Panya road azinduka akiwa Mortuary

Panya road azinduka akiwa Mortuary

inamaana walipofikishwa hospital hakuna daktar aliethibitisha kama kwel wamekufa?au walipelekwa moja kwa moja motuary??
 
Malezi,Malezi,Malezi
Unajua tunaweza kulaumu saana,lakini chanzo cha watoto na makundi ni malezi.
Wazazi wengi hasa wa Jiji la Dar hawana muda wa kukaa na kufuatilia watoto zao.Kila mmoja akitoka anatoka na vyake.

Kwa upande wa Dini na Imani Yangu:
Vijana wengi kwenye matukio kamahayo ni vijana wa Kiislam.
Na hii inaonyesha hata wazazi wao Dini hakuna,ni waislam Jina tu.
Kwa age hiyo ni kwamba mtoto hatokuwa na muda wa kushiriki makundi.Maana akitoka Shule anaungaisha Madrassa jioni,baada ya hapo kuna Darsa la Jioni au anaenda kupumzika na muda mfupi wa kukaa na wenzie ambao wenye mwenenndo mwema.

Wewe mtoto wa Kiislam wa age hiyo anakuambia anaenda kuangalia Singeli?na mzazi kabisaa unaridhika.Na mbaya zaidi,wazazi wengi wamekuwa wakifadhiliwa na hawa watoto,yaani mtoto akifanya ishu,anampa mzazi chochote na mzazi anaona rahaa.
Na zaidi,wazazi wengi wa Dar wanaona mtoto akiweza kujitegemea na kupunguza budget ya nyumbani ndio mjanja na mwema kwao.

Kama mtoto wako ni mhalifu basi wa kwanza kujua ni mzazi,ila mapuuza ndio hatma yake inakuwa hivyo.

Sote tunawatoto na Mungu awanusuru watoto wetu,na awaongoze na kuwaongoa hao watoto wameopotea au wanaotaka kupotea na pia Mungu atupe nguvu na msaada kama wazazi tuweze kuwasimamia watoto wetu.

Naamini kabisa kwamba katika kundi hilo,kuna watoto wana vipaji vikubwa sana either uelewa kishule au Kitaaluma,lakini wa kuweza kujua namna ya awali ya kumsaidia mtoto yoyote ni Mzazi mwenyewe na sio vinginevyo.
 
Madaktari wa dar bhana eti wamemruhusu kutoka mortuary ingekuwa tarime wangemlazimisha kubaki mortuary au sio mikuria katili
Madaktari wa dar bhana eti wamemruhusu kutoka mortuary ingekuwa tarime wangemlazimisha kubaki mortuary au sio mikuria katili
Madaktari wa dar bhana eti wamemruhusu kutoka mortuary ingekuwa tarime wangemlazimisha kubaki mortuary au sio mikuria katili
Madaktari wa dar bhana eti wamemruhusu kutoka mortuary ingekuwa tarime wangemlazimisha kubaki mortuary au sio mikuria katili
Mkuu umenichekesha sana :-D:-D:-D
 
malezi ya watoto si kazi ndogo ati..msiozaa subirini mkizaa mtoto akishabalehe uone mziki wake..!
 
waafrica wengi tunafia kwenye mochwari baada ya kufia wodini inashangaza sana mtu eti anatoka mochwari kupelekwa wodini baada ya kutoka wodini kwenda mochwari
Only in Tanzania. Ma Dokta wa mwendokasi
 
Yaani HAWA watoto siyo wa kuwahitumia kabisa. Poor parental care, wazazi wamekuwa busy kuhangaika na maisha wanasahau malezi ya watoto. Aisee wajiandae kupambana na jamii na matokeo wameshayaona.
 
Kwahyo kumbe temeke hosp hawajampima kuthibisha kama amekufa kweli wao walivyoambiwa tu na hao walompeleka na wao wakamsweka ubaridini hahaaa
 
Pole sana kwa waalimu kwa malezi ya watoto wa siku hizi. Mungu ahusike tu kwa hakika.
 
Mtoto akifanya uhalifu halafu hukumu akapewa mzazi ni kitendo kitakachochea uhalifu miongoni mwa watoto. Naamini sheria ya kuwabana watoto ipo.

Wazazi wawajibishwe kwa kutowatimizia mahitaji watoto wao (ikithibitika mzazi/mlezi alimtelekeza mtoto kwa makusudi) lkn mtoto pia achukuliwe sheria kwa uhalifu aliofanya.

Watoto hao wakiachwa na hukumu kuelekezwa kwa wazazi, yataibuka makundi ya watoto watakaofanya uhalifu maana wanajua wazazi wao watabeba huku yao(watoto)

Watoto wengine watafanya uhalifu ili kuwakomoa wazazi/walezi wao inapotokea hawapatani.

Sheria ifuate mkondo wake kwa watoto na wazazi ikithibitika kuwa wana hatia.
 
Back
Top Bottom