SUA: Panya wanaweza kutumika kubaini Corona na kupunguza gharama na maumivu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Baada ya mafanikkio makubwa ya utafiti wa matumizi ya Panya kwenye kutambua mabomu na vimelea vya kifua kikuu na mambo mengine, Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo SUA wanasema kuna uwezekano mkubwa wa Panya hao kutumika kwenye kutambua maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.

Hayo yamebainishwa kwenye banda la SUA na Mtafiti mwandamizi na Meneja Mradi wa Utafiti wa Panya wa SUA-APOPO Dkt. Georgies Mgode kwenye Maonesho ya Ubunifu na mashindano ya Kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU 2021) Jijini Dodoma.

“Tunaamini Panya wanaweza kutambua virusi vya Corona na Maambukizi yake kwa ufanisi mkubwa maana tumeshaona mafanikio kwenye Utambuzi wa ugonjwa wa kifua kikuu, kwani kila kimelea kina harufu yake na kila ugonjwa unaosababishwa na vimelea tofauti una harufu yake kwahiyo tunaamini Panya wanaweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa sana”. Alibainisha Dkt. Mgode.

Amesema tayari wameshaandika maandiko ya kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza kazi ya kufundisha Panya hao na zikipatikana wataanza lakini wanaamini watasaidia hasa kutambua wale watu ambao wana vimelea lakini dalili hazijajitokeza maana ukiweza kutambua ugonjwa kabla dalili hazijajitokeza ni rahisi kuzuia maambukizi kwa haraka zaidi.

“ Hii itakuwa na manufaa makubwa maana vipimo vya Corona kwa sasa ni ghari sana na vinatoka nje ya nchi lakini kwa kutumia Panya itakuwa rahisi na pia itaondoa maumivu makubwa kwa watu wanaopimwa wakati wa kuchukua sampuli ukilinganisha na vifaa vinavyotumiwa sasa kwenye kupima wahisiwa wa wagonjwa wa COVID-19” Alisisitiza Mtafiti huyo Mwandamizi Dkt. Mgode.

Aidha Dkt. Mgode ameeleza kuwa kitendo cha kutambua maambukizi ya awali kabisa kwa watu wenye vimelea ni jambo muhimu kwani litasaidia watu kujilinda lakini pia wale watakaokutwa na vimelea watapatiwa huduma mapema na hivyo kupunguza vifo na kusambaa kwa ugonjwa.

Amesema kuna wanasayansi wengi huko nchi zilizoendelea baada ya kuona mafanikio makubwa ambayo Panya wamefikia walifanya majaribio ya kutumia Pua bandia (electronic Nose) kunusa ili kutambua vimelea lakini hawajafanikiwa kama ambavyo SUA wamefanikiwa kwa kumtumia Panya mwenyewe hivyo wataendelea na Panya kutokana na uwezo wake mkubwa katika kutambua.

Dkt. Mgode ameishukuru Serikali kwa kupitisha matumizi ya teknolojia ya Panya kwenye hospitali zake na kwa makubaliano kuwa majibu Panya yathibitishwe na teknolojia zingine zilizopitishwa kabla ya majibu kutumia hospitalini na imekuwa ikifanyika hivyo na kusaidia watu wengi kubainika na kupona baada ya kupatiwa matibabu akitolea mfano mwaka jana 2020 jumla ya wagonjwa 2014 ambao hawakugundulika kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu kwa kutumia njia za kawaida za hospitali za vipimo walibainika kwa kutumia Panyabuku.

Dkt. Mgode amesema wanashawishika sasa zaidi baada ya kuona kuwa baadhi ya wale ambao wanashuku matumizi ya Panya kwenye kutambua vimelea vya TB sasa wameanza kujadili namna ya kutumia Mbwa katika kufanya kazi hiyo wakati vyote vinatumia mfumo huohuo katika kutambua.

“Tunaamini kabisa kuwa matokeo bora yanayopatikana hapa Tanzania yataweza kusaidia kushawishi na kubadili mitazamo hasi ya baadhi ya mataifa na wanasayansi wengine ambao hawaamini kwenye matumizi ya Panya na hasa ukizingatia kuwa nchi yetu ya Tanzania inaongoza kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu (TB). Alifafanua Dkt. Mgode.

Mtafiti huyo amesema kwa sasa tusiangalie ni silaha ipi iliyotumika katika kupata matokeao ya ushindi na ugonjwa utakapotokomea ndipo wengine wataamini kuwa mbinu na teknolojia gani inafanya kazi vizuri.

Mradi wa SUA – APOPO unaofanya tafiti za Panya ulio katika kituo cha Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibifu ulianza na utafiti wa Panya kwenye kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini na ukawa na mafanikio makubwa kwa kuwatumia kwenye nchi mbalimbali duniani hasa za Msumbiji, Angola na Kambodia. Kutambua vimelea vya kifua kikuu, Kutambua utoroshaji wa nyara za Serikali kama pembe za Ndovu na faru pamoja na magamba ya kakakuona,Utoroshaji wa Miti ya mbao ngumu ambayo ipo hatarini kutoweka kwa magendo mipakani.
 
