Pata ushauri wa bure wa kesi yoyote, Ardhi, Jinai na Madai (Thanks Giving Days)

Yupo bwana alikamatwa na gari ya wizi, huyo bwana nina ugomvi nae wa kibiashara, sasa jamaa alipoulizwa gari kaitoa wapi akasema mimi ndio nimempa. Polisi wakatukamata sote wakatuweka ndani then tukafikishwa mahakamani.
Kule mahakamani jamaa akakiri kosa ile siku ya kwanza tuliyopelekwa na akahukumiwa miaka 9 gerezani, mimi nilikataa. Mwaka mmoja baadae jamaa akakata rufaa, mahakama kuu ikaamua ashitakiwe upya. Aliposhitakiwa upya akakataa mashitaka na akakana kuwa si mimi niliyempa hiyo gari. PP hakumuuliza alipewa na nani. Wote tupo nje kwa dhamana.
Swali. Kesi ikiisha naweza kumfungulia kesi ya kumdai fidia huyu bwana kwa kunizalilisha, gharama za kesi na kunipotezea muda?
Sio vyema kulizungumzia hadharani jambo ambalo bado liko mahakamani, na kwa faida yako nitafute inbox nikujibu hili kwa ufasaha na ujue cha kufanya.
 
Kuna mtu ananidai million 4 na mpango wangu ni kumdhulumu kabisa! Na nimemkopa tena mdogo wake yani nampango wa kudhulumu familia nzima je wakinifungulia kesi ya wizi wa uaminifu mahakamani watanishinda?
Mimi sio mwanasheria ni 'mpima ardhi 'lakini ngoja nitoe opinion yangu
Opinion
Kwa mujibu wa Maelezo yako hapo juu unasema kwamba 'umepanga kudhulumu ' basi hapo tayari ulishaonesha nia mbaya 'mens rea ' na kitendo unacho kifanya tayari kimezuiwa kisheria 'actus reus ' sasa basi kwa mujibu wa sheria inaitwa 'penal code cap 16' au kwa kiswahili Kanuni ya adhabu hilo kosa linaitwa 'obtaining money by false pretense ' yaani kujipatia pesa kwa udanganyifu.
 
Habari wakili.
He ninaweza kuishitaki vodacom badala ya wakala aliyeingia mitini na fedha zangu?
Mimi sio mwanasheria lakini ngoja nikwambie kitu, madai yana ukomo nenda kadanlodi sheria inaitwa The law of limitation Act hiyo inaitwa sheria ya ukomo, wakili hapo juu kakupa mifano ya kesi na muda wake i. e mikataba, ardhi nk, sasa je nini madhara ya kutokuitii sheria hii?

Jibu ni kwamba endapo utafungua madai yako mahakamani Mfano madai ya ardhi wakati muda ushapita uliowekwa kisheria kwenye baraza la ardhi na nyumba la wilaya matokeo yake ni kwamba utawekewa pingamizi la awali that is notice of preliminary objection, kwamba 'The matter is time barred 'yaani hii kesi muda wake ushapita na hivyo bas kesi yako itatupiliwa mbali
 
Kikawaida ukimuwekea mtu dhamana na akatoroka basi wewe mdhamini hua unapaswa kufika mahakamani na kutoa taarifa mara moja juu ya tukio ilo, mahakama itakupa order ya wewe kumtafuta hadi kumpata ila ukishirikiana na jeshi la polisi, endapo itaonekana kabisaa jamaa hajapatikanika basi mahakama hua inachukua bond uliyoiweka kwa muda mpaka siku atakapo patikanika au inakutozesha fine ulipe na wewe ufanye maombi ya kujitoa kama mdhamini kwa mtu huyo, kwa busara muda mwingine mahakama hua zinawaacha tu huru wadhamini hao na inaendelea na utaratibu wa usikilizwaji in absentia angali mtuhumiwa hayupo, hakuna mtu anaeweza kufungwa kwa kosa la mtu mwingine kisa alimdhamini.
Ahsante sana wakili msomi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Migogoro ya vyama vya ushirika yaani mwanachama na chama chake unaeweza kwenda mahakamani? Nilisikia sheria ya vyama vya ushirika hairuhusu kwenda mahakama,je nini kifanyike?

