Paschal Mayala na ku-declare interest

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,435
1,597
Leo nikifuatilia mdahalo wa mchakato wa katiba uliorushwa na star tv, nilimsikia Paschal Mayala akisema baada ya kupewa kipaza sauti... "Kwanza naomba ku declare interest" halafu akaendelea "mimi si mwanachama wa chama chochote..." Swali langu ni je, alikuwa sahihi? kama hakuwa mwanachama wa chama chochote, alikuwa na haja ya ku declare hiyo interest?
 
Nafikiri alikuwa akimaanisha kwamba kabla hajaendeleza mjadala ilikuwa ni muhimu kwa hadhira kutambua mapema kwamba yeye si mwanachama wa chama chochote kile na wala hana maslahi (interest) humo.

Kwahio chochote ambacho angekuwa akisema kwenye mahojiano hayo kilitakiwa kifahamike kwamba ni mawazo yake binafsi.
 
Katika hali ya sasa ni sahihi ku-declare interests. Wapo wengi tu wasio na vyama lakini wangependa kuwe na katiba nzuri na serikali makini na sikivu. Nchi yetu hoja za mtu zinapimwa kwa chama anachotoka. Unaweza ukawa na hoja nzuri lakini kwa kuwa unatoka opposiion utaonekana hufai.
 
watu wengine wanaona aibu kusema wapo ccm.kama wewe chadema ukamuuliza wewe chama gani atakujibu hana chama.akikutana na ccm wakamuuliza wewe chama gani anajibu mimi ni ccm damu damu. mia
 
Alifanya vizuri, kuashiria hafungamani na upande wowote na kwamba swali lake si lakishabiki kama wengi walivyokuwa wakiuliza kishabiki zaidi
 
Alifanya vizuri, kuashiria hafungamani na upande wowote na kwamba swali lake si lakishabiki kama wengi walivyokuwa wakiuliza kishabiki zaidi

Na hapo ndo swali langu lilipojikita, mimi nildhani mtu an declare interest kama anafungamana na upande fulani, kinyume na hapo angepaswa kuchangia bila ku declare interest au ni vipi jamani. Naomba kuelimishwa nijue matumizi sahihi ya maneno haya.
 
Move ya katiba sasa hivi inaonekana kuwa kati ya CCM na CDM, Pascal hayuko huko, so nadhan yuko sahihi kuonesha hilo wazi kwamba hayuko katika pande zinazovutana. I stand to be corrected.
 
Kachemka kusema na declare interest halafu anasema sifungamani na upande wowote,nani asiyejua p.mayalla ni ccm? Matamasha yote ya miaka 50 ya uhuru wizarani na taasisi zake yupo.
 
Back
Top Bottom