“Tunaamini Panya wanaweza kutambua virusi vya Corona na Maambukizi yake kwa ufanisi mkubwa maana tumeshaona mafanikio kwenye Utambuzi wa ugonjwa wa kifua kikuu, kwani kila kimelea kina harufu yake na kila ugonjwa unaosababishwa na vimelea tofauti una harufu yake kwahiyo tunaamini Panya wanaweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa sana”. Alibainisha Dkt. Mgode.
Hao panya wamekuwa wa hadithi zaidi kuliko matokeo, mbona hatuwaoni wakitumika kwenye maabara mahospitalini badala yake serikali inaagiza tu kemikali za kupimia hayo magonjwa miaka nenda rudi, fugeni panya lakini tuone matunda yake badala ya hadithi kila kukicha.
 
Impact ya SUA kwenye uchumi wa Taifa letu ni ndogo sana. Wenzetu wanazungumzie masuala ya Rocket science SUA wapo kwenye utafiti wa panya.
Kenya is still on course to build its first nuclear power plant facility in the next 12-15 years, a senior Energy Ministry official said on Friday.

Joseph Njoroge, principal secretary for electricity, told Reuters the East African nation plans to turn to nuclear when it has fully exploited other sources of energy.

“It (nuclear plant construction) may be in the next 12 or even 15 years … the Kenya Nuclear Electricity Board is still a going concern and only working to prepare for nuclear,” he said.

Hydropower accounts for 35 per cent of Kenya’s electricity generation, with the rest coming from geothermal, wind and heavy oil plants, the ministry says.

Plans to develop a 1,050-megawatt coal-fired plant on the coast, using funding from China, have been delayed by court action from environmental activists.

The development of nuclear energy will come after other resources have been fully exploited in line with growing demand for energy, Njoroge said.

“That is after we have done a lot of exploitation of the geothermal, the coal that we also want to exploit, the wind, solar and all those,” he said.

“At that time the only option we will have to get clean energy will be from nuclear.” (Reuters/NAN)
 
Ni suala jema,
Angalizo;
Sayansi isiingiliwe na Siasa,
Wanasiasa wakae mbali na hili!
 
Ni suala jema,
Angalizo;
Sayansi isiingiliwe na Siasa,
Wanasiasa wakae mbali na hili!
Ni Nani alikuambia wanasiasa wanahitaji sayansi ya panya Karne ya 21? Itachangia ajira kiasi gani? Nimemkumbuka Joseph Musukuma kauli yake kuhusu maProfesa
 
Impact ya SUA kwenye uchumi wa Taifa letu ni ndogo sana. Wenzetu wanazungumzie masuala ya Rocket science SUA wapo kwenye utafiti wa panya.
SUA wamefanya sehemu yako kutokana na nature yake, wengine wafanye pia sehemu yao kwa nature yao. Michango hiyo ndio italeta impact kubwa kiuchumi ikiwa kila mmoja ataplay role yake.

COSTECH nadhani wanahitaji msukumo wa kina kwenye kuhakikisha sayansi inachangia uchumi wa nchi!!!
 
Hata kwenye soko la ajira graduates wa SUA wana changamoto kubwa sana kupata ajira wengine wanachunga mbuzi na elimu wanayo.
 
Kenya is still on course to build its first nuclear power plant facility in the next 12-15 years, a senior Energy Ministry official said on Friday.

Joseph Njoroge, principal secretary for electricity, told Reuters the East African nation plans to turn to nuclear when it has fully exploited other sources of energy.

“It (nuclear plant construction) may be in the next 12 or even 15 years … the Kenya Nuclear Electricity Board is still a going concern and only working to prepare for nuclear,” he said.

Hydropower accounts for 35 per cent of Kenya’s electricity generation, with the rest coming from geothermal, wind and heavy oil plants, the ministry says.

Plans to develop a 1,050-megawatt coal-fired plant on the coast, using funding from China, have been delayed by court action from environmental activists.

The development of nuclear energy will come after other resources have been fully exploited in line with growing demand for energy, Njoroge said.

“That is after we have done a lot of exploitation of the geothermal, the coal that we also want to exploit, the wind, solar and all those,” he said.

“At that time the only option we will have to get clean energy will be from nuclear.” (Reuters/NAN)
We jamaa inaonekana ni mjuaji na mshamba.
SUA ni chuo kinacho husika na mambo kama hayo asa sijui ulitarajia waje na nini?
 
Ko ulitaka chuo cha kilimo kije na Nini kama sio hayo?
Binadamu sijui tupoje yaani.
Kuna haja ya kufanyika kwa tadhimini ya tafiti na degrees programs zinazotolewa SUA. Zingine zinahitajika kufutwa zimepotea na wakati haswa kwenye mfuko wa ajira .
 
Nao hawa wametuchosha na mapanya wao ,miaka na miaka ni wao na mapanya sijui yameleta tija gani hadi sasa
 
Back
Top Bottom