SI KWELI Paul Makonda asema kuwa Mwandishi wa Habari lazima uwe na leseni kuandika habari za Serikali

SI KWELI Paul Makonda asema kuwa Mwandishi wa Habari lazima uwe na leseni kuandika habari za Serikali

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Kumekuwepo Na Chapisho Linalo Sambaa Kwenye Mitandao Ya Kijamii Hasa Facebook Likiwa Na Ujumbe Kwa Vyombo Vya Habari.Je Lina Ukweli Kiasi Gani?

Hii Ni Nukuu Ya Ujumbe huo ""Baada yakuteuliwa kuwa waziri wa habari, Makonda kaja na Sheria mpya. Mtu yoyote ili aweze kutoa taarifa ya serikali ni lazima awe na leseni, kinyume Cha hapo unaenda segerea miezi 6 au faini ya milioni tano.

"Ni Marufuku kuandika taarifa yoyote ya serikali kwenye mitandao wowote wakijamii au kuongea redioni bila leseni, ukifanya ivyo unakuwa umefanya kosa la jinai"

1767969385288.jpg

~Paul Makonda.
 
Tunachokijua
Januari 08, 2026 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alifanya mabadiliko katika baraza la Mawaziri na miongoni wa mabadiliko aliyoyafanya ni kumpandisha Paul Makonda kutoka kuwa Naibu waziri wa Habari, michezo, sanaa na utamaduni kuwa Waziri Kamili.

Madai

Saa chache baada ya uteuzi huo kuliibuka taarifa inayodai kuwa Waziri huyo mteule ameelekeza kuwa ili uandike habari yoyote kuhusu serikali lazima uwe na leseni la sivyo utahukumiwa jela miezi 6.

Uhalisia wa Madai hayo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejirirdhisha kuwa hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo ama kumnukuu kiongozi huyo.

Hata hivyo Paul Makonda bado hajaapishwa kuwa Waziri kamili wa wizara hiyo ambapo uapisho unatarajiwa kufanyika Januari 13, 2026 hivyo hadi kufikia sasa bado waziri wa wizara hiyo nia Profesa Palamagamba Kabudi.

Ingawa Tanzania inayo bodi ya Ithibati (JAB) ambayo inatoa ithibati kwa watu wanaotaka kufanya shughuli za uandishi wa habari lazima watimize vigezo vilivyowekwa ikiwemo vya kitaaluma ili kupata leseni ama Ithibati hiyo.
Awaonyeeshe hawa wanaharakati uchwara kutwa kucha kubumba uwongo na upupu mitandaoni
 
Afadhali huyu ameamua kuuonyesha udikteta wa samia wazi, na huyu atamsukuma samia hadi korongoni, sijui kama naye ataangukia humo, ila atahakikisha samia amezama kabisa, na asiweze kuinuka tena, huyu atatusaidia sana.
 
Back
Top Bottom