Paris Saint-Germain Special Thread

Kinachovutia zaidi ni kwamba si tu kwamba PSG wameweka rekodi, bali waliongeza magoli mawili zaidi na kuidhalilisha Celti kwa kichapo cha mabao 7-1 wakiwa wamebakiwa na mechi moja.

Lawama pekee kwa PSG ni kwamba waliruhusu goli. Goli la Celtic la kufungua ukurasa wa mbao halikuwa maana yoyote, ila kumbukumbu mbaya kwao mwisho wa mchezo, lakini ilikuwa mara ya kwanza kwa PSG kuruhusu goli hatua ya makundi.
Goli hilo pia lilikuwa la haraka zaidi ambalo klabu hiyo ya Ufaransa iliruhusu kwenye michuano ya UEFA.
 
Achilia mbali goli lolote, PSG wamekuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kutawala mchezo katika hatua ya makundi, wakiwa wameigaragaza Bayern Munich, Anderlecht na Celtic, timu nyingine za Kundi B. Wameshinda kila mechi kwa angalau magoli matatu.
Celtic wamepata kipigo kizito kwa kufungwa 12-1 katika mechi mbili, na wamekuwa vibonde wa PSG walioshinda kwa kishindo Ligi ya Mabingwa Jumatano.

Hata hivyo, licha ya umahiri wao katika kumiliki mchezo, PSG bado hawajamaliza kazi kwenye kundi lao. Bayern Munich wapo nyuma yao kwa pointi tatu na timu hizo zinatarajiwa kukutana kwenye mechi ya mwisho hatua ya makundi Disemba 5. Bayern wanataka kulipa kisasi cha kipigo cha 3-0 Parc des Princes, ikiwa wataweza kuibuka na ushindi wa mabao manne, watafaanikiwa kuipiku PSG na kukaa kileleni mwa kundi.
 
Badilisheni kocha lasihivyo mkikutana na timu zenye makocha wazoefu Kma chelsea au allegri mtadhalilishwa na mastaa wote waliojazana humo

PSG ilifaa kuwa na kocha world class sio huyo mbabaishaji
 
PSG ni moja ya timu bora kwasasa duniani.
Aaaah wapi wamekutana na vibonde ila wakikutana na miamba ya Ulaya Kma barca au timu yoyote kutoka madrid ndio itakuwa kipimo ya kiwango chao katika world stage sio vibonde Kma Sc anderlecht
 
Bayern Munich ni vibonde!?
Kwa ulaya anasubiri kwa atletico na real bia barca na juve hizo timu bayern haziwezi hivyo ndio kipimo kwa PSG ila bayern imechoka cku hzi nahisi sababu hakuna competition ndani ya ligi yao
 
Kwa ulaya anasubiri kwa atletico na real bia barca na juve hizo timu bayern haziwezi hivyo ndio kipimo kwa PSG ila bayern imechoka cku hzi nahisi sababu hakuna competition ndani ya ligi yao

Tusishindane sana, muda utaongea!!!!
 
Tusishindane sana, muda utaongea!!!!
sawa maana naona mashabiki wa PSG Wanaongezeka kwa mihemko kma ilivyokuwa leicester city kipindi inachukua ligi ingawa watu hawakujua experience counts cku mkikutana na simeone utaelewa naongelea nni

anyway muda utaongea
 
RONALDO AANZA MAZUNGUMZO NA PSG


Cristiano Ronaldo amemwambia wakala wake Jorge Mendes kuanza mazungumzo na Paris Saint-Germain, kwa mujibu wa DiarioGol .
Inadaiwa kuwa Mreno huyo anataka aidha kuongezewa ujira Real Madrid au kuondoka mwishoni mwa msimu huu, ombi ambalo rais Florentino Perez hana mpango wa kulifanyia kazi.
 
PSG YAIPIKU MAN CITY MBIO ZA ALEXIS


Paris Saint-Germain inaitangulia Manchester City katika mbio za kumfukuzia nyota wa Arsenal Alexis Sanchez Januari, The Mirror limeripoti.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Chile unafikia ukomo mwisho wa msimu huu, na PSG imeripotiwa kuwa kwenye mchakato wa kumsajli kwa mkataba wa awali wanapojipanga kumruhusu Neymar kwenda Real Madrid msimu ujao wa majira ya joto.
 
PSG kumfunga Bayern kusiwape confidence kupita maelezo, kama PSG walielewa kwanini kocha wa Bayern alitimuliwa baada tu ya kufungwa na PSG basi PSG wakae wakitambua kwamba hii ni dharau kubwa sana kwao na bado wana kazi kubwa sana ya kuprove wao ni the best in the World the like of Real Madrid, Barcelona etc. Otherwise time will tell, let's wait.
 
PSG ni timu itakayopotea keshokutwa tu wala siku si nyingi.

Yaani kumfunga tu Bayern Munich mkaanza kuisifiia na kuipa ubora?

Timu zingine zilizofungwa na PSG ni za kawaida tu.

PSG bado sio timu ya kuiamini kwa 100% .

Subirini muone.
 
Kung'utwa kule
Pigwa sana ka mbwa mwizi
Kumbe Paris nguvu ya soda tu
Bayern kakuweka swafii kabisa
Mi nilitaka upangwe na Madrid 16 bora kumbe nawe walewale 2 si atakutoa
Ila naomba upangwe nae tu siwapendi wale majamaa
Naaminia neymar mtayatoa tu yale majamaa ila si barca
 
Ayo ni matokeo baada ya kuwaeka nje best players wa timu . Cavani & Verrati. kina mbape, neymar hawazidishi hawapunguzi.


Matokeo ya jana Cavani na Verrati walikuwepo. Uwepo wao haukuzuia kipigo cha Pili. Nguvu ya Soda imeisha?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom