Pamoja na umaarufu alio nao Alikiba kwa nini Bado Maskini na Diamond platnumz ni mwanamuziki tajiri?

Kijana kukaa chini kudiscuss maisha ya vijana wenzio ambao huwafikii kwa lolote ni dalili ya kukata tamaa.....
songa mbele kijana bado muda unao au kama vipi jiunge na mimi huku kwenye ukonda wa daladala mbona na sie tuna zichanga tu hizo chenjiiii..... usikate tamaaa bro.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Habari zenu wana jf

Naombeni uzii huu usichukuliwe kiushabiki bali uchukuliwe kama haki ya kila mtu kutoa ya moyoni pasipo kuvunja sheria

Kwa mda mrefu msanii Alikiba amekuwa yupo kwenye game la mziki na amejizolea umaarufu mkubwa kwa kazi zake nzuri na kujipatia mashabiki wengi huku wengine wakimuita "KING" wa bongofleva.

Lakini pamoja na umaarufu wake alionao na mashabiki wengi aliojizolea lakini bado Alikiba ni mtu mwenye maisha ya ya chini tu ambayo hayafanani kabisa na umaarufu wake

Tukija upande wa pili wa mwanamuziki Naseeb Abdul ~Diamond Platnumz yeye si wazamani sana kwenye game kama alikiba lakini nayeye ametokea kufanya kazi nzuri na kujizolea mashabiki wengi na umaarufu lakini hajaweza kufikia record ya The king himself Alikiba

Lakini ukija kwenye maswala ya maendeleo ambayo ndio kipimo cha kazi anayofanya msanii utagundua kuwa Diamond platnumz amejizolea utajiri wa kutisha zaidi ya King himself Alikiba.

Kutokana na kazi ya mziki Diamond platnumz ameweza kujipatia utajiri mkubwa ikiwemo kuachia mijengo mingi ya maana hapa town na mengine South Africa. Diamond amefunguka zaidi kwa kuanzisha biashara zake za Chibu perfume na Diamond karanga ambazo zinafanya vizuri nzuri sokoni bila kusahau mikataba yake ya matangazo na makampuni makubwa wakati king Kiba hana biashara ya maana wala maendeleo yoyote kumzidi Naseeb
1b6a914765dee10191206877f27f3872.jpg

baf5eac734a10fe7a1c795f1258ae853.jpg

b78bdcea38f9fd2b03a2e54e403d5d2b.jpg

dd124671bdcf3d7cdf0e1120c15cafce.jpg


Diamond platnumz amejenga ofisi yake ya kisasa na kufungua studio yake ya wasafi records ambayo inahusika kutengeneza ngoma zote za wasafi na wasanii wengine kutoka nnje kitu ambacho Alikiba hadi leo hana ofisi wala studio yake binafsi
9b5bab3186e9b0ab5b1ec5a21fbd0ab0.jpg

5aba10ffde33e51db20eafe3807c4f89.jpg

a5eefc9f96dbbd47fefa3f02627c4c3f.jpg

0b191687eb9d1141279775010bc4e08f.jpg


Diamond ameanzisha Label yake mwenyewe ya Wasafi records ambayo inawasimamia wasanii wakali kama Rich mavoko,Harmonize,Rayvanny,lavalava na mtandao wa wasafi.com ambao anauza nyimbo zake na za wasanii wengine online. Label ya wasafi imekuwa ni chanzo kikubwa cha kupiga mkwanja mrefu kwa Diamond platnumz hadi ilifika kipindi TRA wakamkadiria kodi hadi swala hilo likatinga bungeni

Huku Diamond platnumz ni msanii pekee anaeilipa kodi kubwa serikali kuliko msanii yeyote hapa tz, Akiwapiku wasanii wengi wakongwe na wapya ambao wamekuwa wakimchukia lakini wengi wao hata mlango wa TRA hawaujui nikimaanisha wanaendesha kazi zao kiujanja ujanja lakini Diamond platnumz ameonyesha mfano kwa kuilipa kodi serikali kwa kazi zake zote
81226d28e38578c6244eb8ea6449258c.jpg


Wakati upande wa pili wa Alikiba yeye bado amesainiwa na Sony music na hana label yake mwenyewe wala wasanii anaowasimamia,Na wala sina uhakika kama anailipa kodi serikali kama anavyofanya Platnumz

Diamond platnumz ameweza kutoa ajira kwa
~Mameneja 2
~Madancer 5
~producer 1
~Bodyguard 1
~Photographer 1
~Mtu wa IT 1
~Mbunifu 1
~Muhasibu 1
~wasanii chini ya label yake 5
Jumla 19

eab9b5e89f9bc0fee68573deed497799.jpg

Ukipiga hesabu hapo Diamond platnumz anaspend zaidi ya 100 millions kwa ajili ya kulipa mishahara tu kwa crew yake au wafanyakazi wa label yake ya wasafi kwa kila mwezi huku mshahara mkubwa ukienda kwa wasanii walio chini ya lebel yake kulingana na mikataba yao

Ukija upande wa pili wa alikiba yeye ni mwajiriwa tu wa sonny music hamlipi mtu mshahara lakini maisha yake hayafanani kabisa na misifa anayopewa na mashabiki wake Mwisho wa siku utagundua kuwa alikiba anaambulia sifa tu kutoka kwa mashabiki zake mitandaoni kakini Diamond ni real money maker nikimaanisha mashabiki wanaompaka sifa Alikiba mchana ndio hao hao Wanaomtajirisha Diamond platnumz wenyewe

Na wapo watakaokuja kusema hapa kuwa alikiba sio mtu wa show off lakini msema ukweli ni mpenzi wa mungu pesa na maisha aliyokuwa nayo Alikiba hata aizidishe mara 10 hamfikii Diamond platnumz japo watu hao hao wanampaka mafuta mwa mgongo wa chupa alikiba kwa sifa ndio hao hao wanaomtajirisha Platnumz

mziki duniani kote sasa hivi ni pesa ndio mpango mzima lakini najiuliza mziki wa alikiba ni wa kuingiza pesa kutokana na kazi nzuri au ni mziki wa sifa mbona hana maendeleo yoyote?

*~Mtotmtamu
Kwanza kabisa maendeleo ya kiuchumi si kipimo cha uzuri wa sanaa ya msanii.

Sanaa haipimwi kwa hela.

Naona unaoanisha maendeleo ya kiuchumi ya msanii na uzuri wa sanaa yake.

Msanii anaweza kuwa mzuri zaidi katika sanaa yake lakini hajui kusimamia haki zake na hivyo akawa na mikataba mibaya itakayomfanya awe masikini.

Na msanii mwingine anaweza kuwa si mzuri sana katika sanaa, lakini akawa anajua kusimamia haki zake katika mikataba na hivyo kuwa tajiri.

Kwa hiyo umelinganisha uchumi na sanaa katika namna ambayo haina ulinganifu.

Sent from my Kimulimuli
 
Nani Kakuambia Diamond Karanga Ni Za Domo?? Huyo Domo Kapewa Kazi Ya Kupromote Soko Tu Kumbuka Hizo Karanga Zilikuwepo Toka Mwaka Juzi Na Zilikuwa Za Rangi Ya Blue
Sasa ww ndo umesema hivo lakini hao wenye kampuni mbona hawasemi karanga ni zao ila matangazo kapewa diamond mbona ni kawaida kupewa tangazo...hiyo kampuni wanaficha nn? Na ww umejuaje? Karanga kuwepo sokoni kwa kipindi kilichopita haina maan mikataba ya uzalishaji na umilikishi kubadilika....lazma uwe na fact na point za kutosha hiyo sio sabab ya msngi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfalme wa bongo fleva ni dully sykes,nyie madogo mlioanza kufuatilia muziki juzi ndo mnadanganywa eti ali ni king,pili muziki ili ukulipe lazima uwe na akili ya biashara na menejimenti nzuri kitu ambacho mwenzetu hana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kabisa maendeleo ya kiuchumi si kipimo cha uzuri wa sanaa ya msanii.

Sanaa haipimwi kwa hela.

Naona unaoanisha maendeleo ya kiuchumi ya msanii na uzuri wa sanaa yake.

Msanii anaweza kuwa mzuribzaidi katika sanaa yake lakini hajui kusimamia haki zake na hivyo akawa na mikataba mibaya itakayomfanya awe masikini.

Na msanii mwingine anaweza kuwa si mzuri sana katika sanaa, lakini akawa anajua kusimamia haki zake katika mikataba na hivyo kuwa tajiri.

Kwa hiyo umelinganisha uchumi na sanaa katika namna ambayo haina ulinganifu.

Sent from my Kimulimuli
Kama unatoa kazi nzuri alafu uchumi wako ni mbovu ni heri uache sanaa tu masna utakuwa unafanya kazi kujaza maji kwenye chujio
 
JAMANI TUWE TUNAONGEA TUKIWA TUMESHA FANYA RESEARCH NDUGU ZANGU MIMI NAISHI JIRANI NA ALI KIBA JAMANI KWANZA AFU PIA JAMAA ANA MANSION MOMBASA NA ANAISHI SAAANA HUKO NA UINGEREZA AMBAPO WATOTO WAKE WAWILI NDIO WANAISHI HUKO AMAYA NA YULE MDOGO JAMANI NIMECHEKA SAAAANA
Acha uwongo mombasa kaishi lini? Mpaka tiket ya Msa anatumiwa na joho, amekaa kipindi hiki cha Kampeni tu, hapo ndio ujue mwanamuziki wako alivyo mdogo, kaenda mombasa mwezi mzima anamfanyia Kampeni Gavana wa msa, Hivi Diamond wangeweza kumlipa pesa ya mwezi mzima?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa uzi rekebisha kauli sio kweli kwamba alikiba kamzidi umaarufu diamond,.....hakuna msanii maarufu zaidi wa tz kama domo...tukija hata kwene mashabiki nadhan domo anao wengi zaidi hasa nje ya mipaka ukizingatia alikiba hajaweka mizizi sana nje ya Africa ila anamashabiki zaidi tz na nairobi kenya..,.......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkubali mkatae, Ali Kiba hana utajiri wa kumzidi Diamond na wala hamfikii ata thumuni. Diamond ana vitega uchumi vingi kama nyumba maeneo mbali mbali ya mji, endorsments na muziki wake mwenyewe ulivyo mkubwa.

Ali kiba anapambanishwa nae tu kwa chuki binafsi maana nae anajitutumua tu na watu wanampa bichwa ila ni wazi hawezi kumpiku diamond kimaisha na hata kimuziki kwa sasa.

Ishu ya utajiri hata hainaga haja ya makelele kwa maana umbea tu wa wabongo ungetosha ku reveal ukweli.Ushahidi wa matukio unatosha kudhihirisha hilo.
Alikiba anapambanishwa na Diamond????au Diamond anapambana na Kiba??????
Ok basi sawa wanapambanishwa lkn kumbuka ni katika muziki siyo maisha binafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ali masikini kwa kigezo kipi?

Kwann heading umemtaja Ali maelezo yote ni ya Diamond?

Kwann umeonyesha mali anazomiliki Diamond na za Ali hujaonyesha?

Naomba kujua umefikiri kwa kutumia Akili au Hisia?
bora umeona nilichokiona japo kwa kuchelewa.
 
Kama unatoa kazi nzuri alafu uchumi wako ni mbovu ni heri uache sanaa tu masna utakuwa unafanya kazi kujaza maji kwenye chujio
Ushawahi kusikia msemo "art for the sake of art" ?

Huo msimamo wako ni wa kiuchumi zaidi, na haubadili ukweli kwamba msanii mzuri anaweza kufa masikini wakati asiye mzuri akatajirika.

Kwa hiyo tunapopima sanaa, kupima kwa mafanikio ya kiuchumi ni kigezo potofu.

Msanii anaweza kutajirika kwa kuuza unga chinichini.Sisemi Diamind anafanya hivyo, nasema ukitumia uchumi kama kigezo, unaweza kusifia sanaa kwa sababu mtu kauza unga.



Sent from my Kimulimuli
 
Haya mambo Ndiyo Yale yale ya kushow off , huyo kiba kauza sana wimbo wake wa aje mwaka Jana kwenye mitandao na hasa audio, kaingiza pesa nzur mkataba wake na sonny , show zake za nje ulaya na marekani, juz juzi tu kapiga pesa ndefu sana huko kenya kwenye kampeni za akina odinga hasa Mombasa ( gavana joho )

Ukija kwenye video ( account za VEVO msaan kule analipwa kwa view zake ) ishu hapa ni mmoja anapenda kujionesha na mwingine ni kimya kimya hata kiba ana jumba lake la maana lipo pale tabata sema ni vile tu haongei , kampuni ya Rockstar ni yake sasa wanauza nyimbo na ishu zote za entertainment Africa lakin hujawahi kusikia akijisifu hata siku moja

Mfano mzuri wasaani wenye pesa ndefu afu wapo simple tu

Yupo A.y huyu ana pesa ( na ndiyo mtu wa kwanza kumtengenezea connection mond na akina davido ) huyu anamilik kipind cha mikasi na ana project zingine lakin huoni akijisifu hata siku moja

Mwisho niseme wote ni vijana na ni wapambanaji ila kila mtu na makuzi yake na tabia yake ya matumiz ya pesa

Wengine kwetu ni somo kuwa upate pesa upige kelele na show off au ukae kimya tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nikweli ila ujue kwa uhalisia tukizungumzia swala la pesa kwene mitandao diamond ndio anaongoza na ndo maan youtube walitoa top ten yao diamond alimpiku mbali sana kiba,....na jarbu kuangalia nyimbo zao zote utaona ni nani ana views wengi zaidi utagundua ni diamond,...dili za matangazo diamond ana matangazo mengi na makubwa zaidi ya Alikiba,......tukija kwene show nadhani hapa hamna ubishi hata tusilizungumzie maan uyo domo uko nje kapiga show nyingi sana na Africa nzima kwa ujumla kulinganisha na alikiba...ukicheki kwa jicho la mbali sehemu anazopita kiba ni zile diamond kashazipitia mara mbili yake uko nyuma.....lifestyle ya kujionyesha na kutojionesha ni mtu mwenyewe....lakini tukiwafananisha zaidi kwa kazi zao kimziki hivo havifichiki maan yuotube kila mtu anaona,matangazo tunaona,shows tunaona na tuzo zinaonekana

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom