Pamoja na ujio wa Lowassa CHADEMA, Dr. Slaa ni chaguo sahihi kugombea Urais

Johnson Mbwambo

WAKATI naandika makala hii, habari zilikuwa zimezagaa ya kuwa Umoja wa Vyama vya Upinzani nchini (Ukawa), na hasa Chadema walikuwa wamekubaliana kumpokea Edward Lowassa na kumfanya kuwa mgombea urais wao kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba. Nathubutu kueleza wazi kwamba hilo ni kosa ambalo watalijutia kwa miaka mingi.

Sijui nini kilikuwa kinaendelea katika vichwa vya viongozi wa Ukawa wakati wakifanya maamuzi ya mwisho ya kumpokea Edward Lowassa na hata kumfikiria kuwa ndiye anayestahili kupeperusha bendera yao kumkabili Dk. John Magufuli wa chama tawala, CCM, kwenye patashika ya Oktoba ya kuwania kukamata dola.

Najua ya kwamba ‘siasa ni mchezo mchafu', lakini bado najiuliza maswali kibao kichwani mwangu ya ni hoja zipi Chadema ilizizingatia katika kumkubali Lowassa – mtu ambaye chama hicho kilimuorodhesha katika ile orodha ya Mwembe Yanga ya watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini – List of shame (orodha ya aibu).

Chadema haikupata kumuondoa Lowassa katika orodha hiyo. Na ndiyo sababu wengi wetu tumepigwa na butwaa kwa hatua yake ya ghafla ya kumkubali mtu huyo kuwa anakifaa chama hicho kubeba bendera yao ya kuwania urais.

Je, ni kwa sababu labda ana maono (vision) ya namna ya kuikomboa nchi hii au ni kwa sababu tu ya mapesa yake? Au tuseme ni kwa sababu ya ‘umaarufu' wake? Au labda ni kwa sababu ya uwezo wake kiutendaji? Au ni kwa sababu ya marafiki zake matajiri atakaohama nao? Vyovyote vile, umma unawadai viongozi wa Chadema na Ukawa majibu ya maswali haya.

Hivi Chadema (achilia mbali CUF) inawezaje kusimama jukwaani na kumnadi urais (au hata kuwa naye tu jukwaani) mtu ambaye yumo katika orodha yao ya mafisadi papa nchini? Wataanzia wapi na wataficha wapi nyuso zao? Au labda ni kwa kuwa IQ ya Watanzania ni ya kiwango cha chini, na ndiyo maana wanaamini watasahau ya jana kuhusu mgombea urais huyo?

Hivi nani asiyejua ya kuwa Lowassa anahamia Chadema si kwa sababu ya kukipenda chama hicho na sera zake, lakini ni kwa sababu ya kuikomoa CCM iliyomtosa? Hivi kweli mtu anayeingia chama kulipa visasi au kukikomoa chama chake cha zamani anaweza kuwa na faida yoyote kubwa na endelevu kwa chama hicho alichohamia na kwa Watanzania kwa ujumla? Tangu lini visasi binafsi na kukomoana vikachukua nafasi ya mustakabali wa taifa?

Vyovyote vile, Chadema na Ukawa yao itabidi, kwenye kampeni ya urais waanze kwanza na kumsafisha Lowassa (sijui kwa sabuni gani) ndipo waeleze sera zao kwa wapiga kuwa. Itabidi kwanza wazifute hadharani kauli zote za nyuma ambazo ziko kwenye kumbukumbu walizozitamka dhidi ya Lowassa kumhusisha na ufisadi, na ndipo waanze kumnadi au hata kuhalalisha tu kuwa naye kwenye jukwaa wakati wa kampeni.

Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, alipata kusema ya kuwa mtu akishakuwa tu na tuhuma kubwa za ufisadi hafai kufikiriwa urais, na naamini ni kwa hoja hiyo hiyo CCM iliamua kumtosa Lowassa hata bila ya kufikisha jina lake kwenye vikao vya juu kabisa vya maamuzi – Kamati Kuu, NEC na Mkutano Mkuu.

Sasa, ni ‘maajabu' kwamba Chadema, badala ya kujisifu kwamba, kimechangia kuifanya CCM imtose urais mtu aliyekuwa kwenye orodha yao ya ‘list of shame', ndicho hicho kinachompokea kwa mbwembwe – yaani mtu yule yule kiliyempiga vita kuwa ni fisadi!!! Jamani, ni kwa sababu ya mapesa yake tu au ni kwa sababu ya maslahi binafsi na si maslahi mapana ya chama na Watanzania?

Nimedadisidadisi ni vipi Chadema na Ukawa walikubali kumpokea mtu ambaye chama tawala CCM kilimtosa kwa sababu ya tuhuma za ufisadi - mtu ambaye Chadema kilishiriki kueneza habari nchini nzima kuwa ni fisadi. Jibu nililopewa na ninalopewa ni kwamba eti Lowassa ni ‘mwathirika' tu wa mfumo (system) wa kifisadi wa Serikali ya CCM. Eti sasa wanadai ya kuwa Lowassa ni msafi ila mfumo wa kifisadi ndiyo tatizo kuu linalopaswa kupigiwa kelele! Mbona haya hawakutueleza tangu mwanzo? Au ndo wameyajua baada ya yeye kutoswa na CCM?

Lakini hapa kuna swali jingine. Huo mfumo (mimi nauita mtandao) uliwekwa na unaendeshwa na kina nani? Si kweli kwamba nyuma ya mfumo huo kuna watu na Lowassa, kama mmoja wa watu walioshika nafasi za juu za uongozi nchini, ni sehemu ya mfumo huo? Kweli Watanzania tumepoteza uwezo wa kufikiri (we have gone crazy)!

Ndugu zangu, nasisitiza tena ya kwamba Chadema na Ukawa wamefanya kosa ambalo watalijutia.

Nadiriki kusema ya kuwa kama kweli watamsimamisha Lowassa kuwa mgombea urais wao, basi wameshindwa uchaguzi wa Oktoba hata kabla hawajaingia kwenye kampeni zenyewe. Kama wamesahau, waulize kilichomkumba Augustine Mrema kwenye uchaguzi wa mwaka 1995 baada ya kutoka CCM akiwa na huo unaoitwa ‘umaarufu' ambao leo tunaaminishwa Lowassa anao hivi sasa nchini!

Binafsi, sioni namna yoyote ambayo Rais Kikwete na CCM yake ataukabidhi urais kwa Lowassa Novemba mwaka huu. Ninachokiona ni kwamba sasa Kikwete na CCM yake watafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha Lowassa hakamati Ikulu. CCM watapindua kila jiwe kuhakikisha Lowassa hawi rais wa nchi hata kama atasimama kwa tiketi ya Ukawa. Kama mnabisha, subirini Oktoba muone matokeo!

Kwa mtazamo wangu, niliamini, na bado naamini ya kuwa ‘The Chosen One' kutoka Ukawa alistahili kuwa Dk. Slaa wa Chadema. Takwimu za uchaguzi wa mwisho wa mwaka 2010 zinaonyesha ya kwamba walijiandikisha wapiga kura 20,137,303 lakini waliopiga kura ni 8,626,283. Kati ya kura hizo zilizopigwa Rais Kikwete alipata kura 5,276,827, Dk. Slaa kura 2,271,941 na Lipumba kura 695,667.

Kwa takwimu hizo, na kwa kigezo cha lojiki, Slaa anampiku Lipumba kwa mbali. Ingawa katika siasa kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla chama husika hakijateua mgombea urais wake, lakini utahitaji maelezo ya kuridhisha kumtosa mtu ambaye uchaguzi uliopita alipata kura 2,271,941 na badala yake kumteua mtu ambaye aliambulia kura 695,667 tu.

Kwa hiyo, kwangu mimi, uteuzi wa Dk. Slaa ungekuwa ni uteuzi sahihi awepo Lowassa au kwenye Upinzani au asiwepo.

Kiupambanaji, Dk. Slaa ni zaidi ya Lowassa. Ana ujasiri. Kumbukumbu zinaonyesha kwamba damu yake na ya mkewe Josephine (sijui kama wameshaoana) iliwahi kumwagika akipambana na dola kuwatetea wanyonge.

Aidha, ni mwadilifu, mweledi, ana busara, na hana maamuzi ya jazba kama Lowassa (rejea skandali ya Richmond) au Magufuli.Katika kipindi cha miaka 15 iliyopita, Dk. Slaa amewaongoza Watanzania (wakiwemo wabunge) kubadilisha kabisa mwelekeo wa uwajibikaji wa watawala wetu Tanzania. Aidha, amehangaika huku na kule nchini kuwaamsha wapiga kura usingizini ili wawatathmini watawala wao (siwaiti viongozi) wakiwa na upeo mkubwa wa ufahamu.

