Part 4: TISS bado safari ngumu

Part 4: TISS bado safari ngumu

My Son drink water

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
4,930
Reaction score
13,333
Asante sana mkuu Kihava ktk comment yako post #87, umenikumbusha mbali sana.
Kabla sijaendelea nainukuu post yako Kama ilivyo kwa faida ya wengine ili wajue nini maana ya usalama wa taifa na una umuhimu gani kwa nchi.

"TISS ndio nchi yenyewe kama hujui. Hata ungekuwa na elimu kiasi gani huwezi kufanya jambo lolote la maana kama TISS hawataki.

Nakuhakikishia hata kama una uwezo wa kujenga kiwanda kikubwa kiasi gani, kilichopo eneo halali kabisa kama TISS hawataridhika na wewe huwezi! Wewe ni 'mgeni' kwenye utawala wa nchi. Nchi ina wenyewe, sisi wengine hata tungekuwa na cheo kikubwa kiasi gani kama TISS wakisema NO! Huwezi kwenda tofauti nao 'ukaishi'.

Hata huyu mzee wetu vituko anavyofanya vya kuwaumiza wenzake ni kwamba TISS wameridhia. Wakisema hatutaki hiki lifanyike hana ubavu wa kukataa. Maan ukiwakatalia wanachokisema kwa maslahi ya nchi basi wewe utaondoka ili Taifa libaki salama. Kwa hiyo kwa ujumla TISS ndio mhimili wa nchi.

Hakuna anayeweza 'kukohoa' mbele ya TISS kama wakisema hili hapana. Kwa hiyo hata Musiba TISS waliamua wamwache afanye atakavyo, lakini wangesema MUSIBA 'stop' misiba yako hatuitaki hangekuwa na jeuri ya kuendelea kufanya chochote.

Hivyo ndugu yangu jua ya kwamba hakuna mwenye ubavu kuliko TISS ndani ya nchi yoyote duniani. TISS ikiwa dhaifu nchi itakuwa dhaifu tuuuu! Tunaiombea TISS ya nchi yetu iwe imara kwa Taifa imara."


Mwisho wa kunukuu.

Baada ya mashambulizi ya kigaidi Marekani Sept 11, Rais George Walker Bush alifanya kikao cha siri Whitehouse chini ya handaki akiwa na waziri wake wa mambo ya nje, Condollezza Rice, mkuu wa majeshi ya Marekani Jenerari Tommy Franks, pamoja na mkurugenzi mkuu wa CIA Bob Tenet.

Katika kikao hicho Bush alimwambia Bob Tenet kwamba, hakuna Marekani bila CIA imara, CIA ingelikuwa legelege Marekani ingekuwa magofu hapa Duniani au ingekuwa ombaomba na maskini wa kutupwa.

Naandika makala hii kwa uchungu sana, nashangaa kuna watu wanaleta siasa ktk jambo gumu wakati mimi nazungumzia mustakabali wa taifa letu Halafu watu wanaleta habari ya vyama vya siasa.

Makala hii haina u-CHADEMA wala u-CCM, ni maalumu kwa ajili ya Taifa lenu.

Marekani, Uingereza, Ujerumani, Japan ,Sweden, Norway Finland, Australia, Canada, viongozi hawana ujanja chini ya idara za Usalama wa Taifa linapokuja suala la usalama wa nchi na maslahi ya uchumi, huwa wanafanyiwa zengwe na kutolewa.

Mungu ibariki JamiiForums, makala hii ingelikuwa kwenye Gazeti la hard copy ingekuwa imeshapata misukosuko mikubwa Kama kufungiwa Gazeti na mwandishi kukamatwa.

Pia Mungu ibariki Kenyan forum, hiyo pia imechangia uwepo wa JF, waliona kabisa kwamba endapo wataifungia JF bado tungehamia jumla Kenyan forum ambako ndo ingekuwa hatari kwa sababu watu wangetapika nyongo bila breki, bora hapa kuna speed governor.

Mungu mbariki Maxence Melo kwa kuanzisha huu mtandao unaotikisa Dunia kwa sasa.

INAENDELEA

 
Tatizo ninaloliona ndani ya idara yetu ni kugawanyika kwa idara katika vipande Viwili .

Kuna manaoleta habari za kweli na mafaili yamejaa makao makuu ya idara na Ikulu ila cha kushangaza hayafanyiwi kazi na mamlaka manachoambulia Ni Kupigwa Bench ( yaani wanakuwa ndani ya Idara Ila Uamuzi hawana)

Kundi la pili Ni wafia chama wanao leta habari za umbea kama walivyowafanyia wakina Simbachawene kipind kile, Anthony Mtaka Na wengine Kibao.

