MUSIGAJI
JF-Expert Member
- Dec 26, 2014
- 2,187
- 2,462
Watanzania wenzangu, hongereni kwa nchi yetu kutimiza miaka 60 ya Uhuru.
Jana katika hotuba Yake kwa Taifa Mh Rais atoa takwimu mbalimbali ya wapi tulipokuwa kipindi tunapata Uhuru na wapi tumefikia baada ya miaka 60 ya Uhuru.
Moja ya takwimu zilizotolewa ni pato la Mtanzania mwaka 2020. Mh Rais ametanabaisha kuwa mwaka 2020 pato la Mtanzania lilikuwa shilingi 2,653,790 kwa mwaka sawa na shilingi 221,149.16 kwa mwezi.
Binafsi takwimu hii, ya pato la Mwananchi limenitafakarisha sana.Ukiangalia hali za wananchi waliowengi achilia mbali kupata shilingi 221,149 kwa mwezi hata kuitengeneza 100,000 ni changamoto kubwa mno, sasa hii ya laki mbili plus kwa mwezi nazidi kutafakari.
Lakini kwa kuwa Mh Rais anazo taarifa kutoka katika ofisini mbalimbali ikiwemo ofisi ya Taifa ya Takwimu, Naomba niwapongeze Watanzania kwa kuwa na uwezo wa kutengeneza 2,653,790 kwa mwaka.
Hongereni kwa Uhuru.