Part Two: Wajue "MadadaPoa" wa Kwenye Madanguro

Part Two: Wajue "MadadaPoa" wa Kwenye Madanguro

Nusratt mimi napenda vile unavyoandika herufi kwa ufasaha na mtiririko mzuri. Ila siku hizi kuna makaka poa pia, siku uje na hii mada. Kuna wanaofanya kama massage parlour kumbe ukizidiwa, unaambiwa utaongeza kiasi kadhaa uhudumiwe.

Kuna kaka poa, kapanga nyumba nzima kazi ni hiyo.
Haya wanunuzi wa utelezi, mmekaribishwa, mtupe mauzoefu yenu.
Asante sana kipenzi Bantu Lady
Unajua katika kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa, matumizi sahihi ya herufi na namba ni muhimu ili ujumbe ufike vyema.
Nashukuru kwa kuliona hilo.

Karibu sanađź«¶
 
Umeshawahi kumhisi mtu kama ni mteja wa makaka poa?
Basi kuna watu na heshima zao ndio wateja wakubwa. Kuna mtu mmoja mwenye degree nyingi tu amempangishia msenge wake nyumba Tabata. Nikikuonesha picha yake utakataa.
Au yule uchafu mwingi wa dampo ambaye hana shida na kitu kinaitwa K, yeye ni wanaume tu tena watu wenye wake na familia zao.
Hiii ya Makaka poa imejificha sababu wanaofanya ivi sana ni wanaume wenye ndoa zao wanaume wengi wanaogopa kujulikana
 
Unaweza kujiuliza hao madada poa 3 kwa kila chumba wanalalaje?
Iko hivi, si kila dada poa analala danguroni.
Wapo wanaokuja kufanya kazi usiku tu na asubuhi huondoka na wapo pia wanaofanya kazi asubuhi na jioni wanaondoka makwao.
Na hata hao waliopangisha au kugeuza nyumba zao madanguro pia hugharamia godoro na maji tu.
Shuka, mto,  MAFUTA, condom huja nazo dadapoa.
Hapo kwenye mafuta nimekumbuka jambo 🤣🤣🤣

Kuna mmoja nilizunguka nae usiku wa saa 7 tukitafuta mafuta kisa kuna kitu nilitaka
 
Katika principles zangu nilizo ona nimeziweza ni pamoja na hii ya kuto kununua utelezi kwa style ya hawa dada poa.
Na ni mtu wa tungi sana naweza kesha club na naweza kupiga gambe mpaka asubuhi ila ila eti nilewe nipite na malaya hehehe never sijafikia kiwango hicho cha kutafuta utelezi.
 
Katika principles zangu nilizo ona nimeziweza ni pamoja na hii ya kuto kununua utelezi kwa style ya hawa dada poa.lezi
Na ni mtu wa tungi sana naweza kesha club na naweza kupiga gambe mpaka asubuhi ila ila eti nilewe nipite na malaya hehehe never sijafikia kiwango hicho cha kutafuta utelezi.
Utelezi usio na shida unaupata Barber shop na Spa
 
Kuna staili nyingine ya kujiuza, unakuta jimama lina genge la kuzugia nyumbani kwake, mabinti hawakauki pale, unawedha kudhani wananunua mbongamboga kumbe wako kwenye misheni za kujiuza na wateja wanajua pale kuna dadapoa wapo. Ukimpata mnazama ndani chumbani kwa jimama lina vitanda viwili, unabuza tani yako kisha unatoka. Wengine unakuta mshangazi ana mgahawa wa kuzugia, kajaza mabinti mpaka wengine hawana kazi za mapishi. Wateja huenda kuzuga kula kumbe wameenda kupata dadapoa. Ukimpata unaacha hela kwa mshangazi we unazamia na dadapoa chumbani kumtafuna. Kumekuwa na vijiwe visivyodhaniwa kuwapata madadapoa
 
Mkuu mbona unawapa maujiko sana hao wanaosimama barabarani.

Binafsi sionagi pisi zaidi ya wazee wazee tu, hayo madanguro ya lodge au nyumba za watu nako wamejaa wazee na pisi mbovu mbovu kishenzi.

Kidogo vijumba vya wahay kuna vijana vijana.
Ila kwa ujumla siku hizi wanawake wanaojiuza kwa kujianika wengi wamechoka haijalishi umri wao, vijana wanazichakata mno mpaka wanakongoroka.
 
Back
Top Bottom