SoC02 Pande mbili za Tanzania yetu

Stories of Change - 2022 Competition

GoJeVa

Member
Sep 15, 2021
41
59
PANDE MBILI ZA TANZANIA YETU.

SEHEMU YA KWANZA: TANZANIA YETU KATIKA MAANDISHI NA PICHA.
SEHEMU YA PILI: WANANCHI NA UFUKARA, WATAWALA NA UKWASI.

TANZANIA YETU KATIKA MAANDISHI NA PICHA.


NC1.jpg


Chanzo cha picha: mtandaoni.(hawa ni vijana wa kitanzania waliovalia kiasili).

Tanzania ni nchi inayopatika barani afrika upande wa mashariki, nchi hii imetokea baada ya nchi mbili kuungana nchi hizo zilizoungana ni Tanganyika na Zanzibari. Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 na Zanzibari ilipata uhuru mwaka 1964. Mwaka 1964 tarehe 26 mwezi wa nne nchi hizi mbili ziliungana na kuwa nchi moja iitwayo Tanzania. Katika sehemu hii ya kwanza, tutaingalia nchi yetu ya Tanzania katika maeneo tofauti touti kwa maandishi na picha, SONGA NAMI;

1. Lugha

Nchini Tanzania lugha inayotumika kama lugha ya taifa ni Kiswahili. Lugha hii pia ndio utambulisho mkubwa wa watanzania, Kiswahili pia hutumika katika shule na ngazi mbalimbali za elimu kama somo na pia lugha ya mawasiliano katika baadhi ya mazingira. Licha ya lugha hiyo nchini Tanzania pia kuna lugha zingine za makabila mbalimbali kama vile kinyakyusa, kihehe, kingoni, kimatengo na nyinginezo nyingi.

2.Maliasili na utalii
Ndani ya nchi hii pendwa ya Tanzania kuna maliasili nyingi sana kama vile kuna madini, misitu, milima mikubwa, fukwe za kuvutia na mbuga mbalimbali za wanyama. Maliasili kama hizo, huifanya nchi yetu iwe kivutio kikubwa cha utalii.

NC1.jpg


Chanzo cha picha: mtandaoni.(hawa ni simba wakiwa katika mbuga ya wanyama Serengeti nchini Tanzania).

NC1.jpg


Chanzo cha picha: mtandaoni (Hili ni bonge ya almasi lililowai kuchimbwa katika mgodi wa Williamson kule Mwadui nchini Tanzania.)

3.Utamaduni na Michezo
Katika nchi yetu, tunajishughulisha na michezo na tamaduni mbalimbali kwa kujiburudisha na kama ajira. Michezo hiyo ni kama vile, mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa kikapu, na baadhi ya tamaduni ni kama vile; ngoma za asili mfano mnanda, mdundiko.

NC1.jpg


Chanzo cha picha: mtandaoni(Huyu ni Mbwana Samatta, mtanzania anayechezea club ya mpira wa miguu K.R.C Genk huko nchini Ubeligiji).

4. Siasa na utawala
Tanziania ni nchi yenye mfumo wa vyama vingi kikatiba. Chama tawala katika nchi yetu ni CCM(Chama Cha Mapinduzi), na raisi wa nchi anaitwa Samia Suluhu Hassan.

NC1.jpg

Chanza cha picha: mtandaoni(Huyu ni raisi wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.)

5. Eimu
Mfumo wa elimu nchini Tanzani unaanzia ngazi ya chekechea, elimu ya msingi, elimu ya sekondari na elimu ya chuo. Elimu ya msingi mwanafunzi anapitia madarasa saba, ambayo darasa la kwanza hadi darasa la saba. Elimu ya sekondari ina madarasa sita ambayo ni kidato cha kwanza hadi kidato cha sita na upande wa elimu ya chuo hapo imegawanyika mara mbili yaani kuna vyuo vikuu na vyuo vya kati.

NC1.jpg


Chanzo cha picha; mtandaoni(hii ni picha ya maktaba iliyopo ndani ya chuo kikuu cha Dar es salaam).

