Paris Restaurant Shootings and Blasts: at least 100 People have been killed

Paris Restaurant Shootings and Blasts: at least 100 People have been killed

Status
Not open for further replies.

Observer

JF Member
Joined
Oct 18, 2006
Posts
195
Reaction score
378
Watu 100 mpaka sasa wamethibitishwa kufariki kutokana na matukio ya kulipuka kwa mabomu na kupigwa risasi katika mitaa ya Paris

Watu 100 wasadikiwa kuwa wameshikiliwa mateka

UPDATE 1 : Idadi ya watu waliofariki imefikia watu 40 mpaka sasa

UPDATE 2
: Polisi wavamia Bataclan Concert Hall: Watekaji 2 wauawa, Watu 100 wafariki

UPDATE 3
: Zaidi ya watu 140 wanaaminika kuuwawa kwenye matukio hayo

====================================

2-2-589x442.jpg

cegrab-20151113-213450-801-1-736x414.jpg

attachment.php


At least 118 people have been killed inside the Bataclan concert hall where attackers seized hostages, police officials say.

Elite police commandos launched an assault on the venue and killed two gunmen - but were unable to save the hostages.

One official described "carnage" inside the building, saying the attackers had tossed explosives at the hostages.

Witnesses outside the venue in the 11th arrondissement reported hearing five successive explosions followed by gunshots.

President Francois Hollande and other top government officials have arrived at the scene.
Officials said they expected the toll of victims to rise.

Earlier, UN secretary general Ban Ki-moon demanded "the immediate release" of the hostages in the theatre.
US band Eagles Of Death Metal was scheduled to play to a sell-out crowd at the Bataclan.

In a Facebook post, the management for the band said: "We are still currently trying to determine the safety and whereabouts of all our band and crew.

"Our thoughts are with all of the people involved in this tragic situation."

At least 40 other people have been killed in other locations in and around Paris in what Mr Hollande has described as "unprecedented terrorist attacks".

Source: Sky News
Watu 120 wauawa katika mashambulio Paris
151114073934_bataclan_theatre_survivors_512x288_epa.jpg
Image copyrightEPAImage captionManusura wamekuwa wakiondolewa eneo la Bataclan kwa mabasi


Ufaransa imetangaza hali ya hatari na kufunga mipaka yake baada ya watu zaidi ya 120 kuuawa kwenye mashambulio kadha mjini Paris.
Watu 120 wameuawa katika ukumbi wa sanaa wa Bataclan, katikati mwa mji wa Paris.
Watu wenye silaha walishika mateka watu waliokuwa kwenye ukumbi huo kabla yao kuzidiwa nguvu na maafisa wa polisi.
Watu wengine waliuawa kwenye mlipuko uliotokea karibu na uwanja wa michezo wa taifa wa Stade de France ambako mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Ujerumani ilikuwa ikiendelea.
151114021413_spectators_512x288__nocredit.jpg
Mashabiki waliingia uwanjani baada ya milipuko kutokea Stade de FranceWasimamizi wa mji wa Paris wamewataka raia kusalia manyumbani na wanajeshi 1,500 wametumwa kushika doria Paris.



Shambulio mbaya zaidi linaonekana kuwa hilo la Bataclan, ambako ripoti zinasema watu waliokuwa wamehudhuria tamasha ukumbini walipigwa risasi na kuuawa baada ya kushikwa mateka.



Akiongea baada ya kufika katika ukumbi huo baadaye, Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameapa kuwa wahusika watakabiliwa "bila huruma".
151113233425_sp_paris_hollande_640x360_afp.jpg
Rais wa Ufaransa Francois Hollande amehutubia taifaMashambulio mengine yalitokea karibu na mighahawa ya Le Petit Cambodge na Le Carillon katika mtaa nambari 10 ambako mwandishi wa BBC anasema aliona watu 10 wakiwa wamelala chini, wakiwa wamejeruhiwa vibaya na wengine kufariki

Mtu aliyeshuhudia ameambia gazeti la Liberation kwamba naye alisikia risasi zaidi ya 100 zikifyatuliwa katika mghahawa wa La Belle Equipe katika mtaa nambari 11.
Milio ya risasi pia ilisikika katika kituo cha kibiashara cha Les Halles.


Rais wa Marekani Barack Obama amelitaja shambulio hilo kuwa "jaribio lisilokubalika la kuhangaisha raia wasio na hatia" na kuahidi kusaidia Ufaransa kukabiliana na waliohusika.


"Hili si shambulio tu dhidi ya raia wa Ufaransa. Ni shambulio dhidi ya binadamu wote na maadili yetu ya pamoja," amesema.
151114010400_french_police_512x288__nocredit.jpg
Hawa ni polisi wa Ufaransa wakiwa karibu na eneo la ukumbi wa Bataclan"Tutafanya kila tuwezalo kuwasaidia watu wa Ufaransa na mataifa kote duniani kuhakikisha magaidi hawa wanakabiliwa."


Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amesema ameshtushwa sana na shambulio hilo na kuahidi kufanya "lolote tunaloweza kufanya kusaidia."

Chanzo:
BBC

Hollande atangaza kundi la IS limehusika katika mashambulizi ya Paris

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema mashambulizi yaliyofanyika katika maeneo kadhaa Paris yamefanywa na kundi la wanamgambo wenye itikadi kali wa dola la kiislamu IS.

Hollande amesema mashambulizi hayo ndiyo mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Ufaransa katika kipindi cha miongo mingi na ametangaza siku tatu za maombolezi nchini humo.

Idadi ya watu waliouawa katika mashambulizi mjini Paris yaliyofanyika jana usiku imeongezaka hadi watu 128 huku wengine 200 wakiwa wamejeruhiwa, 80 kati yao wakiwa katika hali mahatuti.

Inakisiwa kuwa takriban washambuliaji wanane, wote wakiwa wamevaa fulana zilizojazwa viripuzi, walifanya mashambulizi mabaya kuwahi kutokea barani Ulaya tangu mashambulizi ya mabomu katika kituo cha treni cha Madrid, Uhispania mwaka 2004.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametangaza hali ya hatari nchini humo pamoja na kuamuru wanajeshi 1,500 wa ziada kushika doria katika maeneo ya mji huo.

Maeneo ya umma yafungwa

Hadi sasa hakuna mshukiwa aliyekamatwa . Polisi wanaendelea kufanya uchunguzi kwa kupitia video zilizonaswa katika maeneo tofauti. Maeneo ya umma kama shule, makumbusho, mabwawa ya kuogelea,maktaba na vituo kadhaa vya usafiri yamefungwa.

Kundi la wanamgambo la dola la kiislamu IS limetoa video hii leo ikitishia kuishambulia Ufaransa iwapo nchi hiyo itaendelea kuwashambulia wanamgambo hao.

Jumuiya ya kimataifa imelaani mashambulizi hayo ya Paris. Miongoni mwa viongozi waliolaani mashambulizi hayo ni Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ambaye amesema amehuzunishwa na kushtushwa mno na mashambulizi hayo na kuapa kuwa watafanya kila wawezalo kuwasaka washambuliaji na wanaowaunga mkono.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema watafanya kila wawezalo kuisaidia Ufaransa. Umoja wa Ulaya pia umelaani mashambulizi hayo na kuyataja kuwa vitendo vya kinyama huku ikiahidi kusimama na Ufaransa katika kipindi hiki kigumu.

Katibu mkuuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amesema ameshitushwa sana na mashambulizi hayo ya kigaidi.

Jumuiya ya kimataifa yalaani mashambulizi

Kutoka Marekani Rais Barack Obama amesema mashambulizi hayo ni dhidi ya ubinadamu na maadili ya dunia nzima. Rais wa China Xi Jinping amempigia simu Rais wa Ufaransa Francois Hollande na kusema China inayalaani vikali mashambulizi hayo ya kinyama na kuongeza kuwa wako tayari kujiunga na juhudi zozote za kuimarisha usalama na kupambana na ugaidi.

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesitisha ziara yake ya nchini Italia na Ufaransa kufuatia mashambulizi hayo aliyoyataja kuwa ni uhalifu dhidi ya binadamu.

Rais wa Syria Bashar Al Assad ameyalaani mashambulizi hayo na kusema mashambulizi kama hayo ya kigaidi ndiyo wamekuwa wakipitia nchini Syria kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ameitisha mkutano wa baraza la usalama la Uingereza kufuatia mashambulizi hayo. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ambaye ameahidi kushirikiana bega kwa bega na Ufaransa kupambana na ugaidi pia amesema atakutana na mawaziri wake hii leo kujadili hali hiyo ya Ufaransa na masuala yanayohusiana na mashambulizi hayo ya Paris yaliyotokea katika sehemu mbali mbali za umma jana usiku.



Chanzo:
DW
 
Very sad indeed! Fench President has declared State of Emergence, French Borders Closed!

Watu walikuwepo uwanjani wakiangalia game ya France vs Germany, na Rais wa Ufaransa alikuwemo humo...wakasikia vishindo nje wakawa wanashangilia wasijue ni mabomu yanalipuka...baadae mchezo ukasimamishwa na Rais akapelekwa sehemu salama.....



Later French police were involved in a hostage-rescue operation, gunfire heard, Hostage Siege at BataclanConcert Hall Over....CNN

The latest reports, from French media, say at least 153 people are dead .CNN



Agence France-Presse
AFP


#BREAKING Three suspected attackers killed in police raid on Paris concert hall: police



attachment.php
 

Attachments

  • 460x.jpg
    460x.jpg
    25 KB · Views: 6,881
Last edited by a moderator:
Dah, leo hii hii nimetoka kusikia wamarekani wakisema wamemuua 'Jihad John", ama ndo kisasi cha ISIS
 
Siyo ufaransa tu. Bali ni waislam walioko ulaya hufurahia matukio kama haya. Na kibaya wanawakaribisha isis toka syria bila kujua. Thanks God waislam wengi wa tz ni waelewa.

Haya mambo sio ya kufurahisha maana wanaokufa ni watu wa aina tofauti {kiitikadi/kiimani}.... na sio wote wanaofurahia matendo hayo.

Ila Ufaransa wawe waangalifu sana maana hivi vitendo vya kigaidi vinaongezeka siku baada ya siku
 
Hawa hawa walimuua Ghadafi sasa libya imegeuka sehen salama hawa magaidi kujifunza na kuja kuwapiga huko
 
So sad!! MTU yeyote anayeua binadam asiye na hatia ni mnyama hapaswi kupewa heshima ya ubinadamu!
 
What's goes around comes around, mlipokwenda kuchafua nchi zao kwa kile mnakiita demokrasia ndio majibu hayo, hakuna nchi ya kiarabu inayounda silaha, zote zinatoka kwao, wanawagawia kama njugu nia yao wamalizane, sasa silaha wamezizoea sana tu na sasa zinarudi zilikotoka, tena kwa kazi ile ile,
Zile vurugu tulizizoea kuziona middle east sasa zitahamia Europe ni muda tu
 
CNN wanasema atleast 118 wameuawa,NBC wanasema atleast watu 100 wameuawa Ngoja niangalie channel nyingine sasa hivi hapa Inakaribia saa 2 usiku!na msnbc wanasema 140
 
Khatari kubwa, naona vyombo vya usalama vina changamoto kubwa kukabiliana na matukio ya aina hii maana ikiwa ulaya idara za usalama zina kila aina ya mbinu za kukabiliana na matukio ya aina hii zikiwemo CCTV, unasaji wa taarifa mawasiliano ya simu, intaneti, ukusanyaji wa taarifa za transaction za kibenki, tiketi za basi/treni zikionesha kila eneo unalopita n.k lakini bado matukio haya yanatokea basi ni kudra ya Mwenyezi Mungu tu nchi masikini zisiposhambuliwa.
 
Alafu huwa tunawacheka Wakenya eti wameshindwa kuwazuia Al-Shabab.. Hivi na hii mizungu nayo imeshindwa kuwamaliza hao watu kabisa?? Hili liwe somo kwetu pia, Waafrika hasa East Afrika tutafute suluhu ya kidiplomasia kati ya Al-Shabab na serikali ya Somalia kabla mambo hayajawa mabaya.. EA kuna mafuta na gesi sasa (Uganda, Kenya, Tanzania) tuwe macho na hawa Al-Shabab wasije wakaanza kutumika na Western Countries kuchafua amani tuliyonayo EA kwa manufaa yao binafsi..
 
Alafu huwa tunawacheka Wakenya eti wameshindwa kuwazuia Al-Shabab.. Hivi na hii mizungu nayo imeshindwa kuwamaliza hao watu kabisa?? Hili liwe somo kwetu pia, Waafrika hasa East Afrika tutafute suluhu ya kidiplomasia kati ya Al-Shabab na serikali ya Somalia kabla mambo hayajawa mabaya.. EA kuna mafuta na gesi sasa (Uganda, Kenya, Tanzania) tuwe macho na hawa Al-Shabab wasije wakaanza kutumika na Western Countries kuchafua amani tuliyonayo EA kwa manufaa yao binafsi..

Alshabaab, ISIS Boko Haram na the like yote ni makundi yaliyopandikizwa na western kwa malengo maalum. hao alshabaab kenya wanazuga na kupoteza muda tuu lkn mlengwa ni ww mwenye gesi na mafuta....kuna wanaodharau dhana hizi lkn huo ndio ukweli. Hatuko salama!...Hizi gesi zetu ndio kibiriti chetu!
 
nimekudharau sana kwa hii comment yako, bila shaka hilo shambulizi ni la waarabu na uislamu wao but watakamatwa tu coz waarabu akili zao fupi.

sasa wewe unachopinga nini?? nani anatengeneza hizo siraha? nani anawauzia ISIS, Alshababu na Boko Haram Siraha na magari ya kisasa? Hii Biashara inafanywaje Bila CIA kufahamu?.. Boko Haram aliye msituni analipataje gari la kisasa?? mtu anayedai kupinga elimu ya magharibi anawezaje kutengeneza videos na kuzirusha kwenye media bila CIA kufahamu? kwanini US ana support ISIS Syria?. mbona ukiamua kutumia akiliyako vizuri ni rahisi sana kuufahamu mchezo wote!...Hebu jitahidi kutumia akili yako basi kutoka kwenye box!
 
Alshabaab, ISIS Boko Haram na the like yote ni makundi yaliyopandikizwa na western kwa malengo maalum. hao alshabaab kenya wanazuga na kupoteza muda tuu lkn mlengwa ni ww mwenye gesi na mafuta....kuna wanaodharau dhana hizi lkn huo ndio ukweli. Hatuko salama!...Hizi gesi zetu ndio kibiriti chetu!

Kabisa mkuu.. It is just a matter of time.. Tukiendelea kulala na kuona hao Al-Shabab si threat kwetu itakuja kutugharimu mbeleni.. We have to outsmart these Western Countries katika hili
 
ni muhimu kwetu sote hasa ambao sio waislam, kuelewa kwamba Islam sio terrorism, kuna waislamu wapatao bilioni 1.6 duniani, wangapi kati ya hao wanajihusisha na terrorism au wanaamini kwenye kuua watu wasio na hatia? tusisahau kwamba ndani ya nchi kadhaa za middle east na kati ya middle east na nchi zilizoendelea kuna matatizo makubwa na complicated yenye historia ndefu, na wanaokufa na kuteseka zaidi na haya matatizo ni watu wa middle east ambao ni waislam. Tuombee amani ya dunia nzima
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom