni kupoteza uhuru wake, uhuru wa kuchagua jema na baya, wa kuamua kukubali au kukataa na wa kusimamia mawazo yako. Kupoteza uhuru ni sawa na kupoteza uhai.

Tumesikia kwenye vyombo vya habari vijana wakizua uongo kwamba Dk. Slaa alikuwa na mpango wa kumdhuru Zitto Kabwe kwa sumu.

Dk. Slaa ni kati ya watu wachache wa taifa hili wanaoongozwa na fikra. Huwezi kuongozwa na fikra ukawa na mawazo ya kutoa roho ya binadamu mwenzako. Mtu anayeongozwa na fikra, anapambana kwa hoja na wala si kwa silaha na sumu.

Sote tunamfahamu Dk. Slaa kwa kupambana kwa hoja, na wala huyu si mtu wa kutoa roho za watu. Hivyo vijana wanaolipwa kueneza uongo huu wajue watapoteza yote, wanapoteza uhuru wao na uongo wao hauwezi kushinda maana daima ukweli una nguvu zaidi ya kifo.

Tuliamua kuingia kwenye siasa za vyama vingi ili vishindane kwa hoja na kutangaza sera na itikadi. Wananchi wavutiwe na hoja, wavutiwe na sera na kuvichagua. Lakini utamaduni huu uliozuka wa kuwazushia watu ugaidi na mambo mengine ya kuzua ni ushenzi na ni dalili za woga na kutojiamini.

Katika harakati za kulijenga taifa, hakuna anayetamani kusikia maisha ya mtu binafsi juu ya analala wapi, analala na nani, anakula nini, anavaa nini, anasali wapi, ana sura gani, ni kabila gani. Tunachotaka kusikia ni mchango wa mtu huyu katika kulijenga taifa letu.

Hata kama mtu huyu ni malaya, lakini anatumia umalaya wake kulijenga taifa letu na kulinda usalama na rasilimali za taifa letu. Mtu huyu ni muhimu kuliko wale wanaojiita ni watakatifu.

Matokeo ya utamaduni huu wa kishenzi ni taifa letu kuingia kwenye ushenzi kamili wa kuchinjana na kumwaga damu.

Tumeanza kuulizana juu ya kuchinja. Wakristo wanataka kuchinja, Waislamu wanataka kuchinja! Na hili litaendelea hadi kwenye kilimo. Kama Muislamu hawezi kula nyama iliyochinjwa na Mkristo, na Mkristo hawezi kula nyama iliyochinjwa na Muislamu, ni mantiki pia kwamba Mkristo hawezi kula chakula alichokilima Muislamu, na Muislamu hatakula chakula alichokilima Mkristo. Na itakwenda hivyo kwa kila jambo ndani ya jamii yetu, hadi kuvurugana na kuipoteza amani yetu ya miaka nenda rudi.

Sote tunajua kwamba fedha nyingi zinatumika ili kuwarubuni vijana kuukumbatia utamaduni huu mpya wa kishenzi. Ni bahati mbaya kwamba vijana wetu wanashindwa kujifunza kutokana na matukio ya mataifa mengine; kujifunza kwamba ushenzi huu mwisho wake si mzuri.

Na kutambua ukweli kwamba ushenzi huu haujafanikiwa popote duniani. Watapata fedha za muda; watazitumia; zitakwisha. Matatizo yatakuwa yako pale pale na Tanzania yetu itakuwa pale pale.

Mwalimu Nyerere alitufundisha kwamba fedha si msingi wa maendeleo; ukombozi wa fikra unaweza kutuelekeza kwenye maendeleo, lakini si fedha.

Hivyo katika hali kama hii, nisingeweza kujibu maswali ya vijana wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine kwa simu. Wakitaka nitawajibu kwa barua pepe.

Kupanga ni kuchangua, tumechagua kujenga taifa la kutoaminiana na kutiliana shaka kwa kila jambo. Kama hii ni hatua ya maendeleo, historia ndiyo mwamuzi.

Source: Makala Tanzania Daima
 
Jela hakunogi, hadi padri anaogopa...
 
I like this Man of God. Ni hazina kubwa katika jamii isiyo na mwelekeo na inayohitaji tiba.
 
inatisha. vijana wapumbavu wanahaha kugushi video. bora angewataja tu. mwigulu, kijana mpumbavu, nape kijana mpumbavu.
 
Ya huo ndio ukweli,ccm imetufikisha pabaya,tumekuwa TAIFA la waoga,hofu zimetujaa hadi kufikia kuogopa kusema kweli,watu hatuaminiani tena kwa kuogopa vibaka,wezi,majambazi na sasa watesaji wa ccm waliojawa na hila.UKWELI TUMEPOTEA NA TUNAIZAMISHA NCHI YETU TUKIONA KWA AJILI YA KU-FAIL KWA CCM.
 
Makala nzuri, sijui mtu kama Mwigulu anasomaga vitu kama hivi. Mungu anasema kitu ninachoongoza kumuudhi ni usingiziaji!

Kisasi cha Mungu kwa msingiziaji ni kikubwa sana! Hebu tusubiri tuone matokeo yake, najua wengine GOD ha-exist like Mwigulu
 
Punguza jaziba padri hata kama hukutaja majina lakini sio vizuri kusema vijana wapumbavu tafadhari tumia lugha mbadala kufikisha ujumbe.
 
This man is very intelligent and wise.I wish we could have 20 people in this pathetic CCM government with this kind of vision.Wakola muno waitu.Omukama akubele nakulinde.
 
Natumaini kuwa Pasco naye ataisoma makala hii. Yeye alitaka kutuaminisha, kwa kusisitiza kila anapopata nafasi, kuwa ile tape ya Lwakatare ni "authentic," kama anavyosema mwenyewe
 
Punguza jaziba padri hata kama hukutaja majina lakini sio vizuri kusema vijana wapumbavu tafadhari tumia lugha mbadala kufikisha ujumbe.

Hajatumia lugha kali ila sababu hatujazoea kuambiwa ukweli ,kwani ukweli kwetu ni tatizo.Hivi mtu anayeuza UTU na UHURU wake utamwitaje?Utamwita kijana aliyekosa uzalendo au hekima?Au utamwita Mpumbavu?Maana elimu anayo,Utashi anao,lakini bado anaamua kwa hiari yake kuuza utu wake na uhuru wake ili kumdhuru mtu mwingine kwa sababu ya vipande thelathini vya pesa.Huyu utamwitaje?
 
Nadhani wataalamu wa multimedia wanaweza kutuhabarisha ukweli wa video anayozungumzia.Kwa sasa usimwamini mtu tilia shaka kila kitu ikwezekana hata mkeo mtilie shaka.
 
Tena vijana wanarubuniwa kwa 50000 au laki 4. Kijana kama huyu akipewa madaraka tumekwisha
 
Hajatumia lugha kali ila sababu hatujazoea kuambiwa ukweli ,kwani ukweli kwetu ni tatizo.Hivi mtu anayeuza UTU na UHURU wake utamwitaje?Utamwita kijana aliyekosa uzalendo au hekima?Au utamwita Mpumbavu?Maana elimu anayo,Utashi anao,lakini bado anaamua kwa hiari yake kuuza utu wake na uhuru wake ili kumdhuru mtu mwingine kwa sababu ya vipande thelathini vya pesa.Huyu utamwitaje?

Tety mapadri wanatufundusha kusameana kwa hilo bado msimamo wangu huko pale pale kwa nafasi aliyonayo padri na lugha aliyotumia ni kali mno. Kwa suala la vijana kweli inakatisha tamaa. Sijui nafasi yako tety kwa jamii kwa upande wangu kuwaita wapumbavu bado haitoshi maana ni zaidi ya hapo. Lakini sio kwa padri kuita watu hivyo
 
Well said Padri hawa vijana wanatakiwa kwa siku wawe wanaandikiwa makala za kuwasema angalau kama kumi, namaanisha kila media iwe na special page kwaajili yao. Hii tumeiachia sana tangia tulipoona vijana wakiume wakijihusisha na mapenzi ya jinsia moja ikaja mapenzi ya kulelewa na mama zao sasa soko limeshuka wanajipendekeza kwanjia za kujilipua. Nasema kujilipua maana haya wayafanyayo ni zaidi ya kifo cha gonjwa hatari. Vivyovivyo kwa kina dada nao yaani maisha wanachukulia ni kuhongwa tu na wala si vinginevyo.

Vijana mnatia aibu sana yaani hapa hakuna product nzuri mtakaoiacha miaka ijayo, sababu ndio mnaopandikiza chuki baina ya kizazi hadi kizazi. Mmejifunza matabia yenu sasa mnayaamisha kwa watoto na wadogo zenu na hii dhambi haitawaacha sababu kati yenu hamna atakayeushuhudia uzee kwani mmekuwa mkiusakama na kuona ukishakuwa mzee nikama umelaanika na uzee utawakataa hamtafika umri wa uzee bila mauti kuwachukua tena kwa vifo vya aibu.
 
Ni kweli kabsa.. Sisi vijana ni wapumbavu na washenzi maana tuna shindwa kupambambanua mambo kwa elimu ndogo tuliyo nayo...

Binadamu anae kataa kuitwa mpumbavu hatakaa aelimike ata siku moja...

Vijana tujifunze kutokana na makosa na tubadili.. Utu wako unadhamani sana kuliko M-Pesa kabsa kabsaa

Naomba tusigeuzwe kuwa kondomu inayotumika na kutupwa...

Kijana kumbuka unayafanya hayo na jamii inakuona na jamii hiyo hiyo ndo unaishi nayo..je utaishi salama??
Take care!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Haya yanyofanywa na vijana hivi sasa ndio lile bomu tulilokuwa tukiaswa na wenye akili nyakati zilizopita....Limeshaanza kulipuka taratibu sasa!Tuliambiwa ukosefu wa ajira kwa vijana ni bomu, na serikali ikaaswa kushughulikia hilo, lakini kwa kuwa serikali ya CCM haipo kwa maslahi ya TANZANIA wakaupuuza unabii huo......! Si hivyo tu wameamua kulilipua mapema bomu hilo, kwa kuwarubuni vijana hao (pamoja na elimu zao) kufanya haya wanayoyafanya ili tu wao ( ccm) waendele kubaki madarakani.CCM, inataka kuendelea kubaki madarakani kwa nguvu, tena kwa kutumia damu za Watanzania kama kafara yao. Hya wanayoyafanya ni dhambi kubwa na ni laana mbele za Mungu.Wameua elimu, wameua kilimo, wamewanyima vijana ajira, wanagawa rsilimali zetu kwa wageni bila aibu wala staha, wameua uzalendo na kuthamini taifa letu, wameshindwa kudibiti rushwa, wameua sekta ya nishati, wanafukuza watanzania kutoka kwenye makazi yao ya asili kwa kisingizo cha wawekezaji.........LAKINI BADO WANATAKA KUENDELEA KUTAWALA!
 
Tety mapadri wanatufundusha kusameana kwa hilo bado msimamo wangu huko pale pale kwa nafasi aliyonayo padri na lugha aliyotumia ni kali mno. Kwa suala la vijana kweli inakatisha tamaa. Sijui nafasi yako tety kwa jamii kwa upande wangu kuwaita wapumbavu bado haitoshi maana ni zaidi ya hapo. Lakini sio kwa padri kuita watu hivyo

mimi naona Padri yuko sahihi kabisa kuwaita washenzi na wapumbavu,
suala la kusema awasamehe haina mashika maana msamaha ni mpaka pale mtu anapokiri analotenda si sahihi and not otherwise!
 
Back
Top Bottom