Mimi ni saveya aka mpima ardhi , ngoja nitoe opinion yangu akija 'Wakili Msomi ' atasahihisha vizuri Kama nimekosea

ISSUES
.i je migogoro baina ya chama cha ushirika na wanachama inatatuliwaje?

OPINION
kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya ushirika ya 2013 (na marekebisho yake) kifungu cha 8 kinasema moja ya kazi ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika ni kutatua migogoro na malalamiko yanayotokana na Vyama vya ushirika Soma kifungu 8(2)(a) (v) hivyo basi migogoro itapelekwa kwenye 'Tume ya maendeleo ya ushirika ' ambayo imeanzishwa na sheria hiyo ya ushirika kifungu cha 6 cha ' The Cooperative societies Act of 2013 as amended '
 
Mkuu safi sanaaa sanaaa, your a man of honor,,, umefanya kazi ziwe nyepesi thanks.

Labda kwa kukazia tu mashirika mengi hua yana sheria zake ambazo hua zinatoa mapendekezo ya wapi migogoro ikatatuliwe na mara nyingi hua ni mabodi ya usuluhishi utatua kero na matatizo mbali mbali,

lakini baada ya haya mabodi kuonekana kushindwa labda kutatua mgogoro kwa ufasaha hua kuna nafasi kwa wasio ridhika kwenda ngazi ya mahakama kuu kwa ajili ya marejeo tu ya maamuzi yaliotolewa na mabodi.
 
Mimi sio mwanasheria ni 'mpima ardhi 'lakini ngoja nitoe opinion yangu
Opinion
Kwa mujibu wa Maelezo yako hapo juu unasema kwamba 'umepanga kudhulumu ' basi hapo tayari ulishaonesha nia mbaya 'mens rea ' na kitendo unacho kifanya tayari kimezuiwa kisheria 'actus reus ' sasa basi kwa mujibu wa sheria inaitwa 'penal code cap 16' au kwa kiswahili Kanuni ya adhabu hilo kosa linaitwa 'obtaining money by false pretense ' yaani kujipatia pesa kwa udanganyifu.
Kwa hiyo mkinihukumu nitumikie adhabu labda miezi sita na nigome kulipa ili tu adhma yangu ya kudhulumu familia nzima na ikibidi ukoo itimie sheria inasema nini?😝
 
Ahaa asante kwa elimu wakili msomi.
Mkuu safi sanaaa sanaaa, your a man of honor,,, umefanya kazi ziwe nyepesi thanks.

Labda kwa kukazia tu mashirika mengi hua yana sheria zake ambazo hua zinatoa mapendekezo ya wapi migogoro ikatatuliwe na mara nyingi hua ni mabodi ya usuluhishi utatua kero na matatizo mbali mbali,,, lakini baada ya haya mabodi kuonekana kushindwa labda kutatua mgogoro kwa ufasaha hua kuna nafasi kwa wasio ridhika kwenda ngazi ya mahakama kuu kwa ajili ya marejeo tu ya maamuzi yaliotolewa na mabodi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni saveya aka mpima ardhi , ngoja nitoe opinion yangu akija 'Wakili Msomi ' atasahihisha vizuri Kama nimekosea

ISSUES
.i je migogoro baina ya chama cha ushirika na wanachama inatatuliwaje?

