Pascal Mayalla: Rais punguza ukali

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,307
6,514
Mtangazaji huyu nguli ameyasema haya kama ushauri kwa rais, akiwa kwenye viwanja vya sabasaba akitangaza kwa niaba ya PPR.....

Amegusia suala la kuminywa kwa mikutano ya siasa hivi sasa....ila kwa kiwango kikubwa mtangazaji huyu alikuwa akimsifia rais, na wakati akitoa ushauri wake huo alionekana kuhofia hofia.
 
Pascal Mayalla ni kundi la Membe alisha athirika hivuo ushauli wake ni wa mashaka
ijapo ni kweli Magufuli amemenya siasa
 
Mtangazaji huyu nguli ameyasema haya kama ushauri kwa rais, akiwa kwenye viwanja vya sabasaba akitangaza kwa niaba ya PPR.....

Amegusia suala la kuminywa kwa mikutano ya siasa hivi sasa....ila kwa kiwango kikubwa mtangazaji huyu alikuwa akimsifia rais, na wakati akitoa ushauri wake huo alionekana kuhofia hofia.
Mkuu Mcubic, kwanza asante kwa kuangalia kipindi changu cha Saba Saba na PPR, andelea kunifuatilia. Vipindi hivyo vinatangazwa katika vituo vitano vya TV, TBC, ITV, Star TV, Channel Ten, Clouds TV, na ZBC.

Kwa wale wazamani wanaonifahamu tangu enzi zangu za kipindi cha Kiti Moto, wananifahamu na wanafahamu type ya maswali yangu, nikweli jana nilikutana na rais Magufuli kule Saba Saba na baada ya kumsalimia nilimuhakikishia Watanzania wanampenda sana ila pia amezidisha ukali kwa kuzuia mikutano ya siasa.

Katika maisha yangu yote ya miaka 25 ndani ya tasnia ya habari, sijawahigi kuwa muoga, au kuhofia lolote wala yeyote!.

Ni kweli kwenye maonyesho, nilipata fursa ya kumsalimia Mhe. Rais, kwa msiofahamu, Rais Magufuli ni mtu wa kabila langu, na nikienda Chato, nafikia hotelini kwake, na kuna wakati nilifika na wageni fulani wazungu, kula vyakula vya pale kuliwashinda, Mama Janet Magufuli in person, aliingia jikoni kutupikia!. Hivyo ningekuwa ni mtu wa kujikombakomba kwa wakubwa, huu sasa ndio ungekuwa wakati wenyewe!.

Mimi ni muumini wa ukweli daima (nothing but the truth), na uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, (freedom of expression and opinion), yaani kuwa mkweli daima, truthfully na kuwa huru kujieleza na kutoa maoni yangu freely kwa kuitumia, freedom of speech, kusema chochote, freedom of expression, uhuru wa kujieleza, freedom of opinion, uhuru wa kutoa maoni yoyote, freedom of movement, uhuru wa kwenda popote, freedom of employment, uhuru wa kuajiriwa kazi yoyote hadi freedom of love, uhuru wa kumpenda yoyote, tena bila limit number ya mtu mmoja mpenzi mmoja, etc!.

Ni kweli Magufuli ni mkali sana, na ukali mwingine hauna sababu za msingi, waliomzunguka wanamuogopa kumwambia ukweli!, kwa vile mimi ni muumini wa ukweli daima, sikuona shida kushauri kwa kuwa Magufuli ni mtumishi wetu, sisi ndio tuliomuajiri kwa kura zetu, na sisi ndio tunaomlipa mshahara kwa kodi zetu, hivyo sisi ndio mabosi wake!. Kwa vile yeye ndie tuliyemchagua kuwa kiongozi wetu mkuu, tunapaswa sio kumuogopa, bali kumuheshimu, na ndicho nilichokifanya, kumuheshimu na kumueleza ukweli kwa unyenyekevu.

Paskali.
 
Kumbe Magufuli ana Hoteli? Thamani yake ikoje. Ni ya nyota ngapi? Ameijenga toka lini? Ni kwa mishahara yake au dili? Anyway hilo huwezi kujua lakini I can smell fishy kama kweli ni rafiki wa masikini anayejipambanua na Unyerere alikufa bila hata Mghahawa!
Yes anayo na sio moja!.

Sio kosa Mtanzania yoyote kumiliki mali yoyote alimradi hiyo mali awe ameipata kwa haki na halali na umiliki wake pia uwe ni wa halali!.

Paskali
 
Back
Top Bottom