Chumchang Changchum
JF-Expert Member
- Nov 1, 2013
- 6,130
- 6,409
Tunasubiri part 3..
Hongera mkuu.
Hongera mkuu.
Asante mkuu kwa uelewa mkubwa ulionao, ni wachache mno wenye uelewa mkubwa Kama weweWenye biashara zao wanajuafika kwamba wamehujumiwa! Na hawawezi kukaa katika Mass media kusema kuwa tumehujumiwa. Kifuatacho ni kisasi tu kwa aliyemtenda. Kwa kuwa sisi wa Tz tumezoea fitina za siasa lazima tumkatalie jamaa kuwa ana uelewa mdogo, haya mambo yanahitaji tafakuri ya kina sana. Sio kila ukuta uliopakwa rangi ni ukuta daima, kuta zingine milango ya siri ya kwenda kwingine!
Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mkuu, Mungu akipenda leo hii tutakuwa na Part 3Tunasubiri part 3..
Hongera mkuu.
Asante mkuu kwa uelewa mkubwa ulionao, ni wachache mno wenye uelewa mkubwa Kama wewe
Sent using Jamii Forums mobile app
Ikiwa kila kitu kiko kwa waongoza ndege (Air Traffic Controller - ATC) kwanini wanahangaikaga kutafuta blackbox wanasema hatujui tatizo la ndege mpaka tupate black box? taarifa zote si zipo kwa ATC ama ... wakipita anga ambalo hakuna ATC huwa wanafanyaje?Mara baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Sept 11, Rais wa Marekani wa wakati huo George W Bush, alitoa hotuba fupi akiwa na hasira na macho yake yakiwa mekundu, akiwa ametoka kujificha kwenye handaki la kambi kubwa ya kijeshi iliyopo ktk jimbo la Louisiana.
"You're either with us or not with us "
Alikuwa akiiambia Dunia ichague upande wa kukaa, aidha iwe upande wa Marekani au wa adui.
Maana yake ni kwamba Marekani ina maadui wengi mno kuliko marafiki halisi, Kwa hiyo ilikuwa ni furaha kubwa mno kwa US kupigwa siku hiyo kwa adui zake.
Nakumbuka nilikuwa Khartoum Sudan siku hiyo Marekani inapigwa, hata kabla sijajua Kama imepigwa niliona watu mitaani wakishangilia Kwa furaha huku magari yakipita Kwa msululu yakipiga honi za furaha.
Kuna watu wamesema kuwa sijaandika sahihi juu ya ajali ya Boeing 737 kwamba engine haikusababisha ajali bali ni mfumo wa Computer, na kwamba ni ngumu Boeing kuhujumiwa eti kwa sababu engine za Boeing zinanunuliwa UK kutoka kampuni ya Rolls Royce.
Nataka kuwafafanulia kidogo hapo ili kuwaweka sawa, iko hivi, ndege huendeshwa kwa mfumo wa Computer ikiongozwa na watu walio chini ya ardhi na si rubani, waongoza ndege wana uwezo wa kupoteza ndege au kumpoteza rubani asijue analofanya.
Kazi ya Computer kwenye ndege ni kusoma na kuweka Taarifa ya kila kitu kwenye ndege, kuanzia engine zinavyofanya kazi, hali ya hewa na mengine mengi, engine ikiwa imara na Computer ikagoma kusoma mwenendo wa ndege, ndege itapata ajali Kwa kupotea na hii inachukua masaa mengi hadi ije kupata ajali na siyo prompt accident ambayo husababishwa na hitilafu kwenye engine Kama ilivyokuwa Kwa Ethiopian Airway.
Computer haiwezi kuishusha ndege, kazi yake ni ku record na ku monitor movements za kila device kwenye ndege.
Boeing 737 imehuhujumiwa, na ndo toleo jipya kabisa kwa Boeing, Kwa kampuni iliyo na uzoefu sokoni Kwa miaka zaidi ya 100, haiwezi kupata hitilafu ya engine wala Computer system software, Kwa sababu kabla ya kuruhusu ndege ziingie sokoni ni lazima ziwe verified, Kwa hiyo wataalamu wa Boeing wali verify na kujiridhisha kwamba zinafaa?
Jibu ni ndiyo, wali verify, lakini kwa sababu ya hujuma ndo maana zimeanguka.
Mission accomplished, tayari majuzi Rais wa China alikuwa Ufaransa, ameingia mkataba wa kununua ndege zaidi ya 60 na Airbus badala ya Boeing.
Ujasusi ni ujasusi tu, huwezi kuidharau nchi eti kwa sababu ni ndogo, an enemy you despise is always a powerful enemy.
