Paul Makonda ndiye 'Robert Moses' wetu?

Paul Makonda ndiye 'Robert Moses' wetu?

Ngosha akitoka lazima nchi akabidhiwe Muislam. Usisahau huu mzunguko. Japo haujaandikwa lakini unazingatiwa. Lasivyo Mujahidin wataichafua hii nchi
Mumeshindwa kuichafua nchi mashehe wenu wakiwa jela wakifanyiwa uzalilishaji ndo mje muichafue nchi kwa makonda oky tutawaona
 
Hizo habari ni kweli zinasikika ila jpm hatoweza kama ambavyo bwm alishindwa kumuweka fts na pia jinsi jmk alivyoshindwa kumuweka bkm.
Sawa ngoja tusubir lakin nasikia jamaa kashabadili katiba ya chama hakuna wa kumpinga
 
Mi huwa nashindwa kumuelewa, mara Mungu wa Dar, mara mteule wa Mungu. Dah!
 
Kuna mambo niliyasema hapa naona niyakumbushie tu.
 
Niliwahi kuanzisha uzi siku za nyuma nikisema huyu kijana anaandaliwa kuitawala Dar es Salaam kwa jinsi Bwana mmoja anayeitwa Robert Moses alivyoitawala New York. Nakumbuka kuna jamaa mmoja alikuwa anabisha anasema nisimlinganishe kijana kama Makonda na mtu mzito aliyejenga historia kama Robert Moses.

Base ya post yangu ilikuwa kuwa Makonda yupo na ataendelea kuwepo kwa muda mrefu sana na kila mradi wowote mkubwa utapitishwa kwenye ofisi yake na sifa nyingi atakuwa anapewa yeye. Tayari tunashuhudia hayo. Kuna wanaosema amekuwa kama Naibu Rais kwa sababu si cha waziri, Waziri Mkuu au Makamu wa Rais mwenye sauti juu yake. Sitashangaa kuendelea kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa miaka 30 ijayo.

Robert Moses alikuwa na mamlaka makubwa sana, yeye ndiye alikuwa kila kitu na alirundikiwa mavyeo kibao tu. Kwa kiasi ilirahisisha utendaji wake wa kazi kwa sababu iliondoa urasimu. Tofauti kubwa ni kuwa kwa Makonda mamlaka alizopewa hazijarasimishwa. Kila mtu ameshaliona hilo.

Ule uzi nimejaribu kuutafuta siuoni, kwa kweli kuna wakati mods wa JF wanakatisha tamaa sana. Nakumbuka kama walikujaga kuuunganisha na uzi mwingine wa Makonda ambao ulikuwa hauhusiani na nilichokuwa naongelea mimi. Kuna wengine hata tukiwa na nondo ya kuleta humu, huwa tunajiuliza mara mbili mbili na mara nyingi na mara nyingi tunaamua kupotezea tu.


View attachment 695196
Za chin chin zinasema awamu ijayo jamaa ndo wazir mkuu wetu na ngosha akitoka jamaa ndo anakabiziwa nchi
Unamu underated Majaliwa, Yuko kimya lakini atapambana kumzima huyo dogo

Ccm Kuna wazee hawamtaki dogo apande juu atazimwa na apotee kabisa
 
Back
Top Bottom