Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 36,986
- 45,897
Panama papers, lundo la makaratasi iliyosheheni data za makampuni ya watu wakubwa kwenye serikali duniani wafanyabiashara na wengine maarufu , imetoa picha ya unafiki wa viwango vya juu vya nchi za magharibi.
Miaka yote nchi za mnagharibi zimekua zikishutumu nchi maskini kua zijengwe katika misingi ya uwazi na uajibikaji, na haukuchelea kuzichukulia hatua kali nchi hizo kwa kukiuka masharti wanayowapa. Mfano mzuri ni ule wa Tanzania kwa kunyimwa fedha za MCC.
Ukifuatilia sakata hili la nyaraka za Panama utakutana na orodha za watu ambao walikua na makampuni makubwa yanayofanya shughuli zake huko panama wakikwepa kodi kubwa kwa mabilioni ya madola toka nchi zao za asili. Moja ya wahusika ni Baba Yake mzazi Waziri Mkuu wa sasa wa Uingereza Bw. Cameroon ambaye huyu mzee alikua na kampuni kubwa na hakuwahi lipa kodi hata senti.
Washirika wa Rais wa Urusi, mawaziri wakuu nao wanahusika. Hii ni njia ya kuona ni kwa namna gani hawa watu walivyo wanafiki wa viwango vya juu.
Inakuwaje kuzikandamiza nchi ndogo maskini kama Tanzania while wao ndio wanaoongoza kwa Rushwa na kukwepa kulipa kodi?
Ndio maana napata tabu sana kuona mtu akishabikia hata kwa lepe maamuzi ya hawa watu kwa nchi maskini.