666 chata
JF-Expert Member
- Mar 14, 2013
- 1,688
- 3,816
- Thread starter
- #21
Sio vyema kulizungumzia hadharani jambo ambalo bado liko mahakamani, na kwa faida yako nitafute inbox nikujibu hili kwa ufasaha na ujue cha kufanya.Yupo bwana alikamatwa na gari ya wizi, huyo bwana nina ugomvi nae wa kibiashara, sasa jamaa alipoulizwa gari kaitoa wapi akasema mimi ndio nimempa. Polisi wakatukamata sote wakatuweka ndani then tukafikishwa mahakamani.
Kule mahakamani jamaa akakiri kosa ile siku ya kwanza tuliyopelekwa na akahukumiwa miaka 9 gerezani, mimi nilikataa. Mwaka mmoja baadae jamaa akakata rufaa, mahakama kuu ikaamua ashitakiwe upya. Aliposhitakiwa upya akakataa mashitaka na akakana kuwa si mimi niliyempa hiyo gari. PP hakumuuliza alipewa na nani. Wote tupo nje kwa dhamana.
Swali. Kesi ikiisha naweza kumfungulia kesi ya kumdai fidia huyu bwana kwa kunizalilisha, gharama za kesi na kunipotezea muda?