Paula Park na Makala ya Ally Sykes

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
15,441
2,000
PAULA PARK ALIPONZWA NA ALLY SYKES 1986

Hayo hapo chini kwa hakika ni ya kale na yanatufunza matatizo yaliyokuwapo katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Ally Sykes ameacha kumbukumbu nyingi katika historia ya kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hebu tutembee katika Mtaa wa Kumbukumbu.

"Jana hapa Majlis niliweka mkasa wa makala hiyo hapo chini iliyoandikwa mwaka wa 1986 na mama mmoja wa Kiingereza Paula Park na kuchapwa na Africa Events.

Wasomaji walikipenda kisa kile na kuniomba niweke makala yenyewe ili waisome wajue nini kiliandikwa.

Makala ilikuwa kuhusu historia ya Tanganyika.

Mwaka a 1986 takriban miaka 25 ya ukimya baada ya uhuru, Ally Sykes alikubali kufanya majadiliano na mwandishi wa Kiingereza Paula Park.

Park akachapisha majadiliano aliyofanya na Ally Sykes kuhusu ukoo wa Sykes na mchango wao katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Makala ile iliposomwa Ally Sykes akawa anapata simu kutoka kwa marafiki zake na kwa wafanyabiashara wenzake wakitaka uhakika kama yale yaliyoandikwa katika gazeti lile kweli yeye ameyasema.

Haukupita muda mrefu, maofisa wa Idara ya Uhamiaji walimtembelea Park na kumuomba aondoke nchini.

Makala ya Paula Park ndiyo hiyo hapo chini.

Someni kwa furaha."

20210524_225112~2.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom