Panya anapodhaniwa ni Simba

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,913
30,255
"THE SAND PEBBLES": MCHINA KULI DHALILI ALIDHANI MMAREKA NI MBABE NI SIMBA KUMBE PANYA

''The Sand Pebbles,'' ni senema kati ya senema ninazozipenda hadi leo kwani ndani yake alikuwa Steve McQueen na Richard Attenborough waigizaji wakubwa wakati wa utoto wangu.

Senama hii ilikuja Dar es Salaam mwaka wa 1966.

Nakumbuka kuona tangazo la hii movie ndani ya Tanganyika Standard.

Siku zile senema ilikuwa burudani kubwa sana na magazeti yakitangaza michezo itakayokuwa katika theatres zote

Katika filamu hii kuna stori ndani ya meli ya kivita (Gun Boat) ya Kimarekani, ''San Pablo.''

Kulikuwa katika ''Engine Room,'' kijana wa Kichina akitazamwa dharau kama kuli tu na kijana wa Kimarekani ambae yeye alijihisi kuwa ni bora kama Mmarekani.

Mchina alikuwa ''cheap labour,'' mtu wa kutumwa kusafisha viatu, kupika na kufua nguo ndani ya meli hiyo.

Ubaguzi dhidi ya huyu kijana na Wachina wengine ulikuwa mkubwa sana wakiwaona Wachina kama vile si binadamu.

Siku moja yule kijana wa Kimarekani akampiga yule Mchina kwa kuwa alimkuta anakunywa kahawa kwenye kikombe ambacho Wamarekani walikuwa wanakitumia.

Hali ndani ya chombo kile na uadui ambao yule Mmarekani alikuwa akimfanyia yule Mchina ulifikia mahali njia nzuri ya kumaliza sintofahamu ile ilikuwa kutayarisha pigano la ngumi (boxing) katika ya yule kijana wa Kichina kuli na huyu ofisa Mmarekani.

Wamarekani walichukulia ile kuwa burudani watamuona Mchina atakavyoashibiwa kwa makonde mazito ya yule Mmarekani ndugu yao.

Ukiwatazama hawa watu wawili Mmarekani pandikizi la jitu na yule Mchina mfupi na katawaliwa na uoga wa kumwogopa yule Mmarekani kisaikolojia tu ilikuwa wazi kuwa Mchina atatandikwa vibaya sana.

Hili halikutokea.

Mchina alianza kupigana kwanza kwa kumuogopa Mmarekani lakini jinsi duru zilivokuwa zinakwenda Mchina alitambua kuwa yule Mmarekani jitu kubwa na majigambo na kiburi chake chote hakuwa simba anaeunguruma kama alivyomdhania.

Yule Mmrekani alikuwa panya.

Hana ujasiri wala nguvu yoyote ya kuhimili kipigo chake.

Yule Mmarekani aliyekuwa akimuonea, kumtisha na kumtukana kila siku ndani ya Engine Room kwa hakika alikuwa panya.

Mmarekani alipigwa vibaya sana.
 
Back
Top Bottom