Paulo usije kucheza na sisii, una mikono michafu........... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Paulo usije kucheza na sisii, una mikono michafu...........

Discussion in 'International Forum' started by BIN BOR, Jan 15, 2011.

 1. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sina nia ya kumchokoza mtu yeyote aitwaye Paulo (Paul kwa kizungu) bali nimekumbuka wimbo huu wa utotoni uliotusaidia kukumbushana kunawa mikono kabla ya kula.

  Ya majirani zetu tumeyasikia, Rwanda Kagame ananyonga wafuasi wake kama kuku wanavyochinjwa hotelini. Uganda Museveni hataki kukosolewa na mtu yoyote, yupo tayari kuwamaliza makamanda wake wa zamani ili muradi abaki madarakani.

  Lakini hawa ndio wanaokuja kucheza na sisi ktk jumuiya ya Afrika Mashariki, wakiwa na mikono iliyolowa damu. Mikono michafu. Ni bora tuunde jumuiya pamoja na Somalia au Sudani ya Kusini lakini kwa hali ilivyo sasa, Uganda na Rwanda hawana sifa ya kuwa wenzetu katika EAC:
   
 2. October

  October JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Were you serious when you mentioned Somalia?
   
 3. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nipe kashfa ya kiongozi wa sasa wa Somalia, then sitakuwa serious. unajua wakati mwingine tunahukumu tu bila kutafuta picha halisi. Viongozi wa Somalia (wengi wao wanaishi Kenya) wana nia ya kuliendeleza taifa lile, sasa kuna kila El-shabab na mahakama za kiislamu za siasa kali zenye kuzorotesha amani. Na hapa sikumaanisha kuungana na makundi ya kighaidi bali serikali halali. Kwani hatukuwa na uhusiano mzuri tu na Somalia kabla ya 1990? Wengi tulioenda ulaya zamani, tulikuwa tunatua Mogadishu kwanza (Alitalia). Tatizo liko wapi ndugu October? Wasomali wangapi tunao kwetu leo hii, na tena wana vyeo hadi kwenye chama tawala?Ya Somali ni mapito tu...amani inakuja.
   
Loading...