Paul Chizzi amuumbua Mwakyembe


Thanks. Mwaki hapo alichemka. Pia kwa namna alivyokuwa anaongea na staff wa ATCL not proper. Alitumia lugha za kihuni. Hopeful marafiki zake wameshamweleza.
 

Mkuu, si kama namtetea Chizi la hasha najaribu kufikirisha kichwa kidogo....hivi unajua ukitaka kununua uniforms locally utapata wazimu, maana utaletewa quotations za ajabu mno! Wabongo si wakweli hasa kwenye eneo la manunuzi. Mie binafsi nashughulika sana na eneo hilo la manunuzi, kununua uniform China was a good idea, kwani hata kama ni nembo ye TZ au batiki, vitenge whatever unavyotaka ndivyo China watakavyokufanyia ili mradi upeleke design. U$ 200 - 600 per uniform si mbaya kwani what matters ni quality. Uniform per person means nguo, viatu, skarf, tie, bags, badges and related. Pia kuingia kwenye soko la ushindani kwenye airlines si kitu cha mchezo kama wengine wanavyodhani eti washonewe batik etc. Wakitoka na pamba dhaifu nyie hao hao mtaanza kuponda tena mkilinganisha na makampuni mengine ya ndege. Wabongo bana...!

Hoja hapa tunajadili Chizi alivyokanusha tuhuma za Mwakyembe. Tatizo viongozi wa TZ mara zote wanakurupuka mambo yanapoharibika. Jiulizeni nani alimteua Chizi? Matatizo ya ATCL hayakuanza na Chizi, hata yeye ameyakuta, wizi na ubadhirifu uliokithiri, kulindana na kupeana ndio mfumo unaoisumbua nchi yetu kwa sasa. Wanasiasa ni wanafiki sana, wanatafuta pa kupumulia na kuwatoa wengine makafara. Nini kazi ya Usalama wa Taifa? ajira za siku hizi hakuna vetting? Tusilalamike tu, tutafute pia kiini cha tatizo!
 

Kwenye list yako ya wapenda mijisifa muongezee Sitta na Membe...hahahahaa!

Kiukweli hata kama Chizi alikuwa na matatizo yake Mwakyembe alikurupuka. Kwani Chizi alijiteua? Mbona KM Omar Chambo muasisi wa madudu yote ktk wizara hiyo haguswi?
 

Precisely!!!
 

Your suppose to be great thinker, KASOME TENA HABARI.
 
Hawa watu wameshaiba hela nyingi sana,ndio maana hizo dola 18,000 anaziona ni ndogo.
 
Wewe C__r__s una hasira mno na mbunge wako. mpe muda anaelekea kujirekebisha.
 

OK, kuna makosa katika gharama za uniform:

(a) Je, vipi ile ndege iliyokodiwa kutoka Liberia? Yaani katika sehemu zote za dunia, eti mtu anaenda kukodi ndege kutoka Liberai, ambako wao wenyewe wanahangaika na usafiri wa anga?
(b) Tanzania tuna wabunifu wengi sana wa kimataifa akina hassanali, na Asya Idaruous; je shirika lilishindwa kuwatumia katika kushona hizo uniform?
(c) Je, siyo kweli kuwa yeye alishastaafu na ajira yake haikufuata taratibu za kisheria?
 
Mimi kusema kweli ningependa kufahamu CV au resume ya Paul Chizi. Jee, ana qualifications gani kwenye mambo ya aviation: kwa maana ya vyuo gani alivyosoma: shahada au stashahada zipi alizofanikiwa kupata; na waajiri gani tokea aanze kufanya kazi baada ya kuhitimu?
 
Dola 18,000/ kwa Batik za wat 15 bado anaona sawa !? Na wale maofisa wawaili waliosimamia zoezii kwa miezi 2, je walitumia Dola ngapi kwa miezim miwili !?
 
OK, kuna makosa katika gharama za uniform:

(a) Je, vipi ile ndege iliyokodiwa kutoka Liberia? Yaani katika sehemu zote za dunia, eti mtu anaenda kukodi ndege kutoka Liberai, ambako wao wenyewe wanahangaika na usafiri wa anga?

Hiyo siyo ishu mkuu! Liberia inatumiwa kama "tax haven" na nchi nyingi kwenye nyanja za usafiri wa baharini na anga kwa nia ya kukwepa kodi, na haimaanishi kwamba vyombo vya usafiri wa baharini au wa anga vilivyosajiliwa Liberia vina ubora hafifu.
 
Hiyo siyo ishu mkuu! Liberia inatumiwa kama "tax haven" na nchi nyingi kwenye nyanja za usafiri wa baharini na anga kwa nia ya kukwepa kodi, na haimaanishi kwamba vyombo vya usafiri wa baharini au wa anga vilivyosajiliwa Liberia vina ubora hafifu.

Kuna taarifa za kutosha kabisa kuwa ndege ile ni bomu; ukitaka zaidi wewe google ATCL+Liberia+Airbus. Ingawa ni kweli kuwa deal lile lilianza zamani wakati wa Makatta, huyu mheshimiwa angekuwa ni mtaalamu na mwenye nia njema na shilika, ni wazi kuwa asingesukumiza dili hilo liendelee, angelilipiga stop. Kuna kila dalili za kutia shaka kuwa huenda kabla ya kustaafu kwake, alikuwa ni mmoja waliokoleza dili hilo, na alipopewa mwanya tu basi akalisukumiza kwa nguvu zote lifanikiwa.
 

Sawa. inawezekana kabisa kwa sababu moja au nyingine kwamba "ndege ile ni bomu", lakini hoja yako kuwa kwa vile tu ndege imesajiliwa Liberia, basi automatically itakuwa na walakini, kwa kweli haina maana. Ndege au meli inaweza kuwa imesajiliwa Marekani ya Kaskazini au kwenye nchi ya Ulaya ya Magharibi lakini ikaonekana kuwa ni mbovu vilevile, na pamoja na yote, gharama zake zikawa za juu zaidi ya hiyo iliyosajiliwa Liberia.
 

Nafikiri kwa mtu yeyote mwenye akili anajua kuwa swala kubwa hapa lilikuwa ni ubora wa ndege. Fortunately kuna uhusiano mkubwa sana wa baina ya ubovu wa bidhaa na kule ilikotoka, ingawa ubora wa bidhaa unaweza usihusiane sana na kule ilikotoka.
 
BA pamoja na kuwa na ndege nyingi wanatumia washonaji wa ndani ya nchi !!, Inakuwa je sisi tunaotumia ndege za kukodi ,matumizi yetu yanakuwa makubwa hivyo?
 
Kama kulikuwa na option ya kushona kwa bei ya chini ambayo ni $ 200 kwa uniform kwa nini hawakuitumia ilhali shirika halina na uwezo mkubwa kwa sasa, mimi haja ni convice hata kidogo $ 18000 still is too much lets be realistic.

Mkuu hawaja nunua uniform 15 kwani huyo idadi ya mapilot ATC inazidi 15 na kila mtu amapata zaidi ya uniform moja ili isiwa kauka ni kuvae
nguo zimenunuliwa nyingi sana
 
Dola 18,000/ kwa Batik za wat 15 bado anaona sawa !? Na wale maofisa wawaili waliosimamia zoezii kwa miezi 2, je walitumia Dola ngapi kwa miezim miwili !?

Mkuu hakuna lolote hapo Mwakiembe kaingia choo cha kike tena baada ya kutulipisha Bilion 94 kwa dowan sasa hivi itakuwa another bilion 9.4 kwa chizi
Chizi yupo entitled na compensasion kutokana na defamation aliyoitoa kwenye magazeti,
 
Huyu bwana asijitetee amefanya hujuma dhidi ya shirika la ndege. kwanini alituma watu kununua sare ulaya badala ya kutangaza tenda?taratibu za manunuzi za umma zinajulikana ,kwanini alizikiuka? hafu zile nguo zina thamani hiyo kweli? hao aliowatuma aliwalipa fedha shs ngapi?shaka yangu ni kwa watu wanao mtetea,kuna nini nyuma ya pazia wakati madudu aliyo ya fanya yako wazi?watanzania bwana!!!!!
 
Mkuu hawaja nunua uniform 15 kwani huyo idadi ya mapilot ATC inazidi 15 na kila mtu amapata zaidi ya uniform moja ili isiwa kauka ni kuvae
nguo zimenunuliwa nyingi sana
taratibu za manunuzi zimekiukwa na zaidi yate maslahi ya shirika hayakuzingatiwa,kwanini mnamtetea? au bado mnaendeleza mapambano ya kule bungeni ya nani kaharibu ulaji wa nanani hapa? tubadilike watanzania bila kutanguliza maslahi ya Nchi yetu tutaiua nchi hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…