Paul Makonda anza kufanya 'Mazoezi' ya Kuishi 'Jela', kwani Waziri mpya wa Habari Nape hakuachi na kawekwa hapo 'Kimkakati' zaidi

Haya Jirani wa pale Kwako Mbezi Beach ukiwa umepakana na Hekalu la Tajiri wa Kihaya Katunzi na Mtoto wa Mjini Nape Nnauye Mungu akupe nini tena Komredi?

Kama kuna Kitu ambacho Waziri Nape utakifanya na Mimi GENTAMYCINE kukifurahia na Kuunga mkono tena kwa 100% ni Kwanza Kumshughulikia Ndugu Paul Makonda ( aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ) kwa Kukufanyia yale Madhila yote ukakoswakoswa Kupigwa Risasi ya Utosini pale maeneo ya St. Peters Oysterbay.

Tafadhali Nape usimcheleweshe huyu 'Gaidi na Fisadi Matege' bali upesi sana andaa Mtu akafungue Kesi ya Kuivamia CMG ( Clouds Media Group ) au Shirikiana na Saed Kubenea ambaye alishaanza Mchakato wa Kumfungulia Kesi ili akamatwe upesi Kesi ianze dhidi yake kisha baada ya hapo tutawaomba na wale Wengine aliowaumiza Kimaslahi ( hasa Kiuchumi ) kwa Kuwaonea akina Yusuf Mehboub Manji warejee Tanzania nao wamfungulie Kesi ili hatimaye akaozee kabisa Gerezani.

Halafu Comrade Nape ukiapishwa tu Kesho hapo Dodoma 'Kudadadeki' ukiingia hapo Ofisini Kwako Wizarani anza Kufyagia hapo Watendaji ( Maafisa ) ambao ni Sita ( 6 ) kwani ni Wanafiki na Kipindi kile 'Ulipotumbuliwa' walifurahi na Kufanya Bonge la 'Pati' maeneo ya Mikocheni na wakawa wanakusema vibaya na Kukuzidishia Uadui na aliyelala mazima pamoja na Wasaidizi wake.

Nape usipodili na Makonda ( hasa kwa Wewe pia Kumlipizia Kisasi kwa aliyokufanyia ) basi 'Ushkaji' nawe utafikia Kikomo kwani Watu tuliokuwa tukikupenda mpaka Kukuunga mkono ( GENTAMYCINE ) nikiwemo tuliumia na Kusikitika mno 'Ulipotumbuliwa' kwa Chuki tu za Mtu ( Watu ) wakati hukuwa na baya na tena ulikuwa ni mpenda Haki na Usawa kwa wana Tasnia na Watanzania wengi.

Hongera mno tu Nape kwa huu Uteuzi!!
Pamoja na kumpongeza Nape,jambo ambalo ni jema, ujue visasi ni tabia ya kihutu.
Msiturudishe tulikotoka.
Kama kuna kesi ya jinai au madai basi aliye athirika ndiyo aende kudai haki.
 
Sasa a-deal na Makonda kwa kutumia mamlaka ipi?! Kwamba, akiwa kama Waziri wa Habari apeleke shauri mahakamani la Makonda kuvamia Clouds, au?!
Hahaaa!!hujui kama kuna ile ripoti ya kuhusu makonda kuvamia clouds?juzi juzi alipoulizwa waziri yule mama, akasema serikali inaipitia kwanza?!!sasa nape ndio anaenda hapo unafikiria kama kweli amewekwa kimkakati, si ndio sehemu ya kuanzia?akishasema tu ile ripoti inaonyesha makonda alifanya makosa si tayari ameshamtoa sadaka?
 
Juzi wakati anamsema spika alisema juu ya kuunda baraza la mawaziri, labda kama ni hotuba nyingine, lakini kwa ma Rc, Dc, Rac, Das, na wakurugenzi alishafanya mabadiriko makubwa sana, japo haimuzui tena kufanya.
Basi itakuwa nilinukuu vibaya! Ngoja niitafute nijiridhishe!
 
Hahaaa!!hujui kama kuna ile ripoti ya kuhusu makonda kuvamia clouds?juzi juzi alipoulizwa waziri yule mama, akasema serikali inaipitia kwanza?!!sasa nape ndio anaenda hapo unafikiria kama kweli amewekwa kimkakati, si ndio sehemu ya kuanzia?akishasema tu ile ripoti inaonyesha makonda alifanya makosa si tayari ameshamtoa sadaka?
Saingine Nauye si mtu wa visasi anaweza kupotezea tu, Kama Mandela waliomfunga,
aliwapa madaraka alivyo kuwa Raisi.

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Hahaaa!!hujui kama kuna ile ripoti ya kuhusu makonda kuvamia clouds?juzi juzi alipoulizwa waziri yule mama, akasema serikali inaipitia kwanza?!!sasa nape ndio anaenda hapo unafikiria kama kweli amewekwa kimkakati, si ndio sehemu ya kuanzia?akishasema tu ile ripoti inaonyesha makonda alifanya makosa si tayari ameshamtoa sadaka?
Hakuna cha kumweka kimkakati wala nini, na kama kimkakati basi mkakati huo HAUWEZI kuhusiana na Makonda!! Kwani alilazimika kuwekwa nani na wizara ipi ili Sabaya kumsweka "Segerea"?

Makonda kwa sasa ni mweupe sana... ni ama wameamua tu kumpotezea au wanamtafutia patakapouma zaidi!! Kwa issue ya Clouds haiwezi kuwa "panapouma zaidi" kulinganisha na umafia ambao aliufanya!!
 
Sabaya utamlinganisha na makonda kwa mama?kwanini kubenea hadi sasa ameamua kwenda juu baada ya zoezi lake la kumfungulia kesi kugonga mwamba kwenye mahakama ya kinondoni?!!lazima itafutwe ignation point, moto uwake!!
 
Back
Top Bottom