Pamoja na yote nampenda mume wangu

Pamoja na yote nampenda mume wangu

Ni ngumu kumeza lakini huo ndo uhalisia wa ndoa,upendo hufunika wingi wa dhambi.

Pasaka hii nilimtembelea mama yangu mdogo kwa kweli nilifurahia sana maisha yake na mumewe ikabidi nimuulize anipe siri ya urembo.

Basi akaniambia mwanangu usione leo naishi kama malkia mamayako nilisota sana,usione hivi baba yako anavyonipenda sana na kunithamin usifikiri ilikuja hvihvi nilifanya kitu kikapindua moyo wake.

Akaniambia mume wake alikuwa mlevi sana na kila siku alikuwa anampiga sana na kumfukuza,yeye alikuwa akilia na Mungu tu,basi siku moja akamwambia nimekupiga vya kutosha naomba uondoke tu kwa amani beba chochote unachokipenda hata kama ni vyote ww beba tu,akamwambia leo nisikukute tafadhal nitakuua.

Basi siku hiyo mumewe alirud amelewa chakar hata hajitambui kabisa aliletwa na watu,basi mamamdogo akaita tax akampakia huyo na bag lake had kwao,bahati nzuri wazazi wa mwanamke walikuwa wanaishi mkoa huohuo.

Alifika kwao usiku sana alipofika akambwaga mumewe sebulen wakalala,kulipokucha mumewe akaamka saa 3 asubuh akastuka anaona mazingira magen kwake kushoto mamamkwe kulia babamkwe pemben yake mke wake,

kwa aibu akauliza hapa wapi?mke wake akamjibu hapa ni kwetu,jana wakati unaenda kazin uliniambia nibebe chochote nikipendacho na niondoke kwako,na mimi nakupenda wewe ndo maana nikakubeba,wewe ndo kitu cha thaman sana kwangu.

Basi mume wake aliona aibu sana na akamuomba mkewe msamaha tena kwa machozi na goti juu,kuanzia siku ile ikawa ni mwisho wa pombe,kuanzia siku ile furaha yake ya ndoa ikarud upya tena mara dufu,kwa kweli anavyopendwa na kuthaminiwa na muwewe sijui nifananishe na nin.

Kwako dada davina usikate tamaa endelea kumuomba Mungu,muombee mumeo,usimuombee mabaya,ipo siku Mungu atasikia kilio chako,kumbuka tu wema hauozi.
 
Last edited by a moderator:
Habari za masiku mengi
Naamini mko wazima tunaendelea salama na ujenzi wa Taifa
Kama nilivyowahi kuandika mikasa yangu hapa pamoja na mume wangu kunitenda sana pamoja na kunisaliti sana pamoja na mabaya yake yote ukweli ni kuwa nafurahia kuwa nae,nafurahia kuwa baba wa mtoto wangu,najivunia kumfahamu,sikati tamaa,sirudi nyuma,simuachi huyu ndiye Mume Mungu aliyenipa!
Ni ngumu kumchukia mtu uliyewahi kumpenda kweli, ila ishi nae kwa akili maradhi yapo, Muombe sana Mungu amuondolee moyo wa kukuumiza.
 
Ni ngumu kumeza lakini huo ndo uhalisia wa ndoa,upendo hufunika wingi wa dhambi.

Pasaka hii nilimtembelea mama yangu mdogo kwa kweli nilifurahia sana maisha yake na mumewe ikabidi nimuulize anipe siri ya urembo.

Basi akaniambia mwanangu usione leo naishi kama malkia mamayako nilisota sana,usione hivi baba yako anavyonipenda sana na kunithamin usifikiri ilikuja hvihvi nilifanya kitu kikapindua moyo wake.

Akaniambia mume wake alikuwa mlevi sana na kila siku alikuwa anampiga sana na kumfukuza,yeye alikuwa akilia na Mungu tu,basi siku moja akamwambia nimekupiga vya kutosha naomba uondoke tu kwa amani beba chochote unachokipenda hata kama ni vyote ww beba tu,akamwambia leo nisikukute tafadhal nitakuua.

Basi siku hiyo mumewe alirud amelewa chakar hata hajitambui kabisa aliletwa na watu,basi mamamdogo akaita tax akampakia huyo na bag lake had kwao,bahati nzuri wazazi wa mwanamke walikuwa wanaishi mkoa huohuo.

Alifika kwao usiku sana alipofika akambwaga mumewe sebulen wakalala,kulipokucha mumewe akaamka saa 3 asubuh akastuka anaona mazingira magen kwake kushoto mamamkwe kulia babamkwe pemben yake mke wake,

kwa aibu akauliza hapa wapi?mke wake akamjibu hapa ni kwetu,jana wakati unaenda kazin uliniambia nibebe chochote nikipendacho na niondoke kwako,na mimi nakupenda wewe ndo maana nikakubeba,wewe ndo kitu cha thaman sana kwangu.

Basi mume wake aliona aibu sana na akamuomba mkewe msamaha tena kwa machozi na goti juu,kuanzia siku ile ikawa ni mwisho wa pombe,kuanzia siku ile furaha yake ya ndoa ikarud upya tena mara dufu,kwa kweli anavyopendwa na kuthaminiwa na muwewe sijui nifananishe na nin.

Kwako dada davina usikate tamaa endelea kumuomba Mungu,muombee mumeo,usimuombee mabaya,ipo siku Mungu atasikia kilio chako,kumbuka tu wema hauozi.

Mimempenda bure huyo mama yako mdogo. Ila mimi siwezi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom