Pamoja na siasa chafu na rushwa tutashinda Arumeru Mashariki Lema (mb) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pamoja na siasa chafu na rushwa tutashinda Arumeru Mashariki Lema (mb)

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Martin Jr, Feb 23, 2012.

 1. M

  Martin Jr JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  “PAMOJA NA SIASA CHAFU NA RUSHWA TUTASHINDA ARUMERU MASHARIKI”

  Nawasalimu

  Leo asubuhi nimesikia habari za uzushi na majungu kutoka katika gazeti la Chama Cha Mapinduzi Uhuru pamoja na gazeti la serikali la Habari leo . Hivyo basi kilichosemwa na magezeti ya Uhuru na Habari leo ya leo tarehe 23/2/2012 ni uzushi na propaganda , Magazeti haya ya CCM yatatumika sana kipindi hiki kama yalivyotumika kule Igunga yalipojaribu kutaka kuwatenganisha watu hata kwa dini zao lakini baadae ukweli ulijulikana na ikawa aibu kwao .
  Kwa zaidi ya miaka hamsini ya uhuru wa Taifa letu kutoka kwa mkoloni bado Watanzania wa Arumeru sio huru na Watanzania wote kwa ujumla bado wanaishi maisha magumu kama wakimbizi nje ya Nchi yao.
  Ninafahamu wajibu wangu katika kupigania demokrasia safi ya Nchi yangu na wakati huu jimbo la Arumeru Mashariki litakuwa mfano wa mapambano hayo na nitakuwa mstari wa mbele bila hofu wala kumuogopa mtu yeyote na wa cheo chochote katika kupigania ukweli na haki.
  Wajibu wangu na wa chama changu kwa sasa ni kutoa matumaini kwa watu wote wa Taifa letu , na tunazo sababu za msingi za kwenda kushinda jimbo la Arumeru na ni wito wangu kwa kila kijana wa Arumeru anayeishi mjini kuona fursa hii ni kwa ajili ya ukombozi wa Nchi yetu na sio Arumeru peke yake na hivyo kwenda kutoa elimu vijijini tulikoacha wazee wetu.
  Jana nilikuwa Meru , wazee na vijana wamekataa kuburuzwa na siasa za CCM ambazo kwa miaka hamsini ya uhuru wa Nchi hii zimeshindwa kutatua matatizo yao bali kufikiri rushwa ya pesa kipindi hiki cha Kampeni ndio mahitaji yao ya Msingi.
  Nimesikia Tendwa msajili wa vyama vya siasa naye ameanza kusaidia CCM kufanya propaganda chafu labda ni vyema akatambua wajibu wake na sio kuanza kufanya kazi za siasa za CCM ni vyema akajua kuwa yeyote anayeitetea uovu leo itakuwa hasara kwake au kwa familia yake kesho .
  Mwisho . Ninajua macho ya Watanzania yako Arumeru mashariki , Ninawatia moyo wale mlioko mbali lakini mnapenda mabadiliko , sisi tulioko huku tutapambana kwa niaba yenu kufa na kupona kuhakikisha haki, usawa, na demokrasia vinapata thamani halisi bila uhuni wowote kufanikiwa , Msiogope pengine huwezi kabisa kufika Arumeru kusaidia ukombozi basi wewe huko uliko tuombee kwa Mwenyezi Mungu , hakika hatutakubali uhuni ,udhalimu , na Nguvu ya rushwa iwachagulie ndugu zetu wa Arumeru Mbunge , kama Mbunge mmoja wa CCM Mwigulu Nchemba alivyotamba jana pale katika Hotel ya Mount Meru kuwa pesa bado hazijaanza kumwagwa kwani ndio kwanza ziko njiani zinakuja. Hata hivyo Msiogope Udhalimu utashidwa Arumeru ““ Ni Afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu .
  Godbless J Lema (Mb)
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Sema jembeeeeeeeeee!!!!! Umesuuza roho yangu ngoja nikapate pepsi bariiiiiidi.
   
 3. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tunawatakia kila la kheri! hakikisheni mnabana kila kona!
   
 4. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Nilitegemea mwishoni angesema anamfungulia mashtaka Tendwa, anyway tamko linaeleweka kwa kila aliye sawa sawa kumkichwa
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  go Lema go.....Lakini kumbuka kumfungilia jalada Tendwa.
   
 6. N

  NGONYA NM Member

  #6
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakika mh lema Mungu akiwa upande we2 hakuna aliye juu yetu kama uliwezakuzuia tifu lajana mwambie huyo mzinz wa ccm ar ud dar kwan meru sio igunga hawanajinsi yakuwadanganya wameru wote niwasomi hawana shda na vihela vyao wanahtaji m2 makini wakuwawakilisha
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kamanda,umesema magazeti yamepotosha ukweli lakini mbona hujatupa ukweli wenyewe ni upi sasa????????
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  pia kamanda,tupe ukweli kuhusu wewe kufanya vurugu kwenye msiba na hivyo wazee kukupiga marufuku usikanyage arumeru.

  ni hayo tu mkuu ili tuamini kwamba arumeru sio igunga wala uzini
   
 9. k

  kanjanja Member

  #9
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pamoja sana Mh. LEMA
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  MSAJILI wa Vyama vya Siasa, John Tendwa amemshauri Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuwaomba radhi wazee wa kimila wa kabila la Wameru ‘Washiri' vinginevyo hali ni mbaya kwake na kundi lake.

  Tendwa alisema hayo jana kwa waandishi wa habari wakati akizungumzia mambo ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

  Alisema utovu wa nidhamu alioonesha Lema siku ya maziko ya aliyekuwa mbunge wa jimbo
  hilo, Jeremiah Sumari, kiliwakera Washiri na kumtaka asikanyage jimbo hilo wakati wa kampeni.

  Alisema yeye alikwenda katika jimbo hilo kuonanana wakuu wa Serikali na taasisi zake kupanga mkakati wa uchaguzi, lakini ghafla alikutana na wazee hao waliosema mbele yake, kuwa Mbunge huyo wa Arusha Mjini, hawataki kumwona katika kampeni, vingivevyo damu inaweza kumwagika juu yake.

  ''Washiri wamesema hawataki kumwona Lema katika kipindi cha kampeni kwani alileta dharau kubwa na utovu wa nidhamu siku ya maziko ya Sumari, hatua ambayo iliwakera wazee hao … ni busara tu, Lema kwenda kuwaomba radhi wazee hao kama anataka kufanya kampeni ya mgombea wa chama chake- Chadema," alisema Tendwa. Pia Tendwa amesema Lema asipowaomba radhi huenda damu ikamwagika.

  Msajili alivitaka vyama vya siasa kuheshimu mila na desturi za makabila, ili kuepuka umwagaji damu na kushauri kuwa ni vema vyama vya siasa katika kampeni kuzingatia hilo.

  Alisema eneo la Arumeru Mashariki ni tete na lenye ushindani mkubwa wa kisiasa na kutokana na hilo, aliwataka wagombea wa vyama vyote na viongozi katika kipindi cha kampeni, kufuata kanuni na sheria za maadili ya uchaguzi tofauti na hapo hali inaweza kuwa mbaya.

  ''Hatutaki uvunjifu wa amani uwepo kwa kupindisha demokrasia na maadili ya uchaguzi,
  hivyo kila mgombea anapaswa kuzingatia hilo mara moja na vyama vinapaswa kukubali matokeo na si kuchukua sheria mkononi," alisema.

  Msajili alisema; ''ujambazi wa siasa'' hautaruhusiwa katika kampeni za jimbo hilo kama vile
  kupigana risasi na kumwagiana tindikali, kwani ofisi yake kwa kushirikiana na Polisi watakuwa mstari wa mbele kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa kwa asilimia 100.

  Tendwa alisema matusi, udini, jinsia na kashfa, ni kauli zinazopaswa kuepukwa katika kampeni hizo, kwani zinaweza kuleta madhara makubwa ya umwagaji damu na ni kinyume na maadili ya uchaguzi, lakini viongozi
  nao wanapaswa kuziepuka.

   
 11. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  nina matumaini makubwa kuwa kitaeleweka tuu!!
  Maneno haya yamesheheni busara na ushupavu..
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Labda huko hakuna wapiga kura Wamasai na Lowassa asiende. Lakini kama kuna wamasai, unajuwa Laibon wao nani? na akisema kitu huyo hapingwi.
   
 13. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  poa kamanda
   
 14. s

  sirng'udi Member

  #14
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ndo maana huwa nasema chama pekee teule toka mwenyenzi ni CDM kwani kipo kwa ajiri ya kuwakomboa watz ktk janga la umaskini, ujinga na n.k kwa tamko hili la kamanda LEMA nimeamini chadema ni bahari ya majembe yaliyo na makali yakuweza kumkata fisadi yeyote yule akijitokeza na leo hii tayari fisadi/kibaraka tendwa kashakata kwan kashindwa kusimamia dhamana aliyopewa ya kuongoza vyama kama mlezi na wazi wazi kaonekana anawabeba wezi wa rasilimali zetu CCM je huo ndo msingi wa malezi bora? Mm kama mtz mwenye machungu na rasilimali zetu nasema viva peoplez powerrrr a.k.a CHADEMA arm ni jimbo letu kamanda lema ongoza mashambulizi kwan mi naamini wewe ni martin luser king wa tz GOD BLESS U & CHADEMA mwisho wa CCM ndo huu.
   
 15. MALI YA BABA

  MALI YA BABA JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 461
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Pamoja sana kamanda hakuna kulala hadi kieleweke!Pipoooooooz!!!
   
 16. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #16
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Kamanda nenda tupo nyuma yenu hakuna lolote litakalosimama mbele yenu,hii nchi ni mali na tuna kiu kubwa ya mabadiliko
   
 17. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #17
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,297
  Likes Received: 601
  Trophy Points: 280
  Hiki ni kipindi tunachohitaji makamanda aina ya Lema wengi.
   
 18. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #18
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kule hakuna hijabu, mmezoea kuwamwagia watu tindikali mwambieni Mwigulu arudie tena aone wameru watamfanya kitu gani.
   
 19. a

  ashtatu Member

  #19
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  lets wait and see
   
 20. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli Washiri wamesema hivyo, Tendwa alitumwa akamweleze Mh. Lema au akawaleleze wanahabari?
   
Loading...