Papaa Msofee alitia Doa Jeshi la Polisi na kumuaibisha Mama Tibaijuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Papaa Msofee alitia Doa Jeshi la Polisi na kumuaibisha Mama Tibaijuka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ray 4, Nov 4, 2011.

 1. R

  Ray 4 Member

  #1
  Nov 4, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wiki hii imeripotiwa katika taarifa ya habari ya saa mbili ITV kwamba mama mmoja mjane kiwanja chake kimevamiwa na mfanyabiashara maarufu Marijani Msofe au kama anavyojulikana mtaani Papa Msoffe. Mama huyu alisema Polisi walimtoa na kumuomba Waziri Mkuu amsaidie.

  Leo tarehe 04/11/2011 taarifa ya habari ya saa mbili ya ITV naona huyu mama akitoa shukrani kwamba Waziri Mkuu amemsaidia kumtoa mvamizi kwakumpa siku 7. Katika taarifa ya habari hiyo watu walichangia na kuelezea jinsi wanyonge wanavyodhulumiwa na watu wenye fedha kwakutumia vyombo vya umma na hasa Polisi. Natumai taarifa hii itarudiwa tena kesho asubuhi saa kumi na mbili au saa moja katika kituo hichohicho cha ITV.

  Swali nililojiuliza ni kwamba Polisi waliezaje kumtoa mama wa watu ambaye tunaambiwa alikuwa na documents zote hali ambayo inaniambia ndio maana ikawa rahisi kwa waziri mkuu kutoa uamuzi wa haraka. Mama huyu mjane nampa hongera kwa jinsi alivyopigana kijasiri kwani ni watu wachache sana wanaweza kupitia ngazi zote alizopitia.

  Maswali ambayo nabaki nayo ambayo sijapata majibu na naomba wadau wanifumbue macho ni haya?

  1. Huyu Papa Msoffe au marijani msoffe ni nani hasa?

  2. Amewezaji kutumia Jeshi letu kufanya hayo aliyofanya bila hata Polisi mmoja wa ngazi za juu kuthubutu kukemea, kuwawajibisha polisi waliohusika au hata kutoa tamko?

  3. Inawezekanaje serekali inampa mhalifu siku 7 arudishe alichoiba bila hata yakumfungulia shitaka la hata mstari mmoja?!!

  4. Mama Tibaijuka ambaye tunamuamini ameweza kumtosa mama mjane na kuwekwa mfukoni na hawa waalifu mpaka waziri mwingine kuingilia na kutoa ufumbuzi?

  Tutafika kweli? Labda kuna ambalo limejificha, naomba nipewe mwanga.
   
 2. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,860
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kuna school of thought moja inasema sheria ziliundwa na watawala ili kuwasaidia kutawala na wanyonge wazitii sasa we angalia nani kaundiwa hizo sheria mtu anadhulumu anaamriwa kurudisha. Ndio hivyo lakini ashukuru karudishiwa apige kimya baaas.
   
 3. m

  myf Member

  #3
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  The world is injustice from time immemorial hivyo usishangae,migodini wanauwawa wa tu hakifanywi chochote.
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 32,251
  Likes Received: 15,048
  Trophy Points: 280
  Papaa Msofe ni rafiki wa M'kwere, ndio maana hata polisi na mahakama zinamuogopa
   
 5. G

  Godwine JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,362
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  msofe ni jamaa anayepata fedha kwa wizi ni mzaliwa wa kongo, kazi yake kubwa ni utapeli wa kimataifa
   
 6. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,854
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  Vigogo wengi wa Police wapo ktk payroll ya Msofe ndo maana anatapeli wazungu,na ata ao wazungu wanapoomba msaada police wanaishia kurudishwa kwao na next flight kwao,pale central kuna makumi ya kesi zake lakini anakula kuku tu mitaani.police anawalipa thus why yupo protected nao
   
 7. T

  The Priest JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,024
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  I hate u papaa musofe!go back to ur country
   
 8. N

  Nagoya Member

  #8
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Police na wizara ya ardhi wabadilishiwe viongozi ningependekeza msofe na mzanili wapewe nafasi hizo, kwani wao wanajua kugawa viwanja vizuri na kuweka ulinzi. Cheche za waziri mkuu zitazimwa muda sio mrefu. Kwani waziri mkuu hujui kuwa viwanja anavyotapeli msofe na muzamili ni mali ya alshabaab?

  Pole sana waziri mkuu hao jamaa waliuza kiwanja cha mama rwakatare mbunge!!! Sembuse mjanea.

  Bado kidogo ukistaafu watauza cha kwako.

  Nadhani ingekuwa ni busara kuhoji nguvu yao chanzo chake kabla hujatoa uamuzi, maana walinzi wenu wa ikulu humpa msofe na muzamil taarifa kabla yenu in short wanaheshimika na kukubalika kwa majeshi yote nchini isipokuwa jwtz tu ndio litabaki mkombozi wetu dhidi ya vikosi vya kisomali vinavyofanya uwekezaji na matapeli muzamil na mfofe.