Ili Kund la pili lina nguvu kuliko la kwanza ndio maana unaona yanayoendelea sasa
 
Mkuu kuna swali niliuliza posti zilizopita, bila shaka katika hizi mada watu wa kitengo wapo wengi tu. Swali langu imekuwaje tiss wakaachia nchi ikapata baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wenye tatizo la afya ya akili. Tiss ipo na inasemwa iko imara na makini kulikoni?
 
Kajifunze kuandika kule vidudu xxxxxc hapa sio fb
Tatizo Ninaloliona Ndan Ya Idara Yetu Ni Kugawanyika Kwa Idara Katika Vipande Viwili .

Kuna Wanaoleta Habari Za Kweli Na Mafaili Yamejaa Makao Makuu Ya Idara Na Ikulu Ila Cha Kushangaza Hayafanyiwi Kazi Na Mamlaka Za Mahamuzi Na Wanachoambulia Ni Kupigwa Bench ( Yaan Wanakuwa Ndan Ya Idara Ila Uamz Hawana)

Kundi La Pili Ni Wafia Chama Hawa Ni Waleta Habari Za Umbea Kama Walivyowafanyia Wakina Simbachawene Kipind Kile, Anthony Mtaka Na Wengine Kibao.

Ili Kund La Pili Lina Nguvu Kuliko La Kwanza Ndio Maana Unaona Nchi Inaendeshwa Kishamba Xana!
 
Mimi nimeanza kujua maana ya TISS miaka ya hapa baada ya Baba wa taifa kututoka, kabla ya hapo, hawa watu huwajui ila wapo, na cha ajabu siku hizi wanatajwa hadharani na wao pia wajitokeza kwenye "live" mtindo wa kisasa, wakikemea mambo.
Yaani Siku hizi wana dili na............ ...... ....... Sio umasikini au rushwa, ufisadi, na mengine..... Mbaya zaidi sasa wanajulikana kama wafia chama na sio Nchi.
 
Mleta mada uko sahihi.
Kipindi kile Wameifungia JF kwa miezi miwili tulipata hifadhi ya ukimbizi Kenya Forum
Kule tulitapika nyongo haswa kutokana na kukerwa na tabia za uminywaji wa haki za kutoa maoni.

laiti wasingeturudishia JF yetu tungebaki Kenya Forum.

Yaani Jamaa wana mambo ya ajabu sana, yaani wako tayari data, elimu nzito iliyomo kwenye archives za JF izimike na ipotee ilimradi tu kumlinda Magufuli dhidi ya criticisms tu za kawaida za kisiasa.

Leo hii ukigoogle kitu kuhusu Tanzania, JF inatokea kama sehemu mojawapo ya Kukupa Taarifa, Sasa cha ajabu hawa jamaa walitaka JF ife na hazina hii ya data.

Ajabu sana!
 
Mkuu TISS ni genge la wahuni si kama ilivyokuwa miaka ile ya nyuma. Huyo Mkuu wa TISS wakati wa fisadi Mkapa Kitine alishiriki kwenye wizi wa $$$ Kwa kisingizio mkewe mgonjwa majuu kalazwa na hivyo wakamtumia $$$ kibao Membe akashtukia mchezo.

Huyo Mkuu wa TISS wakati wa Kikwete Othman sasa hivi ni tajiri wa kutupa kupitia mgongo wa TISS. Wataacha kulinda maovu yanayoendelea nchini huku wakijua fika nao WANANEEMEKA?

TISS ni dhaifu ndo maana ikateua au ikaruhusu mtu mhujumu Uchumi kuwepo. TISS haiwezi mfanya lolote Sponsor
 
As long as niko salama na ndugu zangu wako salama bila kusahau majirani na watanzania wa eneo nililopo. Basi nachekea kusema Tz ni nchi ya maziwa na asali. Lets keep this peace

Mkuu

Haupo salama sana kama unavyofikiria!

Watu wanauawa,wanatekwa,etc halafu unasema upo salama sababu tu sio wewe au familia yako imeguswa!

Aisee,temea mate chini,siku unaguswa ndio utaelewa haupo salama vilevile!
 
Mkuki kwa nguruwe Mkuu. Kwa sababu aliyetekwa, kuteswa, kubambikiwa kesi nzito, kupotezwa na hata kuuawa ni mtu asiyemuhusu basi yeye yuko salama! Unafiki wa baadhi ya Watanzania.

Mkuu

Haupo salama sana kama unavyofikiria!

Watu wanauawa,wanatekwa,etc halafu unasema upo salama sababu tu sio wewe au familia yako imeguswa!

Aisee,temea mate chini,siku unaguswa ndio utaelewa haupo salama vilevile!
 
Back
Top Bottom