Paukwa ……. Pakawa … | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Paukwa ……. Pakawa …

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bikra, May 17, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  May 17, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Paukwa ……. Pakawa … aliondokea chanjagaa mwanangu mwana wa siti kijino kama chikichi …. …………. Naam taim ….!!!!!

  Hakika kilikuwa ni kipindi ambacho tulidiriki kusimama na kutembea kifua mbele iwe katika kambi za Jeshi la Kujenga Taifa ama hata katika sherehe za kitaifa huku tukiimba nyimbo za hamasa kwa kutamka kwa imani zaidi tukisema “Tunaimani na Nyerere .. Oya oya oyaaaa .. Nyerere kweli .. kweli.. kweli .. kweli kweli kweli Nyerere” na kubadilisha jina la kiongozi mwingine kama Karume, Kawawa na hata Moringe.

  Kwa hakika tulitiwa hamasa sana katika utendaji wa mambo mengi na hata kwa namna nyingine kuiga mifano mingi ya heshima na uadilifu wa viongozi hawa. Leo hii nani atathubutu kuimba kibwagizo kama hiki kwa kutia jina la kiongozi wa sasa ambaye hujui baada ya siku chache atakuwa “KILONGOLA” kuongoza wachache ama wengi wa sifa zake ambao kwa imani yao wanakiri kutenda makosa makubwa na mazito kwa “uangalifu” wa dhamana zao walizokabidhiwa?

  Ninasema “uangalifu” tena katika mabano kwa makusudi makubwa ili kutilia mkazo neno ambalo limejiri kinyume cha “uadilifu” katika kutwaa na kuzingatia kanuni za utendaji kazi na hasa katika sekta zetu za umma na serikali.

  Wengi ama jumla ya viongozi wetu katika serikali na sekta za umma siku hizi wamekuwa viogozi na watendaji “waangalifu” – kwa maana kwamba wanaangalia na kuwa makini sana wakati wa kufanya maamuzi ya sekta walizokabidhiwa kwa faida zao binafsi na kwamba kama kuna siku “mtama utamwagwa katika kuku wengi” basi wao watakuwa wa kwanza kusema “mimi nilihusishwa tu na wataalamu na maamuzi yangu yalifuata taratibu na ushauri wa wataalamu hao. Hakika huyu ni kiongozi “muangalifu”. Kinyume na tulikotoka, viongozi wetu walikuwa “waadilifu” kwa maana kwamba hawakukubali tu ushauri wa hao wataalam ili walihimiza kushirikishwa kwa wadau wote na maamuzi yalitolewa pale tu kiongozi alipoamini kwamba kweli linalojiri huu ndiyo ufumbuzi wake na hata ingelikuwa nyumbani kwangu ningefanya vivi hivi kwa mabaya ama mazuri kufurahisha ama kudhuru familia yangu.

  Kwa mtindo huu wa viongozi “waangalifu” umma wetu bado una kazi kubwa sana na yumkini hata midomo kuwa mizito kuimba nyimbo za hamasa kama zile za tulikotoka – Si kazi ya JK pekee bali ni umma mzima wa watanzania sasa kusema na kukubali kwamba tumefikia mahala pabaya kwamba ile IMANI kwa viongozi wetu imetoweka .. (ajabu IMANI hii imetoweka kwa kipindi kifupi sana ukilinganisha na kipindi ambacho tulipitia cha kupambana na maendeleo ya jamii).

  Tuna usemi wa Kiswahili usemao “Samaki mmoja akioza basi ni wote” – Mpaka hivi sasa uozo ambao umetokea bayana wa viongozi wetu wa ngazi za juu kabisa, hauendani na usemi huu? Cha kushangaza zaidi mahakama ya wahusika hawa ni Bunge la Jamhuri ambako mara nyingi hakumu ni kuundwa kwa Tume ambazo huongezea “menthol spirit” kwenye kidonda kipya ili damu iweze kukata haraka na hapo ndipo inakuwa tiba yake, kinyume na mwizi ama kibaka ambaye yeye hukumu yake hufanya katika Mahakama za kisheria na maamuzi huenda yakachukuwa muda mrefu huku muhusika akiwa mahabusu baada ya kuvuliwa haki zake zote na heshima anayostahili kama raia yeyote wa Tanzania.

  Pamoja na mapungufu ya “tulikotoka” bado ningependa kuishi maisha ya viongozi wa kipindi hicho maana nilikuwa nina IMANI nao.
   
 2. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hii nayo ni breaking news? Kweli ni Paukwa pakawa!
   
 3. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hata mi nimeshtuka kidogo1 anyway, good contents! what next?
   
 4. A

  August JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  mimi nime ipenda mada iliyo ongelewa, bila kufuata kibwagizo cha break news, infwact, nilikuwa nafikiria ni jinsi gani ni tawaambia waseme hapana kwa ccm, licha ya ghiliba nyingi za kuseama kwamba, bila wao amani haitakuwepo, pili ndio chama chenye sera bora za kumuokoa mtanzania katika nyanja mbali mbali iwe ya kiuchumi, afya, michezo , elimu, barabara, kupingana na rushwa/ufisadi kulinda mali za watanzania , haki sawa kwa wote etc, kwa sababu wamekuwa na nafasi kubwa za kufanya hivyo katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, lakini kilicho tokea ni matusi na dhuluma kubwa, kwa faida ya wachache ambao wanalindana, kwa maafa ya kiuchumi wa nchi.
  kwa kuanzia na kashfa za chavda, jeetu pate, ukodishaji wa kia iptl wakati wa ali hassan mwinyi, mpaka hizi grand corruption za mkapa na mikataba za mikataba ya madini, radar, ndege ya raisi bot win tower, teuzi ziso fuata maadili, kuuza nyumba za serikali, kuwadhuluma wananchi sehemu za kuchimba madini na kujipa wenyewe kwa mgongo wawekezaji, kujipa mitaji kwa kufunga mikataba mibovu hlafu wanatengue wenyewe na kulipana faida na mengineyo mengi kama miradi ya net group solution, Dowana etc. Kwa kifupi sera za CCm kwa ndani ni za kubinafsisha Nchi kwa Watu wachache, wakati kwa juu juu wanadai hizo sera ni za kumkomboa mtu wa chini.
   
 5. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Tusilaumu sana wakati mwingine huyu yupo kwenye training ground anajaribu kuona different keys zinafanyaje kazi si unajua, Kipya?, hata wewe ukinunua simu mpya utakuwa unajaribu kila function kuona zinafanyaje kazi hata milio utajaribu yote bila kujua unapiga kelele na watu wanakushangaa

   
 6. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Gone are the Good Old Days!
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kweli paukwa.... imekuwa pakawa
   
Loading...