Papaa Msofe, Alex Massawe wahukumiwa

Papaa Msofe, Alex Massawe wahukumiwa

Na mm nachojiuliza makongoro nyerere cjui aliingiaje humo. Huyo papaa alisemekana kuhusika na mauaji, cjui kama justice iko hapa kiukweli.
Mashtaka ya mauaji alibadirishiwa wakampa mashtaka ya kughushi wakati massawe Akitokomea pasipojulikana
 
Bila kupepesa macho hata hicho kifo cha Tully with ni doubt wanahusika tu kwa Ushahidi wa Kimazingara
 
Hii kesi wangewaunganisha yule jamaa mjengwa.lukosi kris. waliokula pesa za mtoto wa mjane wa iringa.


swissme
 
Polisi kama watangelikuwa makini, wakaongea vizuri na huyu Msofe, bila shaka wangepata fununu juu ya mauaji ya Marehemu ambaye sasa anasemwa aliuawa na watu wasiojulikana.
 
Mali na hadaa za dunia zimewafanya wanaadamu.....wasiuone utukufu wa Mungu
Tamaa ya kupata mali na anasa za ulimwengu huu uliojaa dhiki....vimewafanya wanadamu kuwa vipofu na kutokuona thamani ya uhai......
Leo hii mwanadamu anathamisha uhai wa mtu na fedha......hata wanasahau wanasahu kuwa yeye hapa duniani kama msafiri ambaye amepumzika kwenye kivuli huku safari ikiwa bado inaendelea.....
 
Nadhani hapa kuna kesi pia mauwaji inatakiwa kufunguliwa,inawezekana kabisa hao haoa matapeli wanahusika na kifo cha mume wa huyu mama,ili wapate njia rahisi na kufuta ushahidi wa malipo ya yule jamaa,
sijaona nyerere hapo amehusika upande gani?
 
hapana siye ila ni mtoto wa Butiku, ndo wapigaji wa Mjin hao, wanaish kwa majina ya mading zao

katika rekodi zangu mzee butiku hana mtoto mwenye hilo jina ila najua yupo stela aliyepo ulaya, marehemu mbeza, kuna mwingine wa kiume alijiua kwa kuruka ghorofani mwaka 1989 na sangu ambaye yupo hapa hapa dar akihangaika kutafuta kazi katika makampuni ya sheria na amejishikiza kimtindo katika law firm moja mkabala na habib bank. tuache kuwa wazushi tuliopitiliza.
 
Na mm nachojiuliza makongoro nyerere cjui aliingiaje humo. Huyo papaa alisemekana kuhusika na mauaji, cjui kama justice iko hapa kiukweli.

Huyu mzee ni rafiki kipenzi wa Msofe; mzee wa DILI ZA MJINI.
 
Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, imetoa hukumu kwa mfanyabiashara Marijani Abubakar, almaarufu Papaa Msofe, Alex Massawe na Makongoro Nyerere kwa kosa la kughushi hati ya umiliki wa nyumba iliyopo Mikocheni jijini Dar, mali ya marehemu Onesphory Kituly aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi mwaka 2011.

Kesi hiyo iliyounguruma kwa takribani miaka saba tangu 2007, ilifikia tamati Desemba 22, mwaka huu na kuwakuta na hatia washtakiwa hao baada ya upande wa utetezi kushindwa kuwasilisha vielelezo vinavyowapa uhalali wa kumiliki nyumba hiyo.

Akisoma hukumu hiyo, jaji wa mahakama hiyo, John Nchimbi mbele ya wakili wa Msofe na wenzake, Majura Maghafu alisema kuwa baada ya kupitia hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili, mahakama imeamua kumtangaza mke wa marehemu Onesphory, Mary Kituly kuwa mmiliki halali wa nyumba hiyo.

“Pia mahakama imewatoza fani ya shilingi milioni 300, Papaa Msofe, Massawe na Nyerere pamoja na asilimia 12 ya fedha hizo kama fidia ya gharama za uendeshwaji wa kesi hiyo,” alisema Jaji Nchimbi.

Mara baada ya kusomwa hukumu hiyo, mke wa marehemu, Mary aliangua kilio cha furaha na nduguze mbele ya jaji baada ya kuona haki imetendeka, kitu ambacho hakuwa akikitarajia.

“Yaani siamini macho yangu, maana jinsi kesi ilivyonisumbua kwa miaka saba, nimefarijika sana kwa haki kutendeka maana nilikuwa nikishindana na watu wenye pesa, damu ya mume wangu haijapotea bure, namshukuru Mungu kwa kweli,” alisema Mary alipokuwa akizungumza na waandishi ambapo alimshukuru pia Rais John Magufuli kwani serikali yake inajali haki.

Msofe na wenzake walifunguliwa kesi katika mahakama hiyo mwaka 2007 baada ya kudaiwa kughushi hati ya nyumba kwa kuhamisha umiliki wa nyumba namba 288 iliyopo Mikocheni, Dar iliyokuwa ya marehemu Kituly na kuweka jina lake kisha kumuuzia Masawe kinyume cha sheria.

Ilidaiwa kuwa kabla ya kufariki dunia, marehemu Kituly alimkopa shilingi milioni 30 Msofe kwa dhamana ya hati ya nyumba hiyo kwa makubaliano ya kumrudishia kiasi hicho kwa muda wa miezi sita.

Inadaiwa kuwa baada ya miezi mitano, marehemu alipata kiasi hicho cha fedha na kurudisha kwa Msofe na kutaka hati yake, lakini alianza kuzungushwa kuanzia kipindi hicho hadi alipokufa kwa kuuawa na watu wasiojulikana mwaka 2011.

Oktoba 30, 2007, Msofe aliwatoa kwa nguvu marehemu, mke wake na watoto kwa madai kuwa nyumba hiyo imeuzwa kwa Massawe.

Wenye utaalamu wanifundishe kitu, damu ya mmewe ina uhusiano gani na kushinda kesi hiyo? Je aliamua kuimwaga ili ashinde kesi? Au aliamua kuimwaga ili akishinda kesi yeye amilikishwe nyumba hiyo? Hapo bolded red msaada tafadhali.
 
Duh afadhali nimejikuta nafurahi pamoja na mjane Mungu amjalie mema,Mungu amfute macho ya kumpoteza Mume.Walau Mahakama zetu zimeanza kurejesha imani baada ya kutekwa na matajiri kwa muda mrefu.

Hili kundi la Papa Msofe yafaa liangamizwe haraka,tabia za kuishi mjini kwa kuunga unga zimepitwa na wakati.
 
Back
Top Bottom