6. Uchumi na maendeleo.
Tanzania ni nchi inayoendelea. Kutokana na kuwa ni nchi inayoendelea hivyo kuna changamoto mbalimbali kama vile; changamoto za nishati kama vile ukosefu wa umeme baadhi ya nyakati, upungufu wa shule na vituo vya afya bora. Pia, kuna changamoto za miundo mbinu mfano; baadhi ya bara bara, reli na viwanja vya ndege kutokuwa na ubora unaohitajika.

7. Shughuli za uzalishaji mali(kilimo,uvuvi na ufugaji).
Watanzania wengi hujishughulisha na kazi mbalimbali kama vile, kilimo,uvuvi,ufugaji na nyinginezo. Asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima wadogo wadogo(peasants).

WANANCHI NA UFUKARA, WATAWALA NA UKWASI.
UTANGULIZI.
Ufukara ni umasikini uliopindukia. Katika nchi zetu nyingi hasa hizi za dunia ya tatu ufukara umekuwa ni tatizo kubwa, wananchi wanaishi kwenye lindi la umasikini. Cha kushangaza nchi hizi nyingi ambazo wananchi wake wanateseka na hali ngumu za maisha zimebarikiwa rasilimali nyingi kama vile madini mfano; Almasi,dhahabu, Rubi, makaa ya mawe, Tanzanite, pia nchi hizo zina vivutio vingi vya utalii mfano; mbuga za wanyama, sehemu za fukwe za kuvutia na milima.

nc1.png


Chanzo cha picha: mtandaoni(hii ni moja ya kaya masikini).

Ukwasi ni hali ya mtu kuwa na mali nyingi sana, kwa msamiati mwepesi ukwasi ni utajiri. Katika nchi hizi zinazoendelea ikiwemo Tanzania viongozi wengi wa serikali kama vile wabunge, mawaziri, maraisi, viongozi wa vyama vya siasa ndio wanaokumbatia ukwasi kwa kiasi kikubwa. Cha kujiuliza je hawa viongozi wanapata wapi huo ukwasi, wakati nchi zao ni masikini na wananchi wao kwa kiasi kikubwa wamejaa ukata.

nc1.jpg

Chanzo cha picha: mtandaoni(hii ni picha inayoonesha bajeti inayotumika, upande wa magari kwa ajili ya watawala).

Raisi wa sasa wa Zambia Hakainde Hichilema katika hotuba yake nchini kwake alihoji pia, kwa nini gari aina ya VX zinanunuliwa kwa kodi za wananchi na kupewa viongozi wakati wananchi wanakosa huduma za jamii. Pia, alishauri kwa kusema kama hao viongozi wanapenda magari ya kifahari basi wajinunulie wenyewe na sio kunyonya wananchi ilihali wanapokea mishahara mikubwa na posho kedekede.

nc1.jpg


Chanzo cha picha: mtandaoni(hiyo ni picha inayoonesha kauli ya raisi wa Zambia kuhusu magari ya kifahari aina ya VX).

Hivyo sasa ni wakati sahihi wa viongozi wetu wa nchi kujitafakari, juu ya ugumu wa maisha kwa wananchi wao. Kwa sasa nchini Tanzania kuna mjadala mkubwa wa ongezeko la Tozo, Kodi na bei ya bidhaa kuwa juu kwa wananchi. Ukiangalia upande wa pili viongozi bado wanaishi maisha ya anasa na mazuri ukilinganisha na wananchi wao.

Baadhi ya gharama za maisha zinazo umiza wananchi nchini Tanzania na zilalamikiwazo ni kama vile;

1. Ongezeko la tozo kwenye mihamala ya simu na kwenye mabenki.

2. Bei ya bidhaa kuwa juu, kama vile bei ya mafuta ya kula, bei ya mafuta ya petrol, bei ya sukari pia na bidhaa zingine ambazo itachukua kurasa nyingi kama zitaandikwa zote.

Ni vizuri viongozi wajue wapo kwenye nafasi walizopo kutokana na wananchi, hivyo ni jambo jema kutumikia wananchi na kuwasikiliza na si vinginevyo.

RASILIMALI ZETU ZITUNUFAISHE.

AHSANTENI.
 
Back
Top Bottom