Hakuna urafiki wala huruma kwenye maslahi, Marekani ni rafiki mkubwa wa Israel, lakini pamoja na urafiki wao kila mmoja anamwinda mwenzake Kwa staili yake.
Jonathan Pollard, alizaliwa na kukulia Marekani ktk familia ya kiyahudi, Kumbe wazazi wake waliohamia Marekani walikuwa majasusi Hatari sana, Pollard alipokua alianza kazi ya kuipeleleza US na kutuma Taarifa Israel, Hiki ni kisa cha kusisimua kinachohitaji makala yake maalumu.
Na kila mwezi alipokea mshahara kutoka serikali ya Israel .
Baadaye alishtukiwa na kukamatwa, alihukumiwa jela maisha,mwaka 2015,aliachiwa huru baada ya waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kuipigia magoti Marekani.
Hebu fikiria, Marekani haili Chakula kikapita bila kuisaidia Israel, kipesa na silaha, lakini jamaa bado wanawachungulia.
Trump hana maslahi na Russia ila Israel pekee, na kuna Taarifa Mossad walicheza mchezo ili Trump awe Rais wa US, na si Russia ambayo wengi wanaamini, hebu tazama baada ya Trump kuwa Rais ndo aliyeitangaza officially Jerusalem kuwa capital city ya Israel,kwanini marais wengine waliogopa kutangaza?
Aliyemuoa Binti wa Trump ni myahudi anayedaiwa kuwa agent wa Mossad, connect dots hapo.
Unapohujumiwa kijasusi huwezi kujua,utakuja kujua umeshamalizwa. China hakuwa na technology,waliunda kitengo cha ujasusi wa kiuchumi Kwa ajili ya kuiba technology na kweli wakafanikiwa.
Ununuzi wa engine za Rolls Royce Kwa ajili ya Boeing kutoka UK hakuifanyi Boeing kuwa salama eti kwa sababu UK ni rafiki mkubwa wa US.
kenya imehangaika na ujasusi wa kiuchumi hadi imefanikiwa hatua Kwa hatua.
Viwanda vingi vilivyokuwa Tanzania vimekufa na kufufukia Kenya, tumebakia kuwabeza huku wakisonga mbele, ooh hicho ni kiwanda cha ku assemble magari na siyo kutengeneza, ok fine, nyie mnacho? Kiko wapi cha kwenu cha nyumbu??
Ni nani kaihujumu Boeing?
Tukutane part 3 sehemu ya mwisho
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahah....ndo hivyo Boeing imepigwa na si ajabu ikafilisika kabisaTatzo watu Wana mapenzi na Boeing utadhani wanalipwa na hawataki kukubali ukweli
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kuna sehemu hujanielewa vizuri, computer kwenye ndege ndo kila kitu Kwa maana ya kwamba,kuanzia Engine, mfumo wa umeme, mafuta, hali ya hewa na nk vyote vinaripotiwa na Computer ufanyaji kazi wake, kila kitu kinajitegemea kufanya kazi lakini computer inachota Taarifa na rubani kujua status ya ndege kwa wakati husika ,lakini computer haiifanyi engine iwe na efficiency ktk ku operate kazi ya computer kufanya Delivery Report of the relevant device, kwa mfano taa zikiungua kwenye ndege computer inatoa Taarifa kuwa taa zimeungua lakini siyo computer ndo imeunguza taa, sasa computer itawezaje kufanya Engine ya ndege ifeli?Ikiwa kila kitu kiko kwa waongoza ndege (Air Traffic Controller - ATC) kwanini wanahangaikaga kutafuta blackbox wanasema hatujui tatizo la ndege mpaka tupate black box? taarifa zote si zipo kwa ATC ama ... wakipita anga ambalo hakuna ATC huwa wanafanyaje?