OPINION
kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya ushirika ya 2013 (na marekebisho yake) kifungu cha 8 kinasema moja ya kazi ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika ni kutatua migogoro na malalamiko yanayotokana na Vyama vya ushirika Soma kifungu 8(2)(a) (v) hivyo basi migogoro itapelekwa kwenye 'Tume ya maendeleo ya ushirika ' ambayo imeanzishwa na sheria hiyo ya ushirika kifungu cha 6 cha ' The Cooperative societies Act of 2013 as amended '
Ahsante ubarikiwe sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sio mwanasheria lakini ngoja nikwambie kitu, madai yana ukomo nenda kadanlodi sheria inaitwa The law of limitation Act hiyo inaitwa sheria ya ukomo, wakili hapo juu kakupa mifano ya kesi na muda wake i. e mikataba, ardhi nk, sasa je nini madhara ya kutokuitii sheria hii? Jibu ni kwamba endapo utafungua madai yako mahakamani Mfano madai ya ardhi wakati muda ushapita uliowekwa kisheria kwenye baraza la ardhi na nyumba la wilaya matokeo yake ni kwamba utawekewa pingamizi la awali that is notice of preliminary objection, kwamba 'The matter is time barred 'yaani hii kesi muda wake ushapita na hivyo bas kesi yako itatupiliwa mbali
Mpatie na exceptions zake basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikawaida ukimuwekea mtu dhamana na akatoroka basi wewe mdhamini hua unapaswa kufika mahakamani na kutoa taarifa mara moja juu ya tukio ilo, mahakama itakupa order ya wewe kumtafuta hadi kumpata ila ukishirikiana na jeshi la polisi, endapo itaonekana kabisaa jamaa hajapatikanika basi mahakama hua inachukua bond uliyoiweka kwa muda mpaka siku atakapo patikanika au inakutozesha fine ulipe na wewe ufanye maombi ya kujitoa kama mdhamini kwa mtu huyo, kwa busara muda mwingine mahakama hua zinawaacha tu huru wadhamini hao na inaendelea na utaratibu wa usikilizwaji in absentia angali mtuhumiwa hayupo, hakuna mtu anaeweza kufungwa kwa kosa la mtu mwingine kisa alimdhamini.
Nashukuru kwa maelezo haya...nimepata elimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me naomba kusaidiwa swala hili kisheria.
Kuna ndugu yangu akiwa na rafiki yake tulikubaliane bila maandishi wafanye kazi na nikawapa mtaji wa tsh. 1M, wamefanya kazi kwa Muda Mfupi na fedha yote wakaitafuna bila kufikia makubaliano yetu. Je jambo hili linataturika kisheria kwa maana ya kuwashtaki mahakamani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ebu naomba ushauri wako kwenye hili suala 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Wakuu poleni na majukumu, naombeni msaada wenu mawakili wasomi, na wadau wengine Kwenye jukwaa hili. niende moja kwa moja kwenye mada.

Mwaka 2017 nilikutanishwa na Jamaa fulani hivi ambao walikuwa wamejiingiza Kwenye shughuli za Utafiti na uchimbaji wa madini ya Dhahabu.

Walinitaka tufanye kazi pamoja kama mtaalamu wao na mimi nikawaweka bayana kiasi ambacho huwa nalipwa kwa shughuli za Utafiti na uchimbaji wa Dhahabu. (Kiasi XX).

Kiasi kile kwao walisema hawana uwezo wa kunilipa na kimsingi wakasema kuwa hawana kabisa uwezo wa kunilipa ila wakaja na pendekezo kuwa watanipa share katika miradi yote ya Utafiti au Uchimbaji wa madini ya Dhahabu watakayoanzisha au tutakayoanzisha pamoja.

Ila tukakubaliana kuwa wakati nafanya hzo kazi watakuwa wananipa hela ya kujikimu na hata nikitaka pesa zaidi watanipa kwa makubaliano kuwa pesa nitakayochukua nje ya hela ya kujikimu itakuja katwa Kwenye gawio langu.

Basi nikawataka kuwepo na makubaliano rasmi kati yetu na wao, hawakupinga ila kimsingi walitaka tu tufanye kazi kirafiki (gentlemen agreement) ila mm niliwakatalia kuwa haitawezekana.

Kwa hiyo tukakubaliana kuwa waandae makubaliano na kuyatuma kwangu ili na mimi niyapitie.

