JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
Picha ya Maktaba, Rais Vladimir Putin (kulia) alipokutana na Papa Francis, Vatican mnamo Julai 4, 2019.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amesema kuwa aliomba kukutana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin ili kumshawishi kumaliza vita dhidi ya Ukraine lakini hajapata majibu.
Papa Francis wakati vita ikiwa na wiki tatu tangu kuanza Februari 2022 alituma maombi hayo kwa lengo la kutafuta amani lakini hajajibiwa na bado nia yake hiyo ipo.
“Nahisi Putin hatakubali kuwa na mkutano wenye lengo hilo, lakini anaweza kutuma watu wake tukazungumza,” – Papa.
Source: Reuters