Patrick Mfugale awa Mkurugenzi mpya TANROADS

Patrick Mfugale awa Mkurugenzi mpya TANROADS

Hahahahahahahaha huu ndio uzuri wa JF.......................kutunza kumbukumbu
 
ni kitendo cha kushangaza pale magufuli akibishana na rais kuhusu chief mpya wa Tanroads na magufuli ameweka sharti kwa rais kikwete bila ya MFUGALE yeye anajiuzulu kazi
NOTE kudadeki ndo maana jama anampaisha sana kumbe wamepigiana machapuo toka kitambo
 
Taarifa tulizopata punde ni kuwa Bwana. Patrick Mfugale aliyekuwa Acting Chief Executive wa TANROADS ameteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa TANROADS.

Habari zaidi baadae
sasa hivi kapewa kivuko cha Tazara
 
NOTE kudadeki ndo maana jama anampaisha sana kumbe wamepigiana machapuo toka kitambo
Hayo ni majungu! Ninavyofahamu ni kuwa huyu jamaa siyo mpigaji deal kabisa.
Kuna rafiki yangu mmoja ambaye anamfahamu vizuri sana anasema huyu jamaa ni kichwa kweli kweli na kama angeacha kazi serikalini na kufungua 'consultancy' yake tu angekuwa bilionea wa kutupwa maana karibu madaraja yote makubwa jamaa ndiyo ame-design. Vile vile jamaa siyo mzungumzaji sana na wala siyo mtu wa kujipendeza.
Tatizo kubwa aliokuwa nalo jamaa ni ile tabia ya kutopenda kubambika gharama kwenye miradi na vile vile hata pale TANROAD vijana wake wanajua kuwa jamaa ana macho ya tai. Tabia yake hii ilimfanya asielewane na baadhi ya makatibu wakuu wake. Amejengewa mizengwe mingi sana lakini mwisho wa siku jamaa yuko vile vile.
Mheshimiwa rais [ninavyosikia] wakati anaingia wizarani, alipewa taarifa mbovu kuhusu jamaa. Kwa bahati nzuri, karibu kadiri kila siku zilivyokuwa zikiendelea alianza kumuelewa na kumuamini[ Ninasikia Mh. mpaka akuamini ujue pana kazi kweli kweli.
 
Magufuli alipokuwa Ujenzi wakati ule wa Rais Mkapa..........alikuwa na watu wake muhimu sana.............na wote ni "vichwa".......wa kwanza kwenye list alikuwa Mar Eng. Mujungi (huyu alijiua)........wa pili ni huyu Mfugale..........Mujungi angekuwa hai............by "default" hii ingekuwa nafasi yake..............

Notwithstanding uchaguzi/uteuzi huu wa Mh Magufuli....Mfugale ni qualified for the position na ni mchapakazi..........hongera Eng. Mfugale........
Jamani naomba kujua huyo MUJUNGI alijiua kwa sababu gani
 
ni kitendo cha kushangaza pale magufuli akibishana na rais kuhusu chief mpya wa Tanroads na magufuli ameweka sharti kwa rais kikwete bila ya MFUGALE yeye anajiuzulu kazi
😂😂😂
 
Maisha haya...kwa sasa wote Magufuli na Mfugale, bila kumsahau Kijazi, wote waliohudumu Wizara moja na baadaye Ikulu, wametangulia mbele za haki. Hata hivyo wameacha alama za kudumu kwa utumishi na kujitoa kwao kwa ustawi wa Tanzania yetu. Inshallah Mwenyezi Mungu atawapatia haki yao waliistahili.
 
Tanzania itajengwa na wenye moyo wa dhati wa kutetea nchi yetu na sio wale wa uzao wa watumwa kwenye nchi yetu.
 
Back
Top Bottom