Ghafla ikatokea kazi ambayo ilinifanya niende field Mara moja, nikaondoka ila nikawataka waandae hayo makubaliano na kuyatuma kwangu kwa email.(hapo nilienda Kufanya Utafiti Kwenye LESENI zao)

Basi tukawa tunaendelea Kufanya Utafiti huku na kule ila kwa Bahati mbaya LESENI zote walizokuwa nazo hazikuwa na majibu mazuri ya Kufanya kuanza uchimbaji au kuziuza kwa mwekezaji.

Kwa kutumia connections zangu nikapata ushirika fulani hv ambao walikuwa na leseni zao ila hawakuwa na mtu wa kuwawezesha mambo Fulani Fulani.

Basi nikawa nimewajulisha Jamaa zangu tukatembelea huo ushirika na tukakubaliana kuwa tutafanya kazi pamoja. Kwa hyo ikabidi mimi nibaki field nikiandaa miundombinu ya kazi na kuanzisha maduara/mashimo ya uchimbaji wa Dhahabu.

Wakati nikiendelea kuandaa miundombinu ya kazi nikaanda makubaliano ya Kufanya kazi kati yangu na hao jamaa. Nilifanya hivi baada ya kusubiri makubaliano Kutoka kwako kama ambavyo tulikubaliana lakini hawakuandaa.

Baada ya kuwatumia yale makubaliano walianza kwa kuomba samahani kuwa walisahau kama ndio walitakiwa kuandaa makubaliano.

Kimsingi walikubaliana na baadhi ya vipengele nilivyoweka Kwenye makubaliano na vingine walivikataa na kuongeza Vya kwako.

Hawakukubaliana na kipengele cha mimi kuwa sehemu ya mmiliki wa maduara (kwa lugha rahisi Mgodi) tutakayoanzisha kwa madai kwamba endapo ubia kati yangu na wao utavunjika basi mimi nitakuwa nawapelekesha kwa vile ni mmoja ya mmiliki wa maduara.

Hiki kipengele sikukubaliana nacho na hata tulipopata wasaa wa Kufanya mazungumzo kwa simu walishindwa kutetea kipengele hiki na wakawa kama wananishawishi tu nukubaliane nao ila hawakuwa na sababu zinazojutosheleza.

Kipengele kingine ni kwamba walisema mimi sitaruhusiwa kuwa ma maduara yangu peke yangu au kuwa na ubia na mtu mwingine yoyote katika shughuli za uchimbaji kwa maeneo ambayo tulikuwepo tofauti na wao. Kipengele hiki pia sikukubaliana nacho.

Wakati tunaendelea kujadiliana Kuhusu makubaliano maduara mawili niliyokuwa nimeyaanzisha yakawa yamefika Kwenye uzalishaji.

Nikawataarifu kuwa maduara yetu yapo vizuri na kuwa kuna mawe nitasaga ili tujue yana uzalishaji kiasi gani.?? Ikumbukwe kuwa maeneo tuliyokuwa tunachimba yalikuwa chini ya ushirika Fulani na huo ushirika ulikuwa na ofisi iliyokuwa inaratibu shughuli zote za uchimbaji.

Siku tunasaga yale mawe akaja muwakilishi wao kwa hyo mawe yakasagwa na yeye akiwepo na Dhahabu kukamatishwa.

Dhahabu iliyopatikana Kwenye Yale mawe tuliyosaga ilikuwa ni ya kutisha maana kiroba kimoja cha wastani wa kilo mia kilitoa gramu 40 za Dhahabu. Yule muwakilishi wao akawa kama kapagawa vile.

Kesho yake mimi nikawa Naendelea na kazi pale mgodini ila yule muwakilishi wao akawa kama hataki kuwa karibu na mimi na muda mwingi anaongea na simu.

Jioni ya siku hyo nikapata simu Kutoka kwa wale Jamaa wakinituhumu kuwa kuna wizi wa mawe ulifanyika Kwenye duara lao na mimi nimehusika.

Na wakaniambia kuwa ofisi ina ushahidi kuhusu wizi uliokuwa unaendelea na wameshanipa onyo Mara kadhaa ila sikuacha.

