Patrick Assenga arejea CHADEMA akitokea CHAUMMA

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,602
Reaction score
22,706
Aliyekuwa Kada wa CHAUMMA, Patrick Assenga ametangaza kukihama chama hicho na kurejea Chama CHADEMA ambacho kimsingi ni chama alichokitumikia kwa miaka mingi kabla ya kuhama hapo

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Jumanne Mei 26.2026, Assenga amesema maamuzi ya kurejea CHADEMA yamekuja baada ya tafakuri ya kina ambayo ameifanya na kujiridhisha pasipo na shaka kwamba CHAUMMA haina mwelekeo na dhamira ya kweli ya kuiondoa CCM madarakani, badala yake amebaini kuwa CHADEMA ndio chama pekee cha siasa chenye dhamira ya kweli kwa Watanzania na kinachoweza kuiondoa CCM madarakani na kushika Dola

Kupitia mkutano huo na Wanahabari, Assenga amewaomba radhi viongozi wa ngazi mbalimbali wa CHADEMA, wanachama na Watanzania kwa ujumla wake kwa maamuzi aliyokuwa ameyachukua hapo awali ya kukihama chama hicho, akiamini kwamba maamuzi hayo aliyafanya bila kutafakari kwa kina.


Your browser is not able to display this video.

Pia soma
Patrick Assenga avuliwa Uanachama CHADEMA
- Patrick Assenga ajutia kuondoka CHADEMA, amlaumu Boniface Jacob kwa kutokusema ukweli mapema. Amuomba Mungu ampe ujasiri

 
Hamahama!
 
siasa taaluma ya kisayansi sana ndugu zangu,

kuifanya kama biashara ni kujipa usumbufu wa kisaikolojia na umaskini wa kifikra tu
 
Kwa hali ya sasa na kwa namna ya Wasaliti wanavyopiga Magoti kwa CHADEMA kuna haja ya kuanzisha kitengo maalum cha dharula cha usaili wa Wasaliti

Ningeomba pia niwe miongoni mwa Wajumbe wa Kamati hiyo
nani mwenye ubavu wa kumkataa pale chadema kwa mfano kamanda?

na kulivyo na ombwe la uongozi na ukosefu wa agenda,
kuna mtu anaweza kukataliwa kujiunga chadema kweli?

ikitokea,
basi itakua ni unafiki wa kiwango cha juu mno.
 
Ivi huko chadema kuna nini hasa au ndo yale tujenge chama kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…