Panya Asababisha Safari ya Ndege Iahirishwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Panya Asababisha Safari ya Ndege Iahirishwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 4, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,913
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Abiria 205 wa ndege ya Air Canada waliokuwa wasafiri kutoka Kanada kuelekea Uingereza walilazimika kulala hotelini baada ya safari yao ya ndege ilipoahirishwa baada ya panya kugundulika kwenye ndege dakika chache kabla ya ndege kupaa. Panya mkubwa aliyeonekana akirandaranda kwenye ndege dakika chache kabla ya ndege kupaa alisababisha abiria wote 205 waahirishiwe safari zao.

  Ndege ya Air Canada aina ya Boeing 767, ilikuwa ikijiandaa kupaa kuelekea London, Uingereza toka Kanada wakati mmoja wa abiria alipomuona panya kwenye sehemu ya juu ya kuwekea mizigo ndani ya ndege.

  Rubani wa ndege hiyo aliwaamuru abiria wote 205 washuke kwenye ndege ili wataalamu wa wanyama waingie kumkamata panya huyo.

  Lakini pamoja na msako mkali uliofanyika panya huyo hakupatikana. Safari ya ndege hiyo iliahirishwa na abiria walilazimika kulala kwenye hoteli iliyopo karibu na uwanja wa ndege wa Macdonald-Cartier international airport wa mjini Ottawa.

  Tukio hili linawakumbusha watu tukio la mwezi wa nne mwaka jana nchini Australia ambapo ndege ya abria iliyokuwa angani ililazimika kutua kwa dharura baada ya nyoka wanne aina ya chatu walipofanikiwa kuchoropoka toka kwenye sehemu ya mzigo waliyohifadhiwa na kusababisha kizaazaa kwenye ndege
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...