Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Kwa kweli tunaomba Mh Rais utuletee Makonda Mbeya kabla ya uchaguzi 2025.

Sababu zipo nyingi kuanzia za kisiasa na za kiutendaji.
Hapa kisiasa labda ataweza kumsadia Tulia akarudi bungeni vinginevyo hali inaweza kuwa ngumu.

Huyu ndugu atatusaidia sana Mbeya kupata uchangamfu wa mji, na kulikumba hili jiji liliosahaulika kila nyanja.

Ama wanambeya mnasemaje?
 
Kwa kweli tunaomba Mh Rais utuletee Makonda Mbeya kabla ya uchaguzi 2025.

Sababu zipo nyingi kuanzia za kisiasa na za kiutendaji.
Hapa kisiasa labda ataweza kumsadia Tulia akarudi bungeni vinginevyo hali inaweza kuwa ngumu.

Huyu ndugu atatusaidia sana Mbeya kupata uchangamfu wa mji, na kulikumba hili jiji liliosahaulika kila nyanja.

Ama wanambeya mnasemaje?
Aaah kweli 💯
 
Katika watu wanaotumia muda vizuri kwenye uongozi ni Mh. Makonda.

Anahakikisha akiwa kwenye uwanja wa mchezo wa uongozi wake anajizolea point tatu mapema kabisa.

Wanaotoa point za mchezo katika uongozi ni wananchi.

Huko Arusha tayari kesha chukua point tatu zake.

Hiyo inamaana gani?

Maana yake:
Makonda atakuwepo kwenye uongozi siku zote za maisha yake.
Kama Makonda ni kiongozi bora kwako basi wewe ni mtu wa hovyo kabisa!
 
Katika watu wanaotumia muda vizuri kwenye uongozi ni Mh. Makonda.

Anahakikisha akiwa kwenye uwanja wa mchezo wa uongozi wake anajizolea point tatu mapema kabisa.

Wanaotoa point za mchezo katika uongozi ni wananchi.

Huko Arusha tayari kesha chukua point tatu zake.

Hiyo inamaana gani?

Maana yake:
Makonda atakuwepo kwenye uongozi siku zote za maisha yake.
Naunga mkono hoja.
 
Ki
Wakati tetesi za Uteuzi wa Paul Makonda kwenye nafasi ya Ukatibu Mwenezi wa CCM zilipoibuka na uzi wake kuwekwa humu JF, Nakumbuka Mimi nilitoa comment kwamba "Naomba Mungu habari hii iwe kweli ili kuharakisha Anguko." Nafikiri wahusika walikuwa hawajanielewa, matokeo yake kweli Makonda aliteuliwa, na hatimaye ndani ya kipindi kifupi kabisa akasababisha mtikisiko mkubwa sana kwenye Chama Chao hadi kupelekea Katibu mkuu wao kujiudhuru.

Wananchi wenzangu tukubali ukweli mchungu kwamba Paul Makonda ni mtu asiyefaa kuongoza binadamu, hana hata sifa moja ya kuongoza watu.

Isitoshe, kwa Sasa hapa nchini Tanzania amekuwa ndiye Mkuu wa Mkoa mbumbumbu zaidi kuliko wenzake wote, Rais anapaswa kuondokana naye kwa kumuweka kando.

Kama Rais anaona kwamba haitawezekana kabisa kumuweka kando kutoka ktk Serikali yake, basi amteue Paul Makonda kuwa Balozi na amtume kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mataifa ambayo Sera zake ziko against na nchi ya Marekani pamoja na washirika wake, kama vile nchi ya Korea ya Kaskazini, Myanmar (Burma), Belarus, n.k.
Mkuu kichwa kibovu kile na hakina busara na mbaya zaidi hajui mipaka ya kazi yake.

Hafai kuwa hata balozi wa nyumba 10 maana uwezo wake mdogo sana
 
Ndugu zangu Watanzania,

Katika sherehe za leo zinazoendelea mkoani Arusha na kwa nanmna zilivyofaana na kupendeza na kuvutia na kubwa zaidi kwa namna watu walivyofurika na kumiminika ni haijawahi kutokea katika Historia ya sherehe za Mei Mosi. Hii inabaki katika kumbukumbu ya Mei Mosi iliyohudhuriwa na watu wengi sana kuwahi kutokea katika Taifa letu.

Makonda ni Mwamba na bingwa wa mikakati na Jabali la mipango na hamasa. Jamaa anakubalika na kiongozi mwenye nyota kali sana ya kupendwa na watu pamoja na kuheshimika.leo Arusha imeitikia,kanda ya kaskazini imeamka na kwenda kuungana na Mwamba Makonda katika mapokezi mazito ya ugeni wa kitaifa na watu kutoka maeneo mbalimbali ya Taifa letu.

Kwa hakika ukitaka shuguli yako ipendeze katika jambo lolote lile ,basi wewe mkabidhi kazi hiyo Mwamba Makonda halafu muachie akufanyie kazi.kwa hakika leo Mwamba ameonyesha yeye ni mtu na nusu,ni kipenzi cha wana Arusha na watanzania wote kwa ujumla ,ni kipenzi cha vijana na watu wa makundi mbalimbali na ni kiongozi wa kutumainiwa na kutegemewa kwa Taifa letu.

Ipo siku Mwamba atashika nafasi za juu kabisa za uongozi ndani ya serikali yetu.ipo siku watu wataandamana na kumbeba Mwamba Makonda Mabegani mwao kumshukuru ,kumpongeza na kumtia moyo kwa uchapa kazi wake. Ukimchukia Mwamba Makonda unajiumiza tu maana kwa kadri unavyomchukia ndivyo anavyodhidi kuchanja mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania. Usishindane na aliyepewa kibali na Mungu.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Back
Top Bottom