  Warizi mkuu kwani wewe hujapewa fedha za kampeni na hawa jamaa? Kama rais wako alipewa bila shaka na wewe ulipewa, nadhani hutarajii kugombea tena ubunge ndio maana umejikakamua kutoa siku saba kirudiswe bila sharti lolote, hongera waziri mkuu kwani umejikakamua sana hawa jamaa hawakamatiki walisha wazidi mahesabu zamani kinga yao dhidi ya sheria ni kubwa kuliko ya mbunge,

  Kwani hiyo ni nyumba ya kwanza ya mjane kudhulumiwa??? Mbona muzamili alidhulumu nyumba ya mjane sinza na kujenga ofisi yake na kumbana mama mjane uwani akiwa kama kanyumba ka mlini na kuzibiwa njia ya kuoingia ndani ya kakibanda kake. Itv pia iliripoti lakini hukutoa siku 7, au msofe hajakujengea jumba la ufalme kama zawadi ya kuchaguliwa mara ya pili kuwa waziri mkuu??

  Nenda sinza kaangalie unyama uliofanywa na muzamili kwa mjane mwingine.

  Kama jeshi la police lilishiriki kwa nini usianze na wizara kwanza, kisha jeshi halafu umalizie na boss wao msofe,

  Waziri mkuu hivi umejiuliza hawa watu fedha zao zinatoka wapi????

  Pole sana pinda nadhani huwajui vizuri hawa jamaa, siku moja utajua nilikuwa namaanisha nini! Fafanua hili balis likusaidie katika utendaji wako wa kazi na kujua taifa letu liko wapi nadhani wewe umesomea mambo ya usalama na umefanya kazi usalama wa taifa kwa muda mrefu sana tangu ukiwa kijana (hawa jamaa wana uwezo mkubwa wa kumshauri rais jambo kuliko wewe) ikulu imekuwa ya kibiashara tu kazi zenu ni kupanga mikakati ya kufelisha wanaharakati na kutawala kilaini. Wakati msofe na mzamili wakiwaandalia karamu za pongezi na kushiriki nanyi katika mambo mnayoyaagiza, hivi tukiangalia namba ya msofe na mzamil wanapata simu ngapi kutoka ikulu kwa siku? Je rais huongea nao mara ngapi kwa wiki?? Je ni tenda zipi hufanya na mtoto wa rais aka ridhiwani je ridhiwani hana viwanja alivyopewa na hawa jamaa mfofe na muzamil???

  Waziri mkuu umekurupuka kama ulivyokurupuka kwa david jairo.
   
 9. N

  Nagoya Member

  #9
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sio mkongo ni mpare anaeshirikiana na wakongo kutapeli
   
 10. N

  Nagoya Member

  #10
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haaswa tena ni mshauri wa ****** mambo ya madini na ardhi
   
 11. N

  Nagoya Member

  #11
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haaswaaa tena ni mshauri wa raisi wa mambo ya madini na ardhi.
   
 12. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #12
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  The day will come na watu kama hawa na vizazi vyao kupotezwa ktk nchi hii....
   
 13. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #13
  Nov 5, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,321
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Jamaa bado anawaliza tu wanene?
   
 14. Masakata

  Masakata JF-Expert Member

  #14
  Nov 5, 2011
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Eti utasikia sisi CCM tunajali wanyonge..hakuna lolote, matajiri  wanaiba BOT wanaambiwa warudishe,huyu nae anamdhulumu mjane,nae anaambiwa arudishe,hv sheria za nchi ndio zinasema WEZI na WANYANG'ANYI wakirudisha walivyoiba na kupora ndio BASI?..halafu MNAAPA tena mkiwa mmeshika BIBLE na MSAHAFU ya kwamba ;mtaisimamia na kuilinda katiba ya nchi..shame on you!!!!
   
 15. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #15
  Nov 5, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,317
  Likes Received: 4,722
  Trophy Points: 280
  binafsi sio mpenzi wa bongofleva lakini Joseph Haule amewahi kusisitiza kuwa "aliye juu mfuate hukohuko, usingoje chini maana unaweza kusubiri milele".
  Sual la polisi (na taasisi zingine za umma endapo umekutana nazo) linakatisha tamaa. Kwanza uwezo wao wa kuchanganua mambo (walio wengi) ni mdogo mno na katika umaskini na rushwa iliyotuzingira ndio taabu inazidi. Pia kuna suala am
  balo nimesikia baadhi ya polisi wenyewe wakiliongelea la Ukabila/udini, udugu na kujuana kutumika katika kupeana kazi na kugawana vyeo.
  Cha msingi hapa, bila wewe na mimi kusema kwa nguvu zote "HAPANA", akina Papaa Msofe wataendelea kuinjoi na hata wakizeeka wakafa watoto wao nao wataendeleza hayohayo na watakuwa juu ya watoto wako pia. Tuamue haya mambo yaishe kizazi hiki na yasisubiri kizazi kijacho!
   
 16. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #16
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,112
  Likes Received: 2,218
  Trophy Points: 280
  Wapi ndama mutoto ya ng'ombe? Tanzania 4ever
   
 17. M

  Mkatakiu Member

  #17
  Sep 21, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanasema siku za mwizi ni arubaini. Hatimae Professional Cornman Marijani Msofe aka Papaa Msofe anganganiwa na vyombo vya sheria. Lakushangaza hapa ni kwamba tuliambiwa kesi yake imehairishwa kama mara tatu hivi kwasababu anaumwa na mwezi huu mwanzoni alikuwa afikishwe mahakamani lakini ghafla hatuambiwi tena nini kinaendelea! Au ndio tuseme ameshahonga hadi vyombo vya habari wasituletee habari? Nani anajua Kesi yake mwezi huu wamesemaje?
   
Loading...