Niliwajibu kifupi tu kuwa hamna wizi wowote ambao ulishafanyika na hakuna onyo lolote ambalo lilishatolewa na ofisi Kuhusu wizi.

Jamaa haraka haraka tu wakaniambia sisi hatutaki tena biashara na wewe na wakaenda Mbali zaidi wakasema afadhali tulikuwa hatujasaini makubaliano yoyote na wewe. Wakanitaka kila kitu nimkabidhi muwakilishi wao.

Mimi hatua ya kwanza niliyochukua ni kuiandikia ofisi nikawataka kukanusha kuwa kuna wizi ulishatokea na mm nikahusika.

Ofisi ilijibu barua yangu na kukana kuwa sijawahi husika Kwenye wizi wowote na wala sijawahi kupewa onyo lolote.

Baadae ofisi ikaanza Kufanya mchakato wa kunikutanisha na wale Jamaa zangu ili tuone tunamalizanaje. Jamaa zangu hawakukubali kuja site na baada ya mvutano mrefu ofisi wakanishasuri niende nikutane na Jamaa zangu tuone kama tunaweza malizana.

Nilipokutana nao hata zile tuhuma hazikuongelewa badala yake wakasema tu hawawezi kuendelea Kufanya kazi na mm kwa maana hakuna tena trust kati yetu. Mimi nikawaambia kama ndivyo basi wanilipe kile kiasi nilichotaka mwanzoni wakati nakutana na kwa kipindi chote nilichokuwa nao au nibaki na share ya 10% Kwenye ule mradi uliokuwa unaendelea ila mm nisijihusishe na kitu chochote niwepo tu kuangalia maslahi yangu.

Mapendekezo yangu hawakukubaliana nayo, nilipowauliza nyie mnatakaje Mmoja wao akaniambia we ondoka tu tuachie tuendelee na ile kazi halafu siku tukipata faida tutakufikiria, nikawaambia hilo halitawezekana. Tukaachana bila muafaka wowote.

Baadae kupitia kwa mtu fulani wakasema watanipa 30m ili tuachane, baadae ile 30m ikapungua tena ikawa 20m, hata hyo 20m hawakutoa wakawa wanapiga chenga tu.

Sasa hapa nilipo ninataka kwenda mahakamani ili niwafungulie hawa Jamaa kesi ya madai.

Ombi langu kwa mawakili wasomi na wadau wengine yenye uzoefu na kesi za madai, Ni utaratibu/jinsi Gani naweza kuwafungulia hawa Jamaa kesi ya madai.

Au kutokana na Maelezo yangu hapo juu ni utaratibu Gani wa kisheria au kimahakama natakiwa kufuata ili niweze kupata haki yangu.

Nitashukuru sana kwa msaada wenu wakuu
 
Me naomba kusaidiwa swala hili kisheria.
Kuna ndugu yangu akiwa na rafiki yake tulikubaliane bila maandishi wafanye kazi na nikawapa mtaji wa tsh. 1M, wamefanya kazi kwa Muda Mfupi na fedha yote wakaitafuna bila kufikia makubaliano yetu. Je jambo hili linataturika kisheria kwa maana ya kuwashtaki mahakamani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio unaweza ukawashtaki hao mabwana mahakamani, kisheria mkataba unaweza kua wa maandishi au wa maneno, nyie mliingia mkataba wa maneno juu ya kufanyika biashara flani ambayo haikufanyika kwa sababu za jamaa kuila hela yote ya mtaji, so wamevunja mkataba kwa kula hela ambayo imepelekea mkataba kuto tekelezeka,

mwisho naona kulikua na nia ya nyie kuingia mkataba wenye mahusiano ya kisheria kwa maana mlikubaliana kufanya jambo flani litakalo walipa wote....muhimu tu andaa mashaidi ambao walikua wanajua kuna kitu kama icho kilikua kinaenda kutokea,

kama una sms za tigopesa/mpesa ambazo uliwatumia kwa purpose hio, sms zenu za kawaida yaani andaa mazingira ambayo ni kweli yanaonesha juu ya hiki kitu.
 
Back
Top Bottom