Pata hii "Painful Calls"

BatteryLow

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
446
149
Hii sasailikuwa ni majanga kwangu. Nina tabia ya kila siku asubuhi nafungua cm yangu nakuangalia simu zote za jana. sasa bwana cku 1 asubuhi kufungua tu nikakutana namsururu wa namba za nchi za nje tisa zimepigwa kwenye cm yangu, yaani dialled, siyo kwamba nimepigiwa, no,nimepiga. Kwanza nikawa sielewi, yaani nikabaki kama mjinga mjinga flani,naangalia kitu lakini sielewi elewi. Yaani sijapiga mm lakini zimepigwa kwenyecm yangu na zimetoka.

Nikajiambia tu mwenyewe ngoja kwanza kichwa kirudi,nikaachana nazo nikaamua nimpigie jamaa yangu nimweleze hiyo issue, ile napigacm naambiwa "tafadhali huna salio, ongezasalio kabla ya …."Wakati huo jana nililaza cm ikiwa na salio la TAS 4,000=.Nikaona hii kitu imekuwa tatizo la kitaifa, nikafungua faili imeandikwa "painfulcalls" nikazitupia pale zile namba tisa za kigeni.

Nikaongeza salio la TAS 2,000=, ujue hapo niko ofisini,ghafla akaja mtu nikawa nampa huduma hivyo ile simu nikaweka chini kwanza. Ilehuduma ilichukua kama dakika 15 – 20. Baada ya Yule m2 kuondoka nikachukua cmyangu ili nimpigie yule jamaa yangu, ile naweka tu sikioni nasikia "tafadhali huna salio, ongeza salio kabla ya…"Nikagundua kuwa kitendo cha kuongeza salio na kuweka cm chini ilikuwa kosa.Kufungua cm kuangalia dialed numbersnikakuta namba ya nje ishapigwa ikawa ya kumi sasa, na katika hizo namba 10 ninamba moja tu ilipigwa mara 3, nyinginezote saba zilipiga mara moja moja.

Uamuzi uliofuata nilikwenda kuripoti tukio Vodahouse haraka.Nikawatajia namba ya cm yangu. Wakaangalia kwenye kompyuta zao akaniambia "nikweli, hizi simu 9 zimepigwa usiku kati ya saa 8 – 10, lakini ni simu tano tuzilizopitia kwenye mitambo ya Voda na nne zimekwenda bila kupitia kwenyemitambo yetu na tunashindwa kuelewa zilipitaje."

Yule mfanyakazi akaniuliza kama nitawaruhusu wazuie simuzote za kimataifa kwenye hiyo laini yangu, nikawaambia poa, haina shida,nikitaka kupiga cm ya nje ntatumia laini ya Tigo.
Wakafanya hilo zoezi na kweli likafanikiwa na nikanunuavocha palepale nikaweka. Bado sijaondoka pale mezani Voda nikaona screen ya simuinawaka taa na ninasikia sauti ya mtu inaongea, kumbe bwana ni wale watuwalishanifanyia timing ili nikiweka vocha tu wapige.

Nikanyanyua ili nisikilize yale maneno na yalisema "huruhusiwikutumia namba hii, wasiliana kwanza na operator wa Vodacom", tukawatumewakomesha ubishi.
Kama kuna swalinawaruhusu mswali.
 
Na wewe ukajikomesha kwani huwezi pia kupiga au kupigiwa toka nje


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Je, mpaka sasa umeshawajua au kupewa taarifa yeyote na vodacom?
Sijawajua, ni wa nchi za nje, mm nilichokuwa nataka ni voda wazuie tu huo mchezo hivo walivyozuia sikuona haja ya kuhangaika nao.
 
aiseee:confused: vibaya kama utatupia hizo number hapa tuzigoogle mkuu
 
Back
Top Bottom