Panya Mtanzania atunikiwa nishani ya Dhahabu kwa umahiri wake wa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini

Mkuu we wadhani utani, yani serikali ya awamu ya tano ina kila aina ya mbinu. Imeona raia zinazingua kwenye kutuwakilisha, ikatuma panya na sasa nishani ya dhahabu hiyo. Yani lazima kieleweke soon tutatembea kifua mbele.
Tunaelekea uchumi wa Kati
 
Panya Mkubwa wa kiume kutoka Tanzania anayeitwa Magawa ametunikiwa nishani ya Dhahabu kutokana na Uwezo wake wa kubaini mabomu ya kutegwa Ardhini Cambodia, Magawa alizaliwa Tanzania Nov 5, 2014 akiwa na Uzani wa kilo 1.2 na urefu wa Sentimita 70 na Amelelewa pia Tanzania.

Magawa amenusa mabomu 30 na siraha 28 ambazo hazijalipuka katika maisha yake, Shirika la Matibabu ya Wanyama la Uingereza lisilokuwa la kiserikali PDSA limempa medali ya Dhahabu kwa kuokoa maisha kupitia kazi yake ya kubaini mabomu hatari yaliyotegwa ardhini Cambodia.

Panya huyo alipewa mafunzo na Shirika lisilo la kiserikali la Apopo kutoka Ubelgiji lenye Makao yake Makuu Tanzania ambalo linawalea Panya Shujaa kugundua uwepo wa mabomu ya kutegwa Ardhini tangu miaka ya 1990, kwa Wanyama 30 waliopewa tuzo hiyo, huyu ni panya wa Kwanza.

Haya 'Mafanikio' ya huyu Panya 'Magawa' hayawezi kutumiwa tu kama sehemu ya 'Ushindi' wa Miaka Mitano iliyopita na ijayo ya Chama fulani hivi?
 
Hadi panya ananishinda!!! Hii si aibu hii!.. ntaweka wapi sura yangu mimi komamanga la watu!.. panya tayari ananishani ya dhahabu wakati hapa hata nishani ya uji Sina!!

Kweli maisha ni fumbo..
 
wabongo sio mchezo na insta account wameshangulia.
Screenshot_20200925-222123_Instagram.jpg


Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom