Jamaa una propaganda sana, ndege zina matatizo ya kiufundi hata Boeng wenyewe wamekubaliana na hitilafu hiyoo.....
Mambo kama haya unapojaribu kuyaeleze unatakiwa uanze kwanza kwa kielezea mfumo wa ndege za kawaida kitaalamu na sio kwa Lugha za mtaani, then udadavue mfumo mpya wa ndege mpya za Boeng Max 8 then ujaribu kufananisha na kutuaminisha kwanini huo mfumo mpya ni salama na si kweli kama watu wanavyodai kwamba si salama na unachochea ajali.
Sikatai ujasusi wa kiuchumi upo na unafanya kazi pia kwa namna kubwa tu lakini kwa hii ishu ya Ndege za Boeng Max8 labda useme tu imetokea coincidence kwamba uzembe wa Boeng kuweka mfumo mgumu unaopelekea ajali za ndege utumike na makampuni mengine makubwa kujikuza zaidi kibiashara na kuneza propaganda ili kuishusha zaidi kibiashara kampuni ya Boeng.
Sent using
Jamii Forums mobile app