Parking za Kibo Complex (Tegeta) kuna vinara wa wizi

Parking za Kibo Complex (Tegeta) kuna vinara wa wizi

Siku hizi sehemu nyingi sana za biashara zenye parking wameshamaliza huo wizi wa kijinga kijinga wa kwenye magari. Hao Kibo Complex wapo dunia gani kujua sasa kwenye maendeleo ya teknolojia taarifa hasa zikiwa mbaya zinasambaa haraka sana kuwafikia watu kwa muda mfupi. Kwa kifupi huyo mmiliki ana uwezo wa kulimaliza hilo tatizo ndani ya muda mfupi iwapo kama kweli ana dhamira ya kulimaliza. Suala hapo awaondoe walinzi wote na kuajiri kampuni mpya ya ulinzi yenye walinzi waaminifu basi.
Yeye msaki anatumia walinzi wake binafsi na wala hakuna kampuni inayolinda pale zaidi ya wale wanaolinda benki basi
 
Parking at your own risk haiondoi liabililty ya mmiliki wa premises hayo ni maneno tu kisheria huyo mwenye eneo anawajibika kwa kitu kinaitwa occupiers liability mzee kuijua sheria ni raha sana...hapo kesi mahakamani mwenye eneo anakulipa vizuri sema muda mwingi utapotea mahakamani
Sawasawa mwanasheria msomi nimekupata ila mwenye uzi hana mpango wa kushtaki mtu yeye anataka kuroga na tayari wadau mbalimbali wamejitokeza kumsaidia...!!!
 
Parking at your own risk haiondoi liabililty ya mmiliki wa premises hayo ni maneno tu kisheria huyo mwenye eneo anawajibika kwa kitu kinaitwa occupiers liability mzee kuijua sheria ni raha sana...hapo kesi mahakamani mwenye eneo anakulipa vizuri sema muda mwingi utapotea mahakamani
Ata lipwa je? Wakat gari haija vunjwa sasa polisi wataamini vipi kama kaibiwa maana gari alilifunga na funguo na fungua akukabidhi Kwa mtu yoyote
 
Yeye msaki anatumia walinzi wake binafsi na wala hakuna kampuni inayolinda pale zaidi ya wale wanaolinda benki basi
Ngoja nichambue kidogo taarifa zilizoletwa na wachangiaji hapa:-
  • Anatumia walinzi wake binafsi
  • Wateja wanalalamika wanaibiwa kila siku
  • Mmiliki wa eneo haumizi kichwa kuondoa hilo tatizo
  • Anazo CCTV kamera lakini hataki zitumike baada ya wateja kuibiwa.
Naomba niishiie hapa hapa na uchambuzi wangu wa michongo.
 
Pole sana...

Weka gari lako alarm...

Pia ukishashuka na uka lock gari hakikisha unakagua milango yote Kwa kushika vitasa na kufanya kama unafungua...
 
hapana, nilipaki kwa kujua ni parking za hapo,nikaingia ndani kwajili ya kupata chakula
Ila mazoea bwana, mimi huwa siachagi kibegi cha laptop kwenye Gari, natoka nacho, bongo njaa sana aisee...
 
Pole sana. Ila ulinzi na umakini uanze na wewe mwenyewe unayejua thamani ya mali unazoacha ndani ya gari.

Valuables hata siku moja usiache ndani ya gari, haijalishi walinzi wapo au la. Waachie gari walinde lakini sio vilivyomo ndani ya gari maana hata hivyo hawahusiki na vilivyomo ndani ya gari maana hujawakabidhi vilivyomo ndani umekabidhi gari. Ni muhimu kujua tofauti ya hiki kitu.

Laptop, phones, cash money, bank cards, IDs never leave on the car. Beba ndio maana laptop ina potable bag. Usione uvivu, beba nenda nayo restaurant au popote, your laptop must be with you. Hata iwe parking ya kanisani au msikitini, never trust a human being.
 
Mwizi akiona laptop kwenye gari akuna namna ataacha,hata kwa kuvunja kioo atavunja tu aichukue.
 
Habarini wapendwa

Naandika hivi sio kwa kuchafua brand ya mtu ila wahusika wa parking za hapo kibo complex kuna jambo linajificha.

Nimeibiwa laptop na nyaraka kibao kwenye begi zikiwa ndani ya gari ambayo niliegesha pale, na kuingia kupata chakula.

Lakini nimeomba ushirikiano kutoka katika uongozi, tuangalie camera ili kupata ufumbuzi wa kupata vitu vyangu ila majibu yanakuja kuwa camera za kibo complex ni kwajili ya kuangalia mali za kibo complex sio mali za mteja.

Polisi wanasema kuwa pale kumeshakua na kesi nyingi za wizi na mhusika wa camera pale kibo complex hajawahi kutoa ushirikiano wowote.

Nimeshindwa kuelewa kuwa police wanamuogopa mhusika au kuna kitu kinajificha nyuma ya pazia???

NB. Gari haijavunjwa hata kioo, vitu vimeibwa na walinzi wanajibu jeuri.

Nimechanganyikiwa, sijui cha kufanya

asanteni
Fungua kesi mahakamani, mahakama itaomba hizo clip zitumike kama ushahidi na polisi watazipewa
 
Polisi wanasema kuwa pale kumeshakua na kesi nyingi za wizi na mhusika wa camera pale kibo complex hajawahi kutoa ushirikiano wowote.

Nimeshindwa kuelewa kuwa police wanamuogopa mhusika au kuna kitu kinajificha nyuma ya pazia???
Hao walinzi wana mamlaka juu ya polisi au?
 
Roga tu hao mwizi lazima aadhibiwe kwa kila namna we leta udini tafuta fundi uone najua ntashambuliwa hapa ila nasema hivi mimi mbuzi wangu wanne tu nimepeleka kesi nnapopajua sasa hivi heshima na adabu mji mzima n.b sikuwa naamini mambo hayo lakini yakikukuta mbona utajua hujui
Uko sahihi Mwamba
 
Siku hizi sehemu nyingi sana za biashara zenye parking wameshamaliza huo wizi wa kijinga kijinga wa kwenye magari. Hao Kibo Complex wapo dunia gani kujua sasa kwenye maendeleo ya teknolojia taarifa hasa zikiwa mbaya zinasambaa haraka sana kuwafikia watu kwa muda mfupi. Kwa kifupi huyo mmiliki ana uwezo wa kulimaliza hilo tatizo ndani ya muda mfupi iwapo kama kweli ana dhamira ya kulimaliza. Suala hapo awaondoe walinzi wote na kuajiri kampuni mpya ya ulinzi yenye walinzi waaminifu basi.
Basi hapa hapa JF tuanzishe kampeni ya kususia Kibo Complex
 
Back
Top Bottom