Papaa Msofe, Alex Massawe wahukumiwa

Papaa Msofe, Alex Massawe wahukumiwa

cash flow imekata kwa Papaa..!!!teheteh..liquidity kushney.....
 
chuma cha reli papaa msofe ni mfadhili mkubwa wa ukawa
 
Polisi kama watangelikuwa makini, wakaongea vizuri na huyu Msofe, bila shaka wangepata fununu juu ya mauaji ya Marehemu ambaye sasa anasemwa aliuawa na watu wasiojulikana.
ushahidi ulikuwepo ili Kamanda Kinyela alikula hela sana za Msofe ili kuvuruga ushahidi na alifanikiwa..kisa hicho ndio kilimuondosha kuwa RPC Kinondoni sijui walimtupia wapi jamaa yule hakuwa muadilifu
 
Papaa Msoffe alishafirisika, hiyo Million 300 sijui ataipata wapi...

Alex Massawe anacheza na South Africa na Uarabuni, na alishamwambia Msoffe asijisumbue kumtafuta atampoteza..
 
Anafadhili kitu gani wakati hana hata kumi???

Kelele zake za mjini zilishaisha kitambo, unacheza na Massawe wewe...
Mkuu upo sahihi sasa hivi jamaa kaisha kawa mweusi tiiii..yaani nilikutana na dereva wake Hamisi Kitobo wanaendesha vioo wazi ili kusave wese
 
na hapo usikute yeye ndiye alimuua ili achukue nyumba kiulaini
Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, imetoa hukumu kwa mfanyabiashara Marijani Abubakar, almaarufu Papaa Msofe, Alex Massawe na Makongoro Nyerere kwa kosa la kughushi hati ya umiliki wa nyumba iliyopo Mikocheni jijini Dar, mali ya marehemu Onesphory Kituly aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi mwaka 2011.

Kesi hiyo iliyounguruma kwa takribani miaka saba tangu 2007, ilifikia tamati Desemba 22, mwaka huu na kuwakuta na hatia washtakiwa hao baada ya upande wa utetezi kushindwa kuwasilisha vielelezo vinavyowapa uhalali wa kumiliki nyumba hiyo.

Akisoma hukumu hiyo, jaji wa mahakama hiyo, John Nchimbi mbele ya wakili wa Msofe na wenzake, Majura Maghafu alisema kuwa baada ya kupitia hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili, mahakama imeamua kumtangaza mke wa marehemu Onesphory, Mary Kituly kuwa mmiliki halali wa nyumba hiyo.

“Pia mahakama imewatoza fani ya shilingi milioni 300, Papaa Msofe, Massawe na Nyerere pamoja na asilimia 12 ya fedha hizo kama fidia ya gharama za uendeshwaji wa kesi hiyo,” alisema Jaji Nchimbi.

Mara baada ya kusomwa hukumu hiyo, mke wa marehemu, Mary aliangua kilio cha furaha na nduguze mbele ya jaji baada ya kuona haki imetendeka, kitu ambacho hakuwa akikitarajia.

“Yaani siamini macho yangu, maana jinsi kesi ilivyonisumbua kwa miaka saba, nimefarijika sana kwa haki kutendeka maana nilikuwa nikishindana na watu wenye pesa, damu ya mume wangu haijapotea bure, namshukuru Mungu kwa kweli,” alisema Mary alipokuwa akizungumza na waandishi ambapo alimshukuru pia Rais John Magufuli kwani serikali yake inajali haki.

Msofe na wenzake walifunguliwa kesi katika mahakama hiyo mwaka 2007 baada ya kudaiwa kughushi hati ya nyumba kwa kuhamisha umiliki wa nyumba namba 288 iliyopo Mikocheni, Dar iliyokuwa ya marehemu Kituly na kuweka jina lake kisha kumuuzia Masawe kinyume cha sheria.

Ilidaiwa kuwa kabla ya kufariki dunia, marehemu Kituly alimkopa shilingi milioni 30 Msofe kwa dhamana ya hati ya nyumba hiyo kwa makubaliano ya kumrudishia kiasi hicho kwa muda wa miezi sita.

Inadaiwa kuwa baada ya miezi mitano, marehemu alipata kiasi hicho cha fedha na kurudisha kwa Msofe na kutaka hati yake, lakini alianza kuzungushwa kuanzia kipindi hicho hadi alipokufa kwa kuuawa na watu wasiojulikana mwaka 2011.

Oktoba 30, 2007, Msofe aliwatoa kwa nguvu marehemu, mke wake na watoto kwa madai kuwa nyumba hiyo imeuzwa kwa Massawe.
 
Mkuu upo sahihi sasa hivi jamaa kaisha kawa mweusi tiiii..yaani nilikutana na dereva wake Hamisi Kitobo wanaendesha vioo wazi ili kusave wese
Kwisha habari yake... Sasa hiyo Million 300 sijui ataitoa wapi..

Labda akae na Massawe aongee nae kiutu uzima..
 
At least.... Ila Mungu amlinde tu huyo Mama,maana hao ni watu hatari kudeal nayo,ngekuwa mie ngeshawaachia tu Mungu mgawaji wa vyote angenijalia nyingine tu.


Wasiwasi wangu ni hao jamaa wana mpango gani na huyo baada ya kushinda kesi na wao kumlipa 300M?!
Sidhani kama watamuacha,na ikitokea wakamfanyia lolote hata wakishtakiwa tayari huyo mama kashadhurika haitakuwa na faida maana uhai huwa haurudi mara mbili.


Ushauri wangu kwa wajane na yatima hata utapeli wa mirathi ukitokea ni kumuomba Mungu ndo apigane upande wake/kiroho kuliko kushindana kimwili.
Hizi akili ni mgando kabisa..Tukiwa hivi wote basi wageni watabeba gesi,Wanyama na makorokoro kibao huku wenyeji tukishindwa ata kupambana na kumuachia ambaye kwa sasa nafikiri hafanyi kazi mana kama angekuwa yuko on air basi tangu io 2007 Angefanya jambo..Tuachane na mambo ya kutegemea Vitu vya kufikirika (God)
 
Ni huyu Makongoro aliyekuwa anaita watu vibaka?

Au ni kibaka wa Mzee Butiku?
 
Papaa Msoffe alishafirisika, hiyo Million 300 sijui ataipata wapi...

Alex Massawe anacheza na South Africa na Uarabuni, na alishamwambia Msoffe asijisumbue kumtafuta atampoteza..
Ni kawaida ya manyamera KUJIKANA kikishanuka.
 
Connecting dots....Hao ndo walimuua marehemu...
 
Mbona sijaona wamefungwa miaka mingapi?
Baada ya Alex Massawe kutorejea Nchini (inasemekana alionekana Dubai akakamatwa hatumaye akatoroka na mara ya mwisho alionekana afrika ya kusini)
hivyo kesi ya Msofe ikabadilishwa na kuwa ya kugushi na kujipatia nyumba ya Kituly Mkibosho mwenzie na A.M. hivyo Msofe akatolewa rumande
Kesi ya mauaji imesimama hadi hapo upelelezi utakapompata AM
 
Last edited:
Back
Top Bottom