Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Tulielezwa kuwa wenye mamlaka ya kutangaza wagonjwa wa corona nchini ni watu watatu, ambao ni waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, waziri mkuu Kassim Majaliwa na Rais mwenyewe, John Magufuli
Upande wa Zanzibar, anayeruhusiwa kutoa ripoti yoyote ya wagonjwa wa corona, ni waziri wa afya wa huko, Hamad Rashid Mohammed
Kinachosngaza ni kuwa imetolewa taarifa na wizara ya habari Zanzibar, kuwa imemsimamisha kazi kwa miezi 6, mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Talib Ussi, kwa madai kuwa ametoa ripoti ya mgonjwa wa corona, bila ridhaa yake mwenyewe ugonjwa, ambayo wizara hiyo imesema ni kinyume cha sheria, kwa kuwa huko Zanzibar, anayepaswa kutoa ripoti hizo ni waziri wa Afya wa Zanzibar pekee.
Nimekuwa nikijiuliza maswali kadhaa, je sheria zetu zina double standards?
Kwa kuwa siku za hivi karibuni, mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda, alifanya kosa la aina hiyo hiyo, kwa kumtangaza mgonjwa wa corona hadharani, ambaye ni mtoto wa Mbunge wa upinzani, Mheshimiwa Mbowe, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yake!
Hata waziri wa Afya alipoulizwa baadaye alilisitiza hilo kuwa wenye mamlaka ya kuwatangaza wagonjwa wa corona kwa upande wa Tanzania bara , ni yeye mwenyewe waziri wa afya, waziri mkuu, Kassim Majaliwa na Rais mwenyewe, Mheshimiwa John Magufuli
Ndipo hapo ninapojiuliza, inakuwaje mwandishi wa habari wa Tanzania Daima, asimamishwe kazi kwa kosa tunaloambiwa ni la kumtangaza mgonjwa wa Corona, bila ridhaa yake, wakati Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, akifanya kosa hilo hilo, lakini akiachwa bila kuchukuliwa hatua yoyote?
Huu utekelezaji wa Double standards wa sheria zetu, kwa maana ya upendeleo kwa baadhi ya watu, ndiyo unaoelekea kuliangamiza Taifa letu la Tanzania