Ninadiriki kusema kuwa hata kufungwa jela kwa hivi karibuni kwa mawaziri wawili wa zamani – Daniel Yona na Basil Mramba, ni matunda ya kazi ya muda mrefu ya kupambana na ufisadi ya Dk. Slaa na wenzake kadhaa pamoja na vyombo vya habari.

Tofauti na wagombea urais wengine ambao wangeweza kuteuliwa kutoka Upinzani – Lowassa, Lipumba, Mbowe nk, Dk. Slaa yeye anaingia katika kinyang'anyiro hicho akiwa na rekodi safi ya nyuma ya utendaji jimboni na hata alipokuwa ndani ya Bunge. Hadi leo rekodi hiyo haijapata kuchafuliwa na kashfa yoyote ya ufisadi au nyingine yoyote kubwa.

Kama, mpaka sasa, Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inaendelea kuwa mfano wa kuigwa nchini wa halmashauri zinazochacharika kuwaletea wananchi wake maendeleo makubwa, ni kwa sababu ya msingi mkubwa wa Dk. Willbroad Slaa aliouweka akiwa mbunge wa jimbo hilo.

Ndugu zangu, kama bunge sasa linachangamka na linasimama kidete kupambana na ufisadi nchini (mfano Escrow), ni kwa sababu huko nyuma kulikuwa na kina Slaa ndani ya bunge hilo waliojitolea "kufa kidogo" kutetea wanyonge na ambao walionyesha ujasiri wa kutoiogopa serikali kwa kuibana kweli kweli. Hawa wa sasa wanafuata tu njia iliyoanzishwa na hao waliowatangulia – yaani Dk. Slaa na wenzake.

Ndugu zangu, nihitimishe kwa kusisitiza mambo mawili. La kwanza ni kwamba Dk. Slaa ndiye aliyestahili kuwa chaguo sahihi la kumkabili Dk. Magufuli, na si Lowassa, Lipumba, Mbowe au Mbatia. La pili ni kwamba kwa kumkubali Lowassa kuwa mmojawao, Chadema na Ukawa ‘wameipoteza' kabisa agenda ya ufisadi. Itabidi sasa wafunge midomo yao kuzungumzia vita ya ufisadi, kwa sababu sasa Watanzania wanaamini kuwa walikuwa wakibwabwaja tu maneno lakini si waumin wa kweli wa vita hiyo!

Niambieni; ni wapi ambako kuna ushahidi kuwa Lowassa alipata kukubali "kufa kidogo" kuwatetea wanyonge na masikini wa nchi hii. Ni mjinga tu ndiye asiyejua kwamba Lowassa ndiye chaguo la urais la mabilionea wa Tanzania ambao wengi wao mapesa yao hawakuyapata kihalali.

Hakuna namna yoyote ambayo Lowassa anaweza kudai kuwa katika patashika zake za kuusaka urais anawakilisha maslahi ya masikini waliozagaa vijijini! Tiketi yake ni ya mabilionea wenzake na ndiyo atakaowawakilisha kwenye kampeni. Mtu wa namna hiyo akiingia Ikulu, kamwe hawezi kuwakumbuka masikini wala wanyonge bali atawakumbuka mabilionea wenzake waliomwingiza Ikulu.

Rejeeni ile hafla yake ya Arusha ya kutangaza nia ya kuwania urais ilivyokuwa ya mapesa mengi ndo utaelewa ninachomaanisha ninaposema ya kuwa si mwakilishi wa masikini na wanyonge. Na ndiyo maana, kwangu mimi, bado nitaendelea kuamini ya kuwa The Chosen One kutoka Upinzani wa kumkabili Dk. Magufuli alistahili kuwa Dk. Slaa.

Ni bora CCM, ambayo sasa inaanza kujirudi na kujisafisha kwa kuwatosa watuhumiwa wa ufisadi miongoni mwao kuliko Chadema na Ukawa ambao sasa wanapokea makapi ya CCM yanayokimbia tuhuma za ufisadi. Lowassa, kama alivyokuwa mzigo kwa CCM, atakuwa tu mzigo kwa Chadema na Ukawa yao! Time will tell! Tafakari.

