Patakuwa hapatoshi hapa bungeni -BUNGENI

mwanaizaya

Senior Member
Apr 26, 2008
133
1
Patakuwa hapatoshi hapa bungeni

Mwandishi Wetu

Anne Kilango Malecela aliwasha moto mkali wakati akichangia katika mjadala wa Bajeti ya Mapato na Matumizi ya Serikali Juni 19 mwaka huu bungeni Dodoma. Ufuatao ni mchango wake kwa mujibu wa kumbukumbu rasmi za Bunge.

Mheshimiwa Spika kwanza ninaomba mapema kusema naunga mkono hoja.` (makofi)

Mheshimiwa Spika ninaomba niwapongeze mawaziri wote watatu na kwa sababu ninajua wote ni wasikivu na wanaopokea ushauri, watakuwa wanapokea ushauri ambao wabunge tutautoa katika Bajeti hii.

Mheshimiwa Spika, wenzangu wengi wamesema mengi ambayo ningependa kuyasema lakini ninaomba nijikite mahali pamoja tu. Kwanza Serikali nafikiri inaelewa vyema kwamba ili kwamba Taifa lisonge mbele ni lazima mapato ya ndani ndiyo tuyasimamie zaidi. Mapato ya ndani yanapokuwa ni kidogo, tukitegemea mapato ya nje tutakuwa hatuna uhakika na maendeleo ya Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, kwenye mapato ya ndani ndiyo mahali ambako nina matatizo na Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi. Mapato ya ndani hatuyakamui vizuri, kuna sources kubwa za mapato ya ndani ambazo tukizisimamia vizuri, tutakuwa na uhakika wa kusonga mbele.

Mheshimiwa Spika, ninaomba uniruhusu kabla sijaanza kuzungumza, nimnukuu mwanafalsafa mmoja wa Kigiriki aliyekuwa anaitwa Socrates. Wengi mnaosoma vitabu mnafahamu. Siku moja alikwenda sokoni kwenye mkutano wa hadhara akahutubia lakini alisema neno moja kubwa sana.

Kwa ruhusa yako naomba nimnukuu, alisema: “Faithfulness to a cause is the most important thing in life, all great people have been considered great because they died for the causes.” (makofi)

Mheshimwa Spika Socrates alimaanisha kwamba, watu wengi duniani huwa wapo tayari kufa kwa ajili ya kile wanachokiamini ambacho ni ukweli na haki. Ninaomba niongelee ulinzi wa fedha za Watanzania, hiki ni chanzo kikubwa sana cha mapato ya ndani lakini ninaiomba Serikali ikubaliane na mimi kwamba katika ulinzi wa fedha za Watanzania, kwa kipindi kirefu iliacha mwanya.

Serikali iliacha mwanya katika kulinda fedha za Watanzania. Fedha za Watanzania ni fedha za wananchi wa Same, ni fedha za wananchi wa Igunga, Urambo na Kigoma Mjini. (makofi)

Naomba mniangalie ninakokwenda, watu waliingiaje wakachukua fedha za EPA kama kweli Serikali inalinda fedha za wananchi? Hii ni source kubwa sana, ni pesa za mapato ya ndani ni kwamba ulinzi ulikuwa finyu kwa muda mrefu. Iwapo tutaendelea kutokulinda fedha za ndani za wananchi kiasi hiki, kila siku tutakuwa tuna Bajeti ya sungura mdogo, kwa sababu fedha nyingi zitakuwa mikononi mwa wenzetu wachache. Nilitaka kuanza kuzungumzia hapo kwenye EPA. (makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hivi hatutaki wale wabunge ambao tunalitetea Taifa, tuzungumze sana kwa sababu hapa Rais amesimama kidete, amesema pesa ni lazima zirudi na nina imani kwa Mtanzania yeyote anayejua maana ya Rais, atazirudisha. (makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nizungumzie bila ya kuogopa kitisho cha mtu kwamba fedha za EPA zisiporudishwa, mahali hapa patakuwa padogo, hapatatosha kwa sababu wabunge wote ambao tuna nia nzuri na Serikali ya CCM hatutakubali mapato ya ndani ya nchi yetu yawe madogo kwa sababu ya mianya kama hii. Ulinzi wa fedha za Watanzania unakuwa mdogo.

Mheshimiwa Spika, mimi sitakubali kuikana hata siku moja falsafa ya Socrates, kwa sababu na mimi nipo kama yeye. Siku ile alipohutubia pale kwenye mkutano, aliambiwa kana hiyo kauli yako; Socrates akasema sitaikana. Akaambiwa tunakupa adhabu ya kunywa sumu ufe, akanyoosha mkono akapewa sumu akanywa akafa, kuliko akane; akane nini kauli yake anayoiamini? (makofi)

Mheshimniwa Spika, naomba niseme sitakana kauli yangu ninayoiamini kwamba, lazima Serikali isimamie mapato ya wananchi na pesa za EPA zirudi ama sivyo, wananchi huko nje nyamazeni, wabunge tutapambana na zitarudi. (makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niende kwenye pesa nyingine ambazo zinachezewa, ili mjue mapato ya ndani yapo lakini yapo mikononi mwa watu wachache. Kuna bilioni 216 tangu miaka ya 1992, kwa wale ambao mnafuatilia mambo ya nchi. Zilitolewa mkopo kwa ajili ya import support.

Nitaomba mheshimwa waziri atakapokuwa anajumuisha, atuambie kama bilioni 216 zimekwisha kurudi ambazo zilitolewa zaidi ya miaka 16, zimekopwa na wenzetu wananchi wachache. Sasa ni zaidi ya miaka 16 zipo mikononi mwa wenzetu wachache, lakini leo hii tunasema mapato ya ndani ni madogo. Mapato ya ndani jamani si madogo, yapo mikononi mwa wenzetu wachache. (makofi)

Mheshimwa Spika, mimi nilisoma kwenye vyombo vya habari, Serikali iliwapa hawa watu miezi mitatu tangu Aprili wazirudishe, mwisho ni Julai. Okay! Tuwape hata Julai. Waziri atueleze hivi ikifika Julai hawajazirejesha bilioni 216 za wananchi wa Same Mashariki, na Kigoma Mjini, serikali itachukua hatua gani?

Mheshimiwa wabunge, iwapo mtakaa kimya mkiogopa vitisho, mkiacha kutetea wananchi wenu, hamuitendei haki nchi hii. Acha tusimame imara na mbunge ambaye hatawatetea wananchi wake, ina maana hawapendi. (makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba hiki kieleweke; bilioni 216 hizi wakati waziri ana wind up atuambie zimerudi ngapi. Kama hazitarudi patakuwa padogo tena hapa. (makofi)

Madhara ya tabia kama ya kuacha kundi dogo la Watanzania likamate pesa za nchi lenyewe halafu kundi kubwa liachwe linateseka, wananchi wanakufa, wanawake wanazalia barabarani madhara makubwa yako mawili: La kwanza, Taifa linakosa mapato ya ndani, lakini kubwa kuliko yote, waheshimiwa wabunge mpaangalie hapo ni kwamba sura ya namna hii inamomonyoa imani ya Taifa kidogo kidogo, bila ya sisi wenyewe kugundua. (makofi)

Mheshimiwa Spika, niingie kwenye jambo jingine ambalo halina ulinzi mzuri, nalo ni ulinzi wa rasilimali za nchi hii. Mapato ya ndani tunang’ang’ania mno TRA. Hapana, kuna vyanzo vikubwa ambavyo vimekosa ulinzi; eneo la madini haina ulinzi mzuri, mbuga zetu za wanyama kwenye utalii hakuko sawa.

Mheshimiwa Spika, nakwambia Rais akisema leo aunde Tume ifanye kazi vizuri, hakuko sawa kwenye utalii; mapato mengi na pesa zetu nyingi zimelala huko. Mimi naona nimwunge mkono mheshimwa Lazaro Nyalandu alivyozungumza pesa nyingi zimelala huko.

Jamani, naomba kuuliza hivi, usiporingia rasilimali za nchi yako, utaringia nini? Leo hii kuna mfumuko wa bei dunia nzima, naomba Watanzania waelewe kwamba mfumuko wa bei hauko Tanzania tu, hapana, dunia nzima kuna mfumuko wa bei. Nimetoka Marekani, nao sasa wanalia na mfumuko wa bei. Nimepita Uingereza na Waingereza wanalia na mfumuko wa bei na sababu moja kubwa mwenzetu amejali na kuringia rasilimali yake, yaani Mwarabu amekwenda akakataa na mafuta yake, akapanga bei anayotaka yeye kwa ajili ya mapato yake ya ndani.

Sasa sisi tunawaachia watu kwenye tanzanite wanavyotaka na kwenye almasi zetu wanavyotaka, sidhani kama tuna ulinzi wa uhakika, tunapoteza pesa nyingi sana.

Mheshimiwa Spika, kuna mifano mingine nikitoa kwa kweli inachekesha. Hebu angalieni nchi kama Kenya; let us be fair, hivi Kenya ina nini cha zaidi kutuzidi sisi Tanzania? Lakini Kenya mapato ya ndani bajeti ya 90% anajitegemea na sisi tukubaliane jamani; sisi tuna rasilimali nyingi kuzidi Kenya. Kwa hiyo kuna mahali kuna kasoro. Jamani wabunge, sisi ndio wa kurekebisha matatizo ya nchi hii, naomba tuungane, tusiogope vitisho, bali tisumame imara. Tukisimama imara Mungu atasimama na sisi, tutashinda. (makofi)

Mheshimwa Spika, ukienda Botswana, can you imagine; Botswana wana almasi wameilinda vizuri kweli kweli. Wana ng’ombe na wana makaa, lakini leo hii ni aibu sisi Watanzania hatuwezi kuisogelea Botswana. Nenda Libya kuna gesi hatuwezi kuisogelea, lakini sisi jamani Watanzania tuna tatizo gani? Hii tabia ya kuwaachia watu wachache utajiri wa nchi hii waukumbe na Watanzania wafe kwa sababu ya kutokuwa makini, mimi naomba niseme sitakana kile ninachokiamini kuwa ni ukweli na haki. (makofi)

Mheshimiwa Spika, nieleweke ninafanya hivi kwa ajili ya Taifa, na kwa ajili ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Nitaitetea na ninaomba nizungumze bila woga kwamba tutapambana pesa zetu zirudi ziingie kwenye Bajeti, isipokuwa pesa za EPA na zile bilioni 216 kurudi kwake sisi wabunge tuthibitishe, hatutaki kuambiwa kwenye karatasi kumbe pesa hazikurudi, kwa hiyo, tutakuwa hatujafanya kazi tuliyotumwa na wananchi. (makofi)

Mheshimwa Spika, naomba niseme kwamba, iwapo hatutasimama imara, tutakuwa Taifa lisiloheshimika. Ukiona Taifa linaachiwa kikundi kidogo kuhodhi pesa za Watanzania na wabunge mpo, mmechaguliwa na wananchi mnakuja mnakaa kimya; it is wrong, ni bora msije. Tusimame imara tusiogope vitisho wala tusimwogope mtu yeyote yule, bali tusimamie Serikali yetu na CCM. Ugomvi wangu ni kwa wale wanaoichafua Serikali yetu ya CCM, kwa kuhodhi pesa za Watanzania isivyo halali (makofi)

Mheshimwa Spika, naomba niunge mkono hoja . Ahsante sana (makofi)
 
Mwanaizaya,

Mbona hii ishu ya mama kilango na mchango wake tuliishaujadili hapa, nafikiri ingeunganishwa kwenye thread iliyokuwa ikizungumzia hilo swala. Ila thanks kwa kuileta tena.
 
Mwanaizaya,

Mbona hii ishu ya mama kilango na mchango wake tuliishaujadili hapa, nafikiri ingeunganishwa kwenye thread iliyokuwa ikizungumzia hilo swala. Ila thanks kwa kuileta tena.

Mkuu nafikiri huyu mama aliongea maneno mazito na ya busara, si vibaya kujikumbusha maana watanzania huwa tu wepesi wa kusahahu. Aliyoyasema yataendelea kuumiza vichwa vyetu hata miaka kumi ijayo. Hivi katika serikali yetu nani anaangalia suala la Kenya kuwa na RASlimali kidogo zaidi yetu lakini uchumi wao uko juu zaidi yetu?

Yule Mzee wa ndege kupaa nafikiri angelikuwa Kenya angekosa maneno ya kutamka. Angsema uchumi unaondoka kama Missile.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom