Kitabu cha Yona 1:1ff kinaelezea Juu ya Yonah ambaye alipoona amekataa kwenda kule alikoitwa aende alipand chombo kingine kuelekea mji wa Tarshish, Mungu alipoona amekaidi alisababisha dhoruba kali katika kile chombo na abiria na mabaharia walishindwa kujua ni kwa nini chombo kimeyumba vile. Ilibidi awajulishe sababu ni yeye kusababisha chombo kuyumba na akaamua kujihukumu mwenyewe akawaomba wamtose baharini. Alipotoswa baharini chombo kilitulia na yeye akamezwa na samaki mkubwa akapelekwa kule kule ambako Mungu alikusudia aende. Alitubu na kazi ya Mungu ikaendelea.
Katika kutafakari kinachoendelea ndani ya CHADEMA na familia kubwa ya UKAWA, Naanza kushawishika kwamba kama kweli jamaa alishiriki kwenye mchakato na kuridhia ujio wa Edward Lowasa ndani ya CHADEMA ili apeperushe bendera ya CHADEMA ili kufikia hatma ya UKOMBOZI, Nawaomba MAKAMANDA kama mnavyo jiita endeleeni na Mikakati kama mlivyojipangia wakati na Katibu Mkuu alivyoshiriki. Ninajua ni ngumu kuikubali hali na mazingira haya mapya lakini hakuna namna ya kufanya MABADILIKO lazima yaje na mkakati lazima utekelezwe. Iko siku tutaujua ukweli lazima mipango iendelee.
Makosa hutokea katika medani za kivita, hata nyumba ya jirani wamejikuta katika makosa makubwa kwa kukata Jina la Kamanda wao EDWARD LOWASSA. Songeni mbele maana kilichotokea ni ajali kazini.