Raia Mwema
Toleo la 416
29 Jul 2015-
 
Hivi kweli umeacha kufanya shughuli zako ukakaa muda wote huo kuandika huu UTUMBO WA MBWAA..!! Kweli ww jin lako la ubatizo ulitakiwa uitwe IDIOT au labda una ugonjw wa Idiotizimaizationalisim kwenye Medulla yako...!!!
 
Johnson Mbwambo

WAKATI naandika makala hii, habari zilikuwa zimezagaa ya kuwa Umoja wa Vyama vya Upinzani nchini (Ukawa), na hasa Chadema walikuwa wamekubaliana kumpokea Edward Lowassa na kumfanya kuwa mgombea urais wao kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba. Nathubutu kueleza wazi kwamba hilo ni kosa ambalo watalijutia kwa miaka mingi.

Sijui nini kilikuwa kinaendelea katika vichwa vya viongozi wa Ukawa wakati wakifanya maamuzi ya mwisho ya kumpokea Edward Lowassa na hata kumfikiria kuwa ndiye anayestahili kupeperusha bendera yao kumkabili Dk. John Magufuli wa chama tawala, CCM, kwenye patashika ya Oktoba ya kuwania kukamata dola.

Najua ya kwamba ‘siasa ni mchezo mchafu’, lakini bado najiuliza maswali kibao kichwani mwangu ya ni hoja zipi Chadema ilizizingatia katika kumkubali Lowassa – mtu ambaye chama hicho kilimuorodhesha katika ile orodha ya Mwembe Yanga ya watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini – List of shame (orodha ya aibu).

Chadema haikupata kumuondoa Lowassa katika orodha hiyo. Na ndiyo sababu wengi wetu tumepigwa na butwaa kwa hatua yake ya ghafla ya kumkubali mtu huyo kuwa anakifaa chama hicho kubeba bendera yao ya kuwania urais.

Je, ni kwa sababu labda ana maono (vision) ya namna ya kuikomboa nchi hii au ni kwa sababu tu ya mapesa yake? Au tuseme ni kwa sababu ya ‘umaarufu’ wake? Au labda ni kwa sababu ya uwezo wake kiutendaji? Au ni kwa sababu ya marafiki zake matajiri atakaohama nao? Vyovyote vile, umma unawadai viongozi wa Chadema na Ukawa majibu ya maswali haya.

Hivi Chadema (achilia mbali CUF) inawezaje kusimama jukwaani na kumnadi urais (au hata kuwa naye tu jukwaani) mtu ambaye yumo katika orodha yao ya mafisadi papa nchini? Wataanzia wapi na wataficha wapi nyuso zao? Au labda ni kwa kuwa IQ ya Watanzania ni ya kiwango cha chini, na ndiyo maana wanaamini watasahau ya jana kuhusu mgombea urais huyo?

Hivi nani asiyejua ya kuwa Lowassa anahamia Chadema si kwa sababu ya kukipenda chama hicho na sera zake, lakini ni kwa sababu ya kuikomoa CCM iliyomtosa? Hivi kweli mtu anayeingia chama kulipa visasi au kukikomoa chama chake cha zamani anaweza kuwa na faida yoyote kubwa na endelevu kwa chama hicho alichohamia na kwa Watanzania kwa ujumla? Tangu lini visasi binafsi na kukomoana vikachukua nafasi ya mustakabali wa taifa?

Vyovyote vile, Chadema na Ukawa yao itabidi, kwenye kampeni ya urais waanze kwanza na kumsafisha Lowassa (sijui kwa sabuni gani) ndipo waeleze sera zao kwa wapiga kuwa. Itabidi kwanza wazifute hadharani kauli zote za nyuma ambazo ziko kwenye kumbukumbu walizozitamka dhidi ya Lowassa kumhusisha na ufisadi, na ndipo waanze kumnadi au hata kuhalalisha tu kuwa naye kwenye jukwaa wakati wa kampeni.

Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, alipata kusema ya kuwa mtu akishakuwa tu na tuhuma kubwa za ufisadi hafai kufikiriwa urais, na naamini ni kwa hoja hiyo hiyo CCM iliamua kumtosa Lowassa hata bila ya kufikisha jina lake kwenye vikao vya juu kabisa vya maamuzi – Kamati Kuu, NEC na Mkutano Mkuu.

Sasa, ni ‘maajabu’ kwamba Chadema, badala ya kujisifu kwamba, kimechangia kuifanya CCM imtose urais mtu aliyekuwa kwenye orodha yao ya ‘list of shame’, ndicho hicho kinachompokea kwa mbwembwe – yaani mtu yule yule kiliyempiga vita kuwa ni fisadi!!! Jamani, ni kwa sababu ya mapesa yake tu au ni kwa sababu ya maslahi binafsi na si maslahi mapana ya chama na Watanzania?

Nimedadisidadisi ni vipi Chadema na Ukawa walikubali kumpokea mtu ambaye chama tawala CCM kilimtosa kwa sababu ya tuhuma za ufisadi - mtu ambaye Chadema kilishiriki kueneza habari nchini nzima kuwa ni fisadi. Jibu nililopewa na ninalopewa ni kwamba eti Lowassa ni ‘mwathirika’ tu wa mfumo (system) wa kifisadi wa Serikali ya CCM. Eti sasa wanadai ya kuwa Lowassa ni msafi ila mfumo wa kifisadi ndiyo tatizo kuu linalopaswa kupigiwa kelele! Mbona haya hawakutueleza tangu mwanzo? Au ndo wameyajua baada ya yeye kutoswa na CCM?

Lakini hapa kuna swali jingine. Huo mfumo (mimi nauita mtandao) uliwekwa na unaendeshwa na kina nani? Si kweli kwamba nyuma ya mfumo huo kuna watu na Lowassa, kama mmoja wa watu walioshika nafasi za juu za uongozi nchini, ni sehemu ya mfumo huo? Kweli Watanzania tumepoteza uwezo wa kufikiri (we have gone crazy)!

Ndugu zangu, nasisitiza tena ya kwamba Chadema na Ukawa wamefanya kosa ambalo watalijutia.

Nadiriki kusema ya kuwa kama kweli watamsimamisha Lowassa kuwa mgombea urais wao, basi wameshindwa uchaguzi wa Oktoba hata kabla hawajaingia kwenye kampeni zenyewe. Kama wamesahau, waulize kilichomkumba Augustine Mrema kwenye uchaguzi wa mwaka 1995 baada ya kutoka CCM akiwa na huo unaoitwa ‘umaarufu’ ambao leo tunaaminishwa Lowassa anao hivi sasa nchini!

Binafsi, sioni namna yoyote ambayo Rais Kikwete na CCM yake ataukabidhi urais kwa Lowassa Novemba mwaka huu. Ninachokiona ni kwamba sasa Kikwete na CCM yake watafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha Lowassa hakamati Ikulu. CCM watapindua kila jiwe kuhakikisha Lowassa hawi rais wa nchi hata kama atasimama kwa tiketi ya Ukawa. Kama mnabisha, subirini Oktoba muone matokeo!

Kwa mtazamo wangu, niliamini, na bado naamini ya kuwa ‘The Chosen One’ kutoka Ukawa alistahili kuwa Dk. Slaa wa Chadema. Takwimu za uchaguzi wa mwisho wa mwaka 2010 zinaonyesha ya kwamba walijiandikisha wapiga kura 20,137,303 lakini waliopiga kura ni 8,626,283. Kati ya kura hizo zilizopigwa Rais Kikwete alipata kura 5,276,827, Dk. Slaa kura 2,271,941 na Lipumba kura 695,667.

Kwa takwimu hizo, na kwa kigezo cha lojiki, Slaa anampiku Lipumba kwa mbali. Ingawa katika siasa kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla chama husika hakijateua mgombea urais wake, lakini utahitaji maelezo ya kuridhisha kumtosa mtu ambaye uchaguzi uliopita alipata kura 2,271,941 na badala yake kumteua mtu ambaye aliambulia kura 695,667 tu.

Kwa hiyo, kwangu mimi, uteuzi wa Dk. Slaa ungekuwa ni uteuzi sahihi awepo Lowassa au kwenye Upinzani au asiwepo.

Kiupambanaji, Dk. Slaa ni zaidi ya Lowassa. Ana ujasiri. Kumbukumbu zinaonyesha kwamba damu yake na ya mkewe Josephine (sijui kama wameshaoana) iliwahi kumwagika akipambana na dola kuwatetea wanyonge.

Aidha, ni mwadilifu, mweledi, ana busara, na hana maamuzi ya jazba kama Lowassa (rejea skandali ya Richmond) au Magufuli.Katika kipindi cha miaka 15 iliyopita, Dk. Slaa amewaongoza Watanzania (wakiwemo wabunge) kubadilisha kabisa mwelekeo wa uwajibikaji wa watawala wetu Tanzania. Aidha, amehangaika huku na kule nchini kuwaamsha wapiga kura usingizini ili wawatathmini watawala wao (siwaiti viongozi) wakiwa na upeo mkubwa wa ufahamu.

Ninadiriki kusema kuwa hata kufungwa jela kwa hivi karibuni kwa mawaziri wawili wa zamani – Daniel Yona na Basil Mramba, ni matunda ya kazi ya muda mrefu ya kupambana na ufisadi ya Dk. Slaa na wenzake kadhaa pamoja na vyombo vya habari.

Tofauti na wagombea urais wengine ambao wangeweza kuteuliwa kutoka Upinzani – Lowassa, Lipumba, Mbowe nk, Dk. Slaa yeye anaingia katika kinyang’anyiro hicho akiwa na rekodi safi ya nyuma ya utendaji jimboni na hata alipokuwa ndani ya Bunge. Hadi leo rekodi hiyo haijapata kuchafuliwa na kashfa yoyote ya ufisadi au nyingine yoyote kubwa.

Kama, mpaka sasa, Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inaendelea kuwa mfano wa kuigwa nchini wa halmashauri zinazochacharika kuwaletea wananchi wake maendeleo makubwa, ni kwa sababu ya msingi mkubwa wa Dk. Willbroad Slaa aliouweka akiwa mbunge wa jimbo hilo.

Ndugu zangu, kama bunge sasa linachangamka na linasimama kidete kupambana na ufisadi nchini (mfano Escrow), ni kwa sababu huko nyuma kulikuwa na kina Slaa ndani ya bunge hilo waliojitolea “kufa kidogo” kutetea wanyonge na ambao walionyesha ujasiri wa kutoiogopa serikali kwa kuibana kweli kweli. Hawa wa sasa wanafuata tu njia iliyoanzishwa na hao waliowatangulia – yaani Dk. Slaa na wenzake.

Ndugu zangu, nihitimishe kwa kusisitiza mambo mawili. La kwanza ni kwamba Dk. Slaa ndiye aliyestahili kuwa chaguo sahihi la kumkabili Dk. Magufuli, na si Lowassa, Lipumba, Mbowe au Mbatia. La pili ni kwamba kwa kumkubali Lowassa kuwa mmojawao, Chadema na Ukawa ‘wameipoteza’ kabisa agenda ya ufisadi. Itabidi sasa wafunge midomo yao kuzungumzia vita ya ufisadi, kwa sababu sasa Watanzania wanaamini kuwa walikuwa wakibwabwaja tu maneno lakini si waumin wa kweli wa vita hiyo!

Niambieni; ni wapi ambako kuna ushahidi kuwa Lowassa alipata kukubali “kufa kidogo” kuwatetea wanyonge na masikini wa nchi hii. Ni mjinga tu ndiye asiyejua kwamba Lowassa ndiye chaguo la urais la mabilionea wa Tanzania ambao wengi wao mapesa yao hawakuyapata kihalali.

Hakuna namna yoyote ambayo Lowassa anaweza kudai kuwa katika patashika zake za kuusaka urais anawakilisha maslahi ya masikini waliozagaa vijijini! Tiketi yake ni ya mabilionea wenzake na ndiyo atakaowawakilisha kwenye kampeni. Mtu wa namna hiyo akiingia Ikulu, kamwe hawezi kuwakumbuka masikini wala wanyonge bali atawakumbuka mabilionea wenzake waliomwingiza Ikulu.

Rejeeni ile hafla yake ya Arusha ya kutangaza nia ya kuwania urais ilivyokuwa ya mapesa mengi ndo utaelewa ninachomaanisha ninaposema ya kuwa si mwakilishi wa masikini na wanyonge. Na ndiyo maana, kwangu mimi, bado nitaendelea kuamini ya kuwa The Chosen One kutoka Upinzani wa kumkabili Dk. Magufuli alistahili kuwa Dk. Slaa.

