Pamoja na mambo mengine mchango wa Mwalimu Julius Nyerere uko kwenye vitabu alivyoandika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pamoja na mambo mengine mchango wa Mwalimu Julius Nyerere uko kwenye vitabu alivyoandika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magobe T, Oct 16, 2011.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Ndugu wanaJF, huwa nawaheshimu sana watu wanaopata muda wa kukaa chini na kusoma/kutunga/kuandika vitabu. Kati ya marais wa Tanzania, ni Mwalimu Julius Nyerere tu ndiye aliyekuwa na muda wa kukaa chini/kusoma/kutunga/kuandika vitabu vingi zaidi ukilinganisha na 'successors' wake.

  Ametuachia mchango mkubwa sana na leo hii vitabu vyake vinasomwa na watu mbalimbali duniani kwani maktaba nyingi hazikosi vitabu vyake. Hii inatufundisha nini?
   
 2. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Usemayo ni kweli kabisa. Nyerere hakuwa na muda wa kuongoza kama inavyopaswa, baada ya miaka 25 katuwacha maskini wa kutupwa. Hatuna hata kandambili. Benki kuu kweupeeee. Alikuwa bize kuandika vitabu tu. Sijui ulitegemea nini kutoka kwa Mwalim wa English literature?
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,818
  Likes Received: 83,217
  Trophy Points: 280
  Na miaka 26 ya Mwinyi, Mkapa na Kikwete tumekuwa matajiri? Nchi iko gizani, ajira hakuna, rasilimali zetu chungu nzima zinachukuliwa usiku na mchana na wachukuaji wa rasilimali hizo hata kodi hawalipi, malalamiko ya wananchi kuhusu gharama kubwa za maisha yapo kila kona ya nchi yetu. Je, kuna ahueni yoyote tangu Mwalimu ang'atuke miaka 26 iliyopita? Mwalimu alikuwa bora sana kama kiongozi ukilinganisha na hawa wote waliomfuata ambao juhudi zao kubwa ni kuiangamiza nchi na kujitajirisha wao, familia zao na marafiki wao wa karibu.
   
 4. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Miaka 24 ya uongozi wake nchi haina barabara,maji,umeme,shule,vyuo,hospitali watz tulitembelea katambuga,tulivaa magunia!HIVI ALIYEANGAMIZA NCHI NANI? WA MIAKA 24?au wa miaka 5?
   
Loading...