Umesema kompyuta haiwezi kushusha ndege, mkuu pitia zile VNAV na LNAV (vertical navigation & lateral navigation) ndo utaona kama computer za ndege huwa zinaongoza ndege mwanzo mwisho mpaka kufanya AUTOLAND zenyewe, yaani inaweza kuruka rubani asifanye chochote mpaka inafikia kutua salama salimini uwanjani tena hadi braking ambazo ni AUTOBRAKE pamoja na ANTISKIDDING zipo as long as awe amefeed kwenye MCDU/CDU, ukipitia hapo ndo utaona MCAS system iliifanya nini Lion Air na Ethiopian air, ajali kama hizi iliwahi kutokea kwa Airbus ambapo computer ilisoma kuwa ndege imepitch ile nose upward kwa degree nyingi wakati ilikuwa kwenye 180 degree kilichotokea ni ndege kudive vertically kilichosaidia ilikua futi 30,000 juu hivyo alichofanya rubani ni kuondoa autopilot na kuanza kupambana nayo mpaka ikarudi kwenye 180 degrees ambayo ni normal jaribu kuitafuta hiyo habari utaona pia, ile point ya engine mimi niliipinga sababu sio engine iliyofeli (mwanzo ulisema engine kwenye post yako ya kwanza) ila ni hiyo system ya MCAS na kama unafatilia mwaka jana/juzi kuna virus waliivamia boeing kwenda kuharibu system za computer ili kitokee kilichotokea (nimeona nikurahisishie) huko kwenye ugaidi toka awali nilikua nakueleza kuwa 'upo uwezekano' ila tatizo langu ni data zako ziko too general labda kwakuwa hauko karibu na maswala ya aviation so unajumlisha maoni ambayo kitaaluma yako nje kabisa ya ukweli wa ndege inavyofanya kazi, nakushauri ukiwa unakuja na maada ambayo imejumuisha mambo ya taaluma za hawa watu basi ni muhimu upitie kwanza kipengele hadi kipengele then ndo uende kwenye nadharia zinazohusu ujasusi maana huko ushahidi huwa mdogo sana ila huwa tunaishia kuona matokeo yake tu ya mwisho! Hili la Kenya na viwanda sitaki kuliingilia ila halihusiki sana kwa kufeli kwetu, Settlers walifungua viwanda kule coz ile nchi ilikuwa yao settlers so waliiendeleza utaona tofauti iliyokuwepo baada ya kupata uhuru ilikuwa ni mfumo wa kiuchumi, makampuni makubwa ambayo sisi tulisema ya 'mabeberu' tayari yalishajenga viwanda huko Kenya mfano ni Nestle (part ya Unilever) sisi tukakomaa na mashirika yawe ya serikali kitu ambacho hata nchi za magharibi zilishashindwa zikaamua kuwezesha watu binafsi (angalia mfano wa Telegram toka ugunduzi, kufeli ikiwa chini ya serikali na mpaka kubinafsishwa)
Sawa hapo tuko sambamba, na utakubaliana na mimi kompyuta ndio inahusika hata katika kuongoza hizo ndege zenyewe ikiwemo umbali toka ardhini (VNAV) uelekeo wa ndege (LNAV) na hata AUTOLAND kupitia control system ya computer ya ndege (FMS - Flight Management System) ile kauli yako ya "computer haiwezi kushusha ndege tumeizikia hapo kuwa haikuwa sahihi", kwa maoni yangu computer ndiyo iliyovamiwa na kuleta hitilafu hatimaye yakatokea majanga unaweza kuangalia tweet ya Boeing walichojibu kipindi kuna tetesi za kuvamiwa na virus walikubaliana kuwa wako under attack ya computer systms zao angalia kwenye link hapaMkuu kuna sehemu hujanielewa vizuri, computer kwenye ndege ndo kila kitu Kwa maana ya kwamba,kuanzia Engine, mfumo wa umeme, mafuta, hali ya hewa na nk vyote vinaripotiwa na Computer ufanyaji kazi wake, kila kitu kinajitegemea kufanya kazi lakini computer inachota Taarifa na rubani kujua status ya ndege kwa wakati husika ,lakini computer haiifanyi engine iwe na efficiency ktk ku operate kazi ya computer kufanya Delivery Report of the relevant device, kwa mfano taa zikiungua kwenye ndege computer inatoa Taarifa kuwa taa zimeungua lakini siyo computer ndo imeunguza taa, sasa computer itawezaje kufanya Engine ya ndege ifeli?
Sent using Jamii Forums mobile app
Nakushukuru sana mkuu umekuwa bega Kwa bega na mimi hatimaye ukweli umedhihirika kuwa kweli Boeing wamehujumiwa na majasusi ili kuiharibia biashara yaoSawa hapo tuko sambamba, na utakubaliana na mimi kompyuta ndio inahusika hata katika kuongoza hizo ndege zenyewe ikiwemo umbali toka ardhini (VNAV) uelekeo wa ndege (LNAV) na hata AUTOLAND kupitia control system ya computer ya ndege (FMS - Flight Management System) ile kauli yako ya "computer haiwezi kushusha ndege tumeizikia hapo kuwa haikuwa sahihi", kwa maoni yangu computer ndiyo iliyovamiwa na kuleta hitilafu hatimaye yakatokea majanga unaweza kuangalia tweet ya Boeing walichojibu kipindi kuna tetesi za kuvamiwa na virus walikubaliana kuwa wako under attack ya computer systms zao angalia kwenye link hapa