Ni bora CCM, ambayo sasa inaanza kujirudi na kujisafisha kwa kuwatosa watuhumiwa wa ufisadi miongoni mwao kuliko Chadema na Ukawa ambao sasa wanapokea makapi ya CCM yanayokimbia tuhuma za ufisadi. Lowassa, kama alivyokuwa mzigo kwa CCM, atakuwa tu mzigo kwa Chadema na Ukawa yao! Time will tell! Tafakari.

Raia Mwema
Toleo la 416
29 Jul 2015-

wanaccm tutampigia kura lowasaaaaaaaaa
 
Hivi Kikwete si alikuwa kwenye List of Shame iliyoandikwa na Tundu Lissu na kusoma na Dr Slaa?
Najua ya kwamba ‘siasa ni mchezo mchafu', lakini bado najiuliza maswali kibao kichwani mwangu ya ni hoja zipi Chadema ilizizingatia katika kumkubali Lowassa – mtu ambaye chama hicho kilimuorodhesha katika ile orodha ya Mwembe Yanga ya watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini – List of shame (orodha ya aibu).

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...utetea-waraka-wa-chadema-list-of-shame-2.html
 
Kinachopiganiwa ni kuondoa mfumo tawala ambao ndio unakumbatia uozo wote huo ikiwemo ufisadi!na impact ya Lowassa kuhamia upinzani ni kubwa zaidi kwa wale wanaopigana kuondoa mfumo huo!ana ushawishi,anajua madudu yanayofanyika ndani ya ccm etc!na ukumbuke nchi nyingi za kiafrica mabadiliko yameletwa na viongozi waliokua kwenye vyama tawala na hatimae kuhamia vyama pinzani kutokana na ushawishi wao!kwa hiyo kwa akili ndogo kabisa naweza kuona kama vile andiko lako halina mashiko kabisa!ni too low ti say the least!!
 
Lowassa ni mgombea binfasi ambaye ameuziwa na nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya Chadema.

Mgombea binafsi huendesha serikali kwa ilani binafsi. Ingawa Lowassa ataanza kuiongea ilani ya ukawa, lakini moyoni mwake ataendelea na ilani yake ya siri. Hata atakapowageuka ukawa atawajibu kuwa "ndio siasa". Ukawa wenyewe wamehalalisha jibu hili.

Mtanzania mpenda mabadiliko ya kweli hawezi kunasa kwenye mtego wa namna hii. Huu mtego ni rasmi kwa wanasiasa wenye siasa kali ambao hawajali taifa linaenda wapi zaidi ya kuangalia maslahi yao ya kisiasa.

Kila jamii itavuna ilichopanda. Tukipanda uchu wa madaraka, tutavuna uchu wa madaraka...
 
Kuna ukweli kwenye hiyo makala kwa sababu muandishi wake ni mtu anaetetea sana upinzani kuchukua madaraka..Hadi kufikia kuandika hivyo ujue kakwazika na wenzake wengi tu.Nilichofurahi kaweka maangalizo ngoja tuone OKTOBA sio mbali uhai ukiwepo..Kuna wangese humu kazi yao ni maneno ya shombo tu hasa wanapoona kuna ukweli wa hoja madhubuti hio sio dawa ya kuua mijadala bali ni ujinga wa kujipa faraja ya muda mfupi tu ambayo haipo.
 
Umenena Mkuu. Tusubiri Oktoba. Kama watu hawatakimbia nchi kwa aibu
 
Lowassa ni mgombea binfasi ambaye ameuziwa na nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya Chadema.

Mgombea binafsi huendesha serikali kwa ilani binafsi. Ingawa Lowassa ataanza kuiongea ilani ya ukawa, lakini moyoni mwake ataendelea na ilani yake ya siri. Hata atakapowageuka ukawa atawajibu kuwa "ndio siasa". Ukawa wenyewe wamehalalisha jibu hili.

Mtanzania mpenda mabadiliko ya kweli hawezi kunasa kwenye mtego wa namna hii. Huu mtego ni rasmi kwa wanasiasa wenye siasa kali ambao hawajali taifa linaenda wapi zaidi ya kuangalia maslahi yao ya kisiasa.

Kila jamii itavuna ilichopanda. Tukipanda uchu wa madaraka, tutavuna uchu wa madaraka...
Upo sahihi uchambuzi wako una mantiki ya kiuhalisia..
 
Tutafakari hapa hivi kwanini hawa CCM wanaumia sana wakati huyu mtu hawamtaki si mwachen aendeeeeeeeeeeee
 
Back
Top Bottom