Paul Makonda ndiye 'Robert Moses' wetu?

Paul Makonda ndiye 'Robert Moses' wetu?

Niliwahi kuanzisha uzi siku za nyuma nikisema huyu kijana anaandaliwa kuitawala Dar es Salaam kwa jinsi Bwana mmoja anayeitwa Robert Moses alivyoitawala New York. Nakumbuka kuna jamaa mmoja alikuwa anabisha anasema nisimlinganishe kijana kama Makonda na mtu mzito aliyejenga historia kama Robert Moses.

Base ya post yangu ilikuwa kuwa Makonda yupo na ataendelea kuwepo kwa muda mrefu sana na kila mradi wowote mkubwa utapitishwa kwenye ofisi yake na sifa nyingi atakuwa anapewa yeye. Tayari tunashuhudia hayo. Kuna wanaosema amekuwa kama Naibu Rais kwa sababu si cha waziri, Waziri Mkuu au Makamu wa Rais mwenye sauti juu yake. Sitashangaa kuendelea kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa miaka 30 ijayo.

Robert Moses alikuwa na mamlaka makubwa sana, yeye ndiye alikuwa kila kitu na alirundikiwa mavyeo kibao tu. Kwa kiasi ilirahisisha utendaji wake wa kazi kwa sababu iliondoa urasimu. Tofauti kubwa ni kuwa kwa Makonda mamlaka alizopewa hazijarasimishwa. Kila mtu ameshaliona hilo.

Ule uzi nimejaribu kuutafuta siuoni, kwa kweli kuna wakati mods wa JF wanakatisha tamaa sana. Nakumbuka kama walikujaga kuuunganisha na uzi mwingine wa Makonda ambao ulikuwa hauhusiani na nilichokuwa naongelea mimi. Kuna wengine hata tukiwa na nondo ya kuleta humu, huwa tunajiuliza mara mbili mbili na mara nyingi na mara nyingi tunaamua kupotezea tu.

View attachment 695196

Mkuu tafadhali tupia hicho kitabu tumsome huyo Moses Robert sababu si mara ya kwanza kusikia mtu akimuongelea.
 
Dah kina kurasa zaidi ya 1,200 ila fanya juhudi ukipate online kama una interest na mambo ya historia, utawala, mipango miji, nk.
 
Ngosha akitoka lazima nchi akabidhiwe Muislam. Usisahau huu mzunguko. Japo haujaandikwa lakini unazingatiwa. Lasivyo Mujahidin wataichafua hii nchi

Na mimi nilitaka kumjibu hivyo ila uwezi jua, yote yanawezekana nchi hii. Kama hadi wafalme wanakuja tunawaomba watujengee nyumba za ibada, labda wanaweza kukubali kusubiri. Ni kuongea tu na BAKWATA.
 
Beira Boy Inaonekana hstoria ya nchi huijui vzuri wewe. Japo syo rasmi ila utakubaliana na mimi kuwa, Rais wa JMT hupokezana kila baada ya miaka 10 kwa dini.. Hvyo 2025 mgombea urais lazima awe muslim (siyo rasmi kikatiba) ila ndo ukweli

Hvyo, P MAKONDA hawez kuwa mgombea urais labda kasimu majaliwa.

Na kama makonda atagombea urais basi ni 2035

Pia, ukumbuke, Rais wa JMT aktoka bara lazma VP atoke zenji.
 
Niliwahi kuanzisha uzi siku za nyuma nikisema huyu kijana anaandaliwa kuitawala Dar es Salaam kwa jinsi Bwana mmoja anayeitwa Robert Moses alivyoitawala New York. Nakumbuka kuna jamaa mmoja alikuwa anabisha anasema nisimlinganishe kijana kama Makonda na mtu mzito aliyejenga historia kama Robert Moses.

Base ya post yangu ilikuwa kuwa Makonda yupo na ataendelea kuwepo kwa muda mrefu sana na kila mradi wowote mkubwa utapitishwa kwenye ofisi yake na sifa nyingi atakuwa anapewa yeye. Tayari tunashuhudia hayo. Kuna wanaosema amekuwa kama Naibu Rais kwa sababu si cha waziri, Waziri Mkuu au Makamu wa Rais mwenye sauti juu yake. Sitashangaa kuendelea kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa miaka 30 ijayo.

Robert Moses alikuwa na mamlaka makubwa sana, yeye ndiye alikuwa kila kitu na alirundikiwa mavyeo kibao tu. Kwa kiasi ilirahisisha utendaji wake wa kazi kwa sababu iliondoa urasimu. Tofauti kubwa ni kuwa kwa Makonda mamlaka alizopewa hazijarasimishwa. Kila mtu ameshaliona hilo.

Ule uzi nimejaribu kuutafuta siuoni, kwa kweli kuna wakati mods wa JF wanakatisha tamaa sana. Nakumbuka kama walikujaga kuuunganisha na uzi mwingine wa Makonda ambao ulikuwa hauhusiani na nilichokuwa naongelea mimi. Kuna wengine hata tukiwa na nondo ya kuleta humu, huwa tunajiuliza mara mbili mbili na mara nyingi na mara nyingi tunaamua kupotezea tu.

View attachment 695196
Hizo nondo zako ni zipi? Wahaya kwa misifa hamjambo!!
 
Konda amepewa uwanja mpana wa kujivinjari hata zaidi ya baadhi ya mawaziri, na hata akienda kinyume katika baadhi ya maamuzi yake hakuna mwenye ubavu wa kuhoji, na hii inapelekea saa zingine naona bora aongezewe nguvu zaidi ikibidi hata kuweza ku deal na mawziri wasio jitambua ambao wao kila jambo ni ndio mzee,.
 
Makonda ana nguvu kubwa kabla hata ajaukwaa ukuu wa Mkoa wa Dar.
Alimchalanga Warioba bilaaa kujali nyadhifa zake.
Alikuwa DC wa kwanza katika awamu hii kumsweka ndani Mbunge wa Ubungo.
Serikali ya China ilimletea meli yenye Hospitali ya Kijeshi kutibu wananchi wa Dar-es-Salaam.baada ya yeye Makonda kuiomba serikali ya China.
Alianzisha kampeini ya kuwataja majina watu maarufu waliojihusisha na madawa ya Kulevya.
Amefuata mabaraza ya nyumba.
Ni vigumu kujua nani alimpa nguvu hizo,na kwanini anajiamini mno.
 
Niliwahi kuanzisha uzi siku za nyuma nikisema huyu kijana anaandaliwa kuitawala Dar es Salaam kwa jinsi Bwana mmoja anayeitwa Robert Moses alivyoitawala New York. Nakumbuka kuna jamaa mmoja alikuwa anabisha anasema nisimlinganishe kijana kama Makonda na mtu mzito aliyejenga historia kama Robert Moses.

Base ya post yangu ilikuwa kuwa Makonda yupo na ataendelea kuwepo kwa muda mrefu sana na kila mradi wowote mkubwa utapitishwa kwenye ofisi yake na sifa nyingi atakuwa anapewa yeye. Tayari tunashuhudia hayo. Kuna wanaosema amekuwa kama Naibu Rais kwa sababu si cha waziri, Waziri Mkuu au Makamu wa Rais mwenye sauti juu yake. Sitashangaa kuendelea kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa miaka 30 ijayo.

Robert Moses alikuwa na mamlaka makubwa sana, yeye ndiye alikuwa kila kitu na alirundikiwa mavyeo kibao tu. Kwa kiasi ilirahisisha utendaji wake wa kazi kwa sababu iliondoa urasimu. Tofauti kubwa ni kuwa kwa Makonda mamlaka alizopewa hazijarasimishwa. Kila mtu ameshaliona hilo.

Ule uzi nimejaribu kuutafuta siuoni, kwa kweli kuna wakati mods wa JF wanakatisha tamaa sana. Nakumbuka kama walikujaga kuuunganisha na uzi mwingine wa Makonda ambao ulikuwa hauhusiani na nilichokuwa naongelea mimi. Kuna wengine hata tukiwa na nondo ya kuleta humu, huwa tunajiuliza mara mbili mbili na mara nyingi na mara nyingi tunaamua kupotezea tu.

View attachment 695196
hicho kitabu ndo ulitakiwa kuweka hapa.
 
.......Ni vigumu kujua nani alimpa nguvu hizo,na kwanini anajiamini mno.

Jiongeze kidogo utajua ni nani amempa hizo nguvu. Ukihakikishiwa kwamba wewe ni untouchable, hata wewe kujiamini kwako kutaongezeka sana tu.
 
.......Konda amepewa uwanja mpana wa kujivinjari hata zaidi ya baadhi ya mawaziri.....

Tegemea kwamba around 2023 atafarakana na bosi wake. Hiyo itapelekea kupoteza kwa muda ukuu wake wa mkoa wa Dar es Salaam. Itakapotokea, kuna uwezekano akapelekwa mkoa mwingine na atarudishwa baada ya uchaguzi.

Makonda hatakuja kuwa Mbunge, Waziri au Raisi.
 
Vipi ameshampa nyumba yule jamaa aliyetobolewa macho man scorpion au ndio ilkuwa publicity
 
Chakula chake hicho hapo nyuma kuna MTU amemuweka karibu ili akifaidi tu
 
Za chin chin zinasema awamu ijayo jamaa ndo wazir mkuu wetu na ngosha akitoka jamaa ndo anakabiziwa nchi
Hizo habari ni kweli zinasikika ila jpm hatoweza kama ambavyo bwm alishindwa kumuweka fts na pia jinsi jmk alivyoshindwa kumuweka bkm.
 
Back
Top Bottom