Siku hizi sipeleki kabisa laptop lwa fundi, ikizingua nikikomaa mwenyewe nikishindwa naiacha.
Mara ya kwanza ilikiwa Dodoma nilipeleka kwa fundi kuzuia sauti kuwa inakata kata, niliambulia formating ya hard disk na kupoteza documents na hard disk nikawekewa nyingine mbona. Mpk leo zaid ya miaka 8 lakin document nilizopoteza kwenye ile hardDisk zinaniuma na yule fundi sijawai msamehe.
Mara ya pili kwenyw 2014 hivi nilipeleka laptop yangu hapo machinga complex, screen ilikiwa inawaka na kuzima, kufika jamaa akafungua akacheki akasema mkanda umekufa. Gharama nakumbuka kama alinambia elfu 60 hv na ufundi 75 elfu. Nikamwambia funga nikatoe peza nakuja. Nikatoka nikaja maeneo ya makutano ya msimbazi na uhuru mkono wa kulia ukiwa unaenda mnazi mmoja, kuna sehemu unapenya ndani unapanda jui ghorofani.
Kufika fundi akachek, hapo sasa ikawa haiwaki kabisa kioo, akapima alivojua yeye akasema kioo kimekufa. Hapo kinahtaji kama 180'000 tuweke kingine na ufundi itakuwa kama elfu 30, jumla 210k, [emoji3][emoji3] nikachoka. Lakini wakati anaifungua ndani niliona kuna waya haujachomekwa kwenye pin yake ila sikusema.
Nikamwambia funga nikasake pesa. Nikafika home nikafungua screen mwenyewe, nikaufatilia ule waya nikauchomeka, mara waa kitu kimetiki[emoji3][emoji3][emoji1787][emoji1787] serious mpk leo, laptop kioo hakijawai cheza tena.
Bongo matapeli ni kama yote