Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Mumeo huyo
 
Out of Topic.....
Hii dhana ya kwamba Rais hapingwi au hauwezi kupingana na Rais au Kiongozi ndio inayoleta unafiki na Magenge ya Wanasiasa....; Kuondokana na huu Upuuzi na Uchawa na Monarchy System ifike wakati tuwe na Wagombe Huru / Wanasiasa Huru wasio na Chama Pia..., Sababu Mawazo tofauti / mbadala yanakuwa labelled kama Usaliti na tunaendelea kuzalisha Yes Men....
 

Kujua kipi useme, useme wapi, wakati gani, na kwenye mazingira gani, kunahitaji akili ya kiwango fulani. Kama huna hiyo akili utabakia kuropoka chochote, wakati wowote na mahali popote.

Rais Samia ameyataka mwenyewe. Hakuna aliyemlazimisha amteue Makonda kwenye nafasi yoyote ile. Haya ni madogo, asubirie makubwa zaidi. Magufuli aliamua kuachana naye kabisa alipokuja kugundua kuwa aliyekuwa anamwamini alikuwa tapeli. Akaenda kugombea ubunge huku akiwadanganya watu kuwa ametumwa na Magufuli agombee ubunge ili ateuliwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani. Hayati Magufuli alipoambiwa, aling'aka na kusema kuwa yeye hajamtuma mtu yeyote akagombee ubunge. Ndipo akaomba arudi kwenye ukuu wa mkoa, marehemu akamkatalia katakata, wakati huo akiwa tayari amefikishiwa taarifa kuwa jamaa amewatapeli GSM nyumba kwa kuwadanganya kuwa Rais alikuwa ameomba wamjengee, kumbe ni yeye ndiye aliyekuwa anahitaji kujengewa nyumba. Hapo akawa takataka mbele ya JPM.

Samia, takataka aliyoitupa mtangulizi wake, ameiona lulu. Asubirie kashfa zitakazompata kwa kupitia huyu mtu. Atapora magari, fedha na nyumba za watu kwa kutumia jina la anayemwita eti ni mama yake. Rais ameyataka mwenyewe, hajajua kuwa tumbili huwa hafugiki.
 
Hebu fikiria kama ungekuwa unafuatilia maisha yako binafsi kama unavyomfuatilia Makonda Kwa maika mitano TU,ungekuwa mbali kiasi gani ?
 
Kiukweli kauli Ile, ni sawasawa na kuichimbia kaburi CCM
 
Sehemu aliyotolea maneno haikuwa sahihi
Wakati pia hatukuwa sahihi

Sheria pia hairuhusu
 
Makonda kweli nimeamini Ni bashite Hana uweO wa kuelewa mambo


Makonda na sabaya hppy walitakiwa wawe jela
 
Lengo lilikuwa nzuri, lakini umepitiliza muno kusifia.
Anyway jamaa ni jasili sana aisehh..
 
Akaulize familia ya Meya wa Jiji la Mwanza

Familia ya Samweli Sita

Familia ya Rizi Moko
 
Toka jana makonda hajapumzishwa,watu mitandao kila mtu anamnanga makonda,hapa tunaanza kuamini huenda kweli vijana wapo kazini.


2025 tunaenda na mama
Kwa mfumo wa CCM Rais 2025- 2030 ni Samia tu. Labda aseme yeye hapana! Hilo sio jambo linalohitaji mjadala.

Kuhusu Makonda yeye kujadiliwa ni uthibitisho kuwa hafai na ni aibu kwa mtu anayemkumbatia.
 
Habari wana Jf
Kama ilivyo kawaida nimechunguza sana Kwa nini ndugu poul makonda anachukiwa sana,na watanzania wenye huo umri nilioutaja hapo.
Nimegundua ni kupitwa kwa mafanikio,nimekuja kuona wanatanzania kinachotusumbua ni wivu wa mafanikio ya mtu.

Leo hii hata makonda akiongea jema vipi bado watanzania wataendelea kumsakama acheni wivu huo na roho mbaya poul makonda mungu kampa kipaji cha kuongoza watu na anavitu vingi sana kwake na kama watanzania tunatakiwa kujifunza kupitia yeye poul makonda.

Chukua hii Kama hamjui

Kitendo cha Rais @SuluhuSamia kumrudisha Makonda kwenye siasa ni kwasababu kuna mahali amezidiwa nguvu. Makonda ni yule kijana asiye na soni, mwenye kufanya/kuongea yale ambayo wakubwa hawawezi kuyaongea wenyewe.
Hapa, Makonda ni kipaza sauti tu,na anakipawa cha uongozi

Ukweli nimefurahi sana mh rais wetu wa JMT kumchagua poul makonda kurudishwa katika nafasi inatakiwa Tanzania tupate vijana Kama 50 au 100 Kama alivyo poul makonda hii nchi tungekuwa mbali sana.

Watanzania tuigeni mfano kwa ndugu mh.poul makonda tuacheni wivu na chuki tufanyani kazi kutwa tunamtaja makonda bora tungemtaja kwa mema ila Watanzania tunamtaja makonda kana kwamba yeye sio binadamu kila baya anatupiwa yeye.

Watanzania wooote inatakiwa tumuunge mkono poul makonda,huyu ni adhina ya taifa.
Ahsante mh.raisi kwa kumrudisha ndugu poul makonda huyu atakusaidia sana katika kuijenga nchi.

Sisi wengine tumekalia kukosoa na kupiga majungu.
Mungu mlinde ndugu poul makonda
Mungu mlinde mh raisi wetu JMT

NAKARIBISHA MAONI.
KIKUBWA ACHANENI NA WIVU WA PAMOJA NA ROHO MBAYA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…