Pamoja na ujio wa Lowassa CHADEMA, Dr. Slaa ni chaguo sahihi kugombea Urais

Niko mitaa ya DSM tukijaribu kufatilia tukio la lowasa kurudisha fomu leo tumekutana na changamoto kutoka katika makundi ya raia mbalimbali wakisema na kuhoji kwa kwasasa hawataki kusikia habari ya DR Magufuli,LOwasa,CCM na Chadema bali wanachotaka ni kusikia Dr Slaa wao upo wapi, anafanya nini na nini tamko lake katika mchakato wa uchaguzi huu
 
Nimelazimika kuandika hili baada ya kusoma post fulani ya mwanasiasa mmoja maarufu sana katika siasa za nchi hii na sasa nimeanza kuamini yanayoandikwa kwenye magazeti kumuhusu yeye.

Kosa kubwa la mh.Lowassa ni kushindwa kujiuzulu baada ya kutakiwa kutovunja mkataba na kusubiri shinikizo la Bunge.Hili ndio naweza kusema ni kosa kubwa alilolifanya mh.Lowassa lakini kosa hili linavumilika na halimzui kuendelea na ambitions zake za kisiasa.

Kuna huyu mh. anaonekana kususa kisa ni ujio wa Lowassa ndani ya CHADEMA.Mimi naomba kumuuliza bila kumtaja jina hapa.

Je,yeye anaetuhumiwa kujikopesha hela za chama alikuwa sahihi na je hilo halikuwa kosa la kibinadamu kama la Lowassa?

Sometimes huwa najiuliza kama kweli lengo la upinzani ni kushika dola au ni kufanya siasa tu kama ajira?

Hivi ni mwanasiasa gani mwenye kiu ya kweli ya kutaka mabadiliko asieona "potential" ya Lowassa katika kuiondoa CCM madarakani?!

Upinzani nchi hii jambo gumu kama "jabali"!

Mods tendeni haki msiunganishe wala kuondoa huu uzi na isitoshe sijataja jina la muhusika hapa.
 
Dah! Naona mmeanza kutengeneza makundi .... Na hii itawafanya mpokee kipigo kikali. Kuondoka kwa Lowasa CCM kumewafanya kuwa kitu kimoja. Narudia tena kauli yangu, nitawapigia kura Wapinzani lkn wawe ktk umoja wao, vinginevyo nikithibitisha kuwa haya ya kuvurugana ni kweli October 25 nitabaki home.
 
Kitabu cha Yona 1:1ff kinaelezea Juu ya Yonah ambaye alipoona amekataa kwenda kule alikoitwa aende alipand chombo kingine kuelekea mji wa Tarshish, Mungu alipoona amekaidi alisababisha dhoruba kali katika kile chombo na abiria na mabaharia walishindwa kujua ni kwa nini chombo kimeyumba vile. Ilibidi awajulishe sababu ni yeye kusababisha chombo kuyumba na akaamua kujihukumu mwenyewe akawaomba wamtose baharini. Alipotoswa baharini chombo kilitulia na yeye akamezwa na samaki mkubwa akapelekwa kule kule ambako Mungu alikusudia aende. Alitubu na kazi ya Mungu ikaendelea.

Katika kutafakari kinachoendelea ndani ya CHADEMA na familia kubwa ya UKAWA, Naanza kushawishika kwamba kama kweli jamaa alishiriki kwenye mchakato na kuridhia ujio wa Edward Lowasa ndani ya CHADEMA ili apeperushe bendera ya CHADEMA ili kufikia hatma ya UKOMBOZI, Nawaomba MAKAMANDA kama mnavyo jiita endeleeni na Mikakati kama mlivyojipangia wakati na Katibu Mkuu alivyoshiriki. Ninajua ni ngumu kuikubali hali na mazingira haya mapya lakini hakuna namna ya kufanya MABADILIKO lazima yaje na mkakati lazima utekelezwe. Iko siku tutaujua ukweli lazima mipango iendelee.

Makosa hutokea katika medani za kivita, hata nyumba ya jirani wamejikuta katika makosa makubwa kwa kukata Jina la Kamanda wao EDWARD LOWASSA. Songeni mbele maana kilichotokea ni ajali kazini.
 
Sijajua Kama umaarufu wa watu ni kusema watu, na Sijui Kama tuwasema wakajirekebisha na kuungana nasi tunapaswa kuwakimbia? Kama lengo ni kufanya siasa tu Kama ajira na Kama kumsema mtu ndiyo sera akifa tutasema nini? Kama kweli dr. Slaa kamkimbia Lowasaa basi kwake siasa ni kuendelea kuwasema wenye makosa? Maana kama mtu uliyekuwa unamsema kwa ubaya ni Muda mwafaka kujifunza kwake. Na je tunataka kusema Lowasaa asifanye siasa kabisa kwamba yeye ndiye mchafu kuliko